Ee bwana ninakupenda nakupenda, Ninayo kila sababu baba ya kukupenda
Umenitendea mengi ya ajabu, Hata kulipa siwezi baba pokea sifa

Chorus:
Nakupenda Baba, nakupenda, Kila ninapokutafakari mimi natetemeka
Kwanini unidhamini mimi mwanadamu Ninajua ni kwa neema tu umenipenda
Nakupenda Baba, nakupenda Kila ninapokutafakari mimi natetemeka
Kwanini unidhamini mimi mwanadamu Ninajua ni kwa neema tu umenipenda

Upendo wako kwangu ni maalum, siwezi kulinganisha kamwe nao mwingine
wewe ni wa thamani maishani, Nisaidie nisikuache nisonge mbele

(Chorus)

Asubuhi ninaona fadhili zako, Na mchana ninashuhudia upendo wako
Na usiku ninaona kupumzishwa, Kila wakati mimi naona kufarijika