Advertisements

Hakuna (Nothing) lyrics by Jemimah Thiong’o

1 Comment(Sung in Swahili)

Hakuna linalomshinda,(Nothing is impossible to Him)
Yesu mkombozi wangu (Jesus my Savior)
Soma Bibilia utaona,(Read the Bible and you shall see)
Yote Bwana Yesu anaweza(All that Jesus is able to do)
Hakuna lililo ngumu kwake anaweza(Nothing is impossible to him)

Chorus:

Hakuna, hakuna,(Nothing, nothing)
Hakuna linalomshinda (Nothing is impossible to Him)
Yote bwana yesu anaweza (Lord Jesus is able to do all)
Aliwatoa jasho makuhani (He awed the pharisees)
Na wazee hekaluni (And the elders at the temple)

Magonjwa yakulemea, (Illness is overwhelming you?)
Yesu aliponya hata ukoma (Jesus cured even leprosy)
Vipofu viwete na viziwi (The blind, the lame and the deaf)
Bwana yesu aliponya (All of them Jesus healed)
Isitoshe alifufua lazaro anaweza(He even raised Lazarus from the dead)

(Chorus)

Ulevi umekulemea, (Is drunkedness overwhelming you?)
Aligeuza macho kuwa divai (He turned water into wine)
wapoteza macho kwa kumikumi, (You lose your sight from cheap spirits)
Waelekea poteza maisha (You’ll end up losing your life)
Ukimwamini hautaona kiu ya pombe (Believe in Him and you won’t thirst for alcohol)

(Chorus)

Hakuna linalomshinda, (Nothing is impossible to Him)
Njaa kwa yesu sio tisho (Famine to Jesus is not a threat)
Aliwapasha elfu tano kwa mikate miwili (He fed 5000 with 2 loaves)
Kabaki kuokota elfu saba (And had seven basketfuls of leftovers)

(Chorus)

Hakuna linalomshinda, (Nothing is impossible to Him)
Baada ya kutufia msalabani (After He died for us on the cross)
Aliingia kuzimu yesu, (Jesus entered Hell)
Kanyang’anya shetani funguo (And wrested the keys from Satan)
Kampa ibilisi tetemeko kubwa sana (And caused the devil to fear.)

Advertisements

Mwambie (Tell Him) Lyrics by Jemmimah Thion’go

Leave a comment(Sung in Swahili)

Verse 1:
Mwambie Baba shida zako maana yeye atazitatua
(Tell father your troubles for he will solve them)
Ukiwaambia majirani ye, masimango yatakufuata
(If you tell your neighbors, gossip will follow you)
Mwambie Yesu upitiayo maana yeye ayajua yote
(Tell Jesus your troubles for He knows all)
Alishinda kifo Masiya, nini pia asoweza shinda
(The Messiah defeated death, what will thwart him?)

Chorus:
Mwambie, mwambie, mwambie Baba shida zako
(Tell him, tell him, tell the Father your troubles)
Mwambie, mwambie, yote alikusikiza
(Tell him, tell him all he listens)
Mwambie, mwambie, mwambie Baba shida zako
(Tell him, tell him, tell the Father your troubles)
Mwambie, mwambie, Yeye atazitatua
(Tell him, he will solve them)

Verse 2:
Ee mama unajisumbua, washika tama una huzuni
(You woman hold your chin in depression)
Unakosema juu ya shida zako we huwaambia majirani
(When you tell of your troubles you tell your neighbors)
Usiende kwa waganga, hawatosimamisha ndoa yako
(Don’t go to the witch-doctors: They won’t help your marriage)
Mwambie Yesu shida zako, waganga wataivunja
(Tell Jesus your troubles, Witch-doctors will break it)

(Chorus)

Verse 3:
Usiwaambie walimwengu, yakusumbuayo ndugu yangu
(Don’t tell the world whatever troubles you my brother)
Yesu pekee ndiye aweza kuitatua shida yako
(Jesus only would help solve your troubles)
Mbona wasumbuka bure ukitafuta ushauri mwenzangu
(Why do you trouble yourself looking for solutions?)
Hebu soma hiyo Biblia, ina jawabu kwa kila jambo
(Read that Bible, it has a solution for every question)

(Chorus)

Mganga (Healer/Physician) by Jemmimah Thiong’o

Leave a comment(Sung in Swahili)

Nawatangazia mganga wangu Yesu, Ayeyeyeye
(I declare to you, that my healer is Jesus)
mganga wa kweli eh, njoni niwaonyeshe
(The true healer he, let me show you)

Chorus:
Mimi nimemwona (mganga), nimemwona (mganga)
(I have seen Him (the physician), I have seen Him (the physician)
Nimemwona (Mganga wa waganga ni Yesu).
(I have seen Him (the Great Physician is Jesus)

Verse 1:
Nasema nimemwona. Mganga wa waganga
(I say I have seen the Great Physician)
Anayeinamiwa na waganga wote hata na wachawi pia
(That is worshipped by all physicians and even witch-doctors)
Wanaleta madawa yao hata na hirizi
(They bring their medicine, and even their charms)
Na wanatangaza maovu yote walotendea wanadamu
(And they confess the evil they did to men)
Huyu mganga, kazaliwa Bethlehemu
(This Great Physician was born in Bethlehem)
Kalelewa na  na zarati la ajabu ni mwana wa bikira
(And came by a great miracle – he is the son of a virgin)

(Chorus)

Verse 2:
Jina la huyu mganga, kwa kweli lanishangaza
(The name of this Physician, is awe inspiring)
Kwa maana linalo nguvu nyingi kama mganga mwenyewe
(Because it has as much power as the Physician Himself)
Lilipotajwa na Petero, Tabitha akafufuka
(When it was said by Peter, Tabitha was raised from the dead)
Kiwete njiani akatembea kwa ajili la hilo jina
(The cripple by the road walked because of that name)
Paulo na Sila wakasifu kwa hilo jina
(Paul and Silas worshiped by that name)
Milango ya gereza ikafunguka kwa jina la mganga Yesu
(The doors of the jail opened because of the Physician Jesus)

(Chorus)

Verse 3:
Nguo za huyu mganga, hata nazo zina nguvu
(This Physician’s clothes, have power too)
Mama aliyevuja damu alipenya katitati ya umati
(The woman with bleeding passed through the crowd)
Nguvu za upinde wa nguo, damu ikakatika
(Through the power of the hem, the bleeding stopped)
Yesu akamwambia imani yako ndiyo imekuponya
(Jesus told her that her faith was what healed her)
Baada ya kusulubiwa, nguo za huyu mganga
(And after his cricifixion, this Physician’s clothes)
Hazingepasuliwa kwa bei yake ikapigiwa kura
(Because of its value would not be torn; instead they cast lots for it)

(Testimony)

(Chorus)

Akisema Atakubariki [Mwenye Baraka] lyrics by Jemimah Thiong’o

1 Comment


Chorus:
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote

Verse 1:
Akisema atakubariki, wala usitie shaka
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
Mipango yake ya ajabu, tena haibadiliki
Akisema atakuinua, ndiye mwenye kuinua
Akisema atakupa mtoto, katika umri wowote
Aliwapa Sara na Ana, lipi asiloweza

(Chorus)

Verse 2:
Akisema atakubariki, watoto wako waelimike
Wapate na shahada nyingi, hakuna atakayezuia
Akisema utapona, hakuna atakayezuia
Mama aliyetokwa na damu alipona na kazi(?) yake
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
Atalinda afya yako, maana yeye ndiye mwenye afya

(Chorus)

Verse 3:
Watembelea miguu, hata baisikeli huna
Akisema uendeshe Musso, kesho utaendesha
Waishi nyumba ya matope, huna hata mavazi
Akisema atakubariki, majirani watashangaa
Akisema atakuinua, mbele ya adui zako
Atakuandalia meza ule unywe wakitizama

(Chorus) (repeat)

Amenipanda Lyrics by Jemimah Thiong’o

Leave a comment


Chorus:
Bwana asema, amenipanda mimi
Kando ya mito yenye maji mengi
Bwana asema, amenipanda mimi
Kando ya mito yenye maji mengi

Verse 1:
Ni Bwana alonipanda, kwa mikono yake Baba
Kando ya mito yenye rehema na baraka
Kunipalilia Baba, sikosi mbolea maji
Naishi nikiamini, siwezi nyauka nimepandwa ee

(Chorus)

Verse 2:
Kweli Baba wa rehema, amenipanda mimi
Baraka zanifuata kokote niendako
Amenipa uhai, akalinda afya yangu
Ndiposa nashuhudia, sifa alozipanda Mungu wangu

(Chorus)

Verse 3:
Imani ya wokovu, Hushinda majaribu
Hiyo ni baadhi ya mito nilopandwa kwayo
Mambo yangu yote baba, hupanga kwa utaratibu
Kwa maana anijali, aliyenipanda Mungu wangu wee

(Chorus)

Verse 4:
Hakuna juu mbinguni, wala chini duniani
Anayeshinda Mungu muumba mpanzi wangu
Hunizunguka mimi, kwa damu ya mwanao
Hunilinda vyema, sipati madhara kwani nimepandwa ee

(chorus)

%d bloggers like this: