Chorus:

Mungu baba yeye hafungi macho
Habadiliki jana leo na kesho
Azijua hata na shida

Verse 1:

macho yake makali yaona mambo yote
Hata yale yamefichika anaona
Hamna jambo la siri asiloliona
Umekosa chakula mavazi hata pesa
Kodi ya nyumba karo ya shule hata mchumba
Unadhani sasa dunia imefika mwisho

(Chorus)

Verse 2:

Jirani wacha mirungirungi
Rafiki wacha maneno mengi
Sijui kwanini mwanisema woo…
Ati mimi nimekuwa kafiri
Ati mimi nimekuwa mrogi
Sijui wala sisemi kitu woo…

(Chorus)

Verse 3:

Akisema yuakuona jamani usitie shaka
Ye halali na hachoki na wala ye habadiliki
Azijua raha zako azijua na shida zako
Tuimbeni haleluya hosana ye amefufuka
Haleluya, Ye halali na hachoki na ala ye habadiliki
HAleluya tuimbeni haleluya hosana ye amefufuka

(Chorus)