Roho Yangu (My Soul) Hymn Lyrics Sung by Esther Musila and Guardian Angel

Leave a comment


(Sung in Swahili – A Hymn)

Bwana Mungu nashangaa kabisa (O Lord my God, when I in awesome wonder)
Nikifikiri jinsi ulivyo (Consider all the worlds Thy hands have made)
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia (I see the stars, I hear the rolling thunder)
Viumbavyo kwa uwezo wako (Thy power throughout the universe displayed)

Refrain:
Roho yangu na ikuimbie (Then sings my soul, my Savior God, to Thee)
Jinsi wewe ulivyo mkuu (How great Thou art, how great Thou art)
Roho yangu na ikuimbie (Then sings my soul, my Savior God, to Thee)
Jinsi wewe ulivyo mkuu (How great Thou art, how great Thou art)

Nikitembea pote duniani (When through the woods, and forest glades I)
Ndege huimba nawasikia (Wander and hear the birds sing sweetly in the trees)
Milima hupendeza macho sana (When I look down, from lofty mountain grandeur)
Upepo nao nafurahia (And see the brook, and feel the gentle breeze)

(Refrain)

Nikikumbuka vile wewe Mungu (And when I think, that God, His Son not sparing)
Ulivyompeleka mwanao (Sent Him to die, I scarce can take it in)
Afe azichukue dhambi zetu (That on the Cross, my burden gladly bearing)
Kuyatambua ni vigumu mno (He bled and died to take away my sin)

(Refrain)

Yesu Mwokozi atakaporudi (When Christ shall come, with shout of acclamation)
Kunichukua kwenda mbinguni  (And take me home, what joy shall fill my heart)
Nitaimba sifa zako milele (Then I shall bow, in humble adoration)
Wote wajue jinsi ulivyo (And then proclaim My God, how great Thou art!)

Kijito cha Utakaso (River of Cleansing) Lyrics Sung by Guardian Angel

Leave a comment


(Sung in Swahili – A Hymn)

Kijito cha utakaso (The Cleansing River)
Ni damu ya Yesu (Is the Blood of Jesus)
Bwana anao uwezo (The Lord has the might)
Kunipa wokovu (To give me salvation) (Repeat)

Refrain:
Kijito cha utakaso (The cleansing river)
Nizame kuoshwa humo (That I may be immersed and cleansed there)
Namsifu Bwana kwa hiyo (I praise the Lord because)
Nimepata utakaso (I have received the cleansing) (Repeat)

Viumbe vipya naona (I see new creatures)
Damu ina nguvu (For the Blood is powerful)
Imeharibu uovu (It has destroyed the evil)
Ulionidhulumu (That tormented me)

(Refrain)

Ni neema ya ajabu (It is His Great Mighty)
Kupakwa na damu (To be covered by the Blood)
Na Bwana Yesu kumjua (And to know the Lord Jesus)
Yesu wa msalaba (The Jesus of the Cross)

(Refrain)

Mungu Hapokei Rushwa (God Cannot be Bribed) Lyrics by Goodluck Gozbert

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Uzuri ni kwamba, Mungu hapokei rushwa x2
(The good news is that God cannot be bribed)
Angepewa mabilioni, tungetupwa mbali sana x2
(If that was so and he was given billions, we would have been abandoned)
(Repeat)

Na wengine tuna damu mbaya, mabifu kama yote
(Others have bad blood, looking for quarrels)
Mtu hujamkosea, anatamani ufe
(You have not wronged them, but they wish death on you)
Wengine bwana we, tulipewaga sura
(And others, were given looks)
Mtu akikukuona, akalinganisha hufanani
(Someone looks at you, and they compare you with others)
Wewe unadhani angepewa oxygene
(What do you think – if they were given oxygen)
Yangu angeminya, angeminya — nifie mbali
(My oxygen – they would have squeezed it, that I died)
Wewe unadhani angepewa kesho yako wee
(What do you think, if they were given your tomorrow)
Kwanza angefinya, angefinya — ufie mbali
(They would have squeezed it so that you died)

Pre-Refrain:
Ila mungu wee, hajui kukosea (But God does not wrong us)
Ametupa thamani, tulioitwa vikaragosi
(He has given us worth, us who are called cartoons)
Ila mungu wee, mwingi wa huruma
(For God is full of mercy)
Ametupa vicheko, vicheko bila manoti
(He has given us joy, joy without payment)

(Refrain)

Mfano jitu lipate lama za Laiza: lingetuchakaza vibaya
(For example, if someone gets Laiza’s fortune: they would have hurt us)
Au lipate kama za Dangote, Lipewe kuamua Kesho yako eeh
(Or they would be fortunate as Dangote, to judge your tomorrow)
Wengine, Baba zetu walala hoi (For some of us, our Fathers are needy)
Wengine, mama zetu hohehahe (For some of us, our mothers are poor)
Wengine, familia zetu choka mbaya (For some of us, our families are destitute)
Wengine, ndio kabisa mayatima (For some of us, we are complete orphans)
Hakuna anayetujua wala hatuna connection (There would be no one to give us connections)
Kusema sababu ni elimu mbona wasomi kibao ni jobless?
(Saying that it is because of lack of education, why are degree holders jobless?)
Tumewekwa Mahali kwa neema ya Mungu (We have been placed in the place of God’s Grace)
Tunavuka Mapito kwa neema ya Mungu (We have crossed through troubles through God’s Grace)

(Pre-Refrain)

(Refrain)

Mwema (Good) Lyrics by Paul Clement ft. Bella Kombo

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Wema wako, si kwa wakati wa furaha tu
(Your Goodness, is not only present in times of joy)
Wema wako, pia wakati hata wa majonzi
(Your Goodness is also present in times of grief)
Wema wako, haupimiki, kwa majira fulani tu
(Your Goodness cannot be measured in time)
Wema wako, ni kila wakati, na kila nyakati
(Your Goodness is present at all times, in all seasons)
Hata sasa ni mwema, tunapoimba ni mwema
(Even now He is Good; when we sing He is Good)
Tunapolia ni mwema, tunapocheka ni mwema
(When we weep, he is Good; when we laugh, He is Good)
Tunapopanda ni mwema, tunapovuna ni mwema
(When we plant, He is Good; When we harvest, He is Good)

Refrain:
Wewe ni mwema, u mwema, wewe ni mwema
(You are Good, You are Good, You are Good)
Wewe ni mwema, u mwema, wewe ni mwema (Repeat)
(You are Good, You are Good, You are Good)
Unatupenda x2 Wewe ni mwema (Repeat)
(You love us x2 You are Good)

Wema wako, ni kama mchanga, siwezi kuhesabu
(Your Goodness is like the soil; I cannot count it)
Wema wako, ni kama maji, yanayomiminika bila kukoma,
(Your Goodness is like the water; that flows without ceasing)
Mtu akinge, ama asikinge, hayataacha kutoka
(Should someone obstruct it or not, it will not cease)
Hata sasa ni mwema, tunapoimba ni mwema
(Even now, He is Good; When we sing He is Good)
Tunapolia ni mwema, tunapocheka ni mwema
(When we weep, He is Good; when we laugh, He is Good)

(Refrain)

Mungu Mwenye Ishara (God of Signs) Lyrics by Boaz Danken

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Mungu mwenye ishara na maajabu (God of Signs and Wonders)
Twakuinua Mfalme wa wafalme (We lift You King of kings)
Umetamalaki duniani kote (You have reigned over all the earth)
Twakuinua Mfalme wa wafalme (We lift You King of kings) (Refrain)

Ulimwonyesha Musa njia zako (You revealed Your paths to Moses)
Wana Isiraeli matendo yako (The children of Israel Your works)
Ulimpiga Farao kwa mapigo ngumu (You soundly defeated the Pharaoh)
Ukawaokoa watoto wako (You rescued Your children)

Habari zimeenea, madui watetemeka (The word has spread, and the enemies tremble)
Twakuinua Mfalme wa wafalme (We lift You King of kings)
Waliokombolewa wanashangilia (The saved ones rejoice)
Twakuinua Mfalme wa wafalme (We lift You King of kings)

(Refrain)

Imela Chineke Imela
Oh Imela Chineke Imela

Igwe, igwe, igwe!
Oh Igwe, igwe, igwe!

Siyabonga Nkosi, Siyabonga
Oh, Siyabonga Nkosi, Siyabonga

Thank You! Thank You!
Oh, Thank You Jesus Thank You

Ahsante, Yesu ahsante
Oh, Ahsante Yesu ahsante

Older Entries

%d bloggers like this: