ILe nyota ya ajabu, yaonekana mashariki
Imejaa ishara zote, za kuzaliwa mfalme
Mamajuzi wako nyuma, kuifuata nyota ile
walifika Yerusalemu, nao wakauliza (repeat)
Yuko wapi yeye aliyezaliwa,
mtawala wa wayahaudi ili tumsujudie
Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana
Walikuwako na wachungaji, waliokaa makondeni
Wakilinda kundi lao kwa zamu usiku
Malaika kawatokea, kawambia msiogope
Maana leo katika Yuda, amezaliwa messiah
(Chorus)
Walipokwisha kusema haya, Malaika wa bwana
Waliimba wimbo ule, wimbo usio na mwisho
Utukufu juu kwa Mungu mbinguni
Duniani we amani kwa aliowaridhia
(chorus)
Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana
Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana
(chorus)
Mar 19, 2023 @ 06:06:30
Mungu akubariki kwa kazi yako!
LikeLike
Aug 12, 2012 @ 17:05:51
What a blessing you are!!! ♥♥
LikeLike
Mar 19, 2023 @ 06:01:42
Nzuri sana
LikeLike