Hapo mwanzo mungu alimwumba Adamu (In the beginning God created Adam)
Bustani ya edeni aitunze (To care for the Garden of Eden)
Baadaye Mungu aliona sio vyema(Then God saw that it was not good)
Adamu awe pekee yake akampa mke mwema(For Adam to be alone, He gave him a wife)
Hapo mwanzooo(In the beginning)

Chorus:

Mke mwema anatoka kwa Bwana(A virtous wife is from the Lord)
Nimemwomba Mungu nangojea(I have asked God, I am waiting) (x2)
Mke mwema aaa (A virtuous wife…)

Kwa akili zangu ni vigumu kutambua (On my own it is hard to determine)
ni nani aliyeumbwa kwa ajili yangu(Who was created for me)
Katika mabinti wengi ni nani(In the midst of all the women, who is it)
Mungu ndiye anajua mke mwema(It is only God knows who)

(Chorus)

Majukumu yananizidi jamani nachoka
Kazi za ndani haziishi mke sina
Majukumu yananizidi jamani nachoka
Kazi za ndani haziishi kazi sina
Nimeshapika deki, Nguo zangu zote chafu
Nimemaliza kufua, vyombo vyote ndani vichafu
Maharage yanaungulia, ndani maji nimeishiwa
Nimeamini mwanaume bila mke hajakamilika
Nimeamini mwanaume bila mke hajakamilika bado

(Chorus)

Ukitafuta chumba cha kupanga kama hujaoa
Unaweza kuzunguka mpaka ukachoka
Ukitafuta chumba cha kupanga kama hujaoa
Unaweza kuzunguka mpaka ukachoka
Kila nyumba unayokwenda unaambiwa
“Vyumba viko, umeoa? kama hujaoa kaka samahani
Hapa hatupangishi vijana ambao bado hawajaoa.” Oh!

(Chorus)

Advertisements