Watu Wote (All People) Lyrics by Kambua

Leave a comment(Sung in Swahili)

Watu wote, pazeni sauti (Lift up your voice, all people)

Mwimbieni Bwana wimbo mpya enyi watu wote (Sing to God a new song all people)
Mwimbieni Bwana nchi zote kwani astahili (Sing to God all countries, he is worthy)
Mwimbieni Bwana viumbe vyote pazeni sauti (Sing to God all creatures, lift up your voices)
Mwimbieni Bwana, yeye ni mkuu (Sing to the Lord, He is great)

Chorus:
Watu wote, paza sauti sifu Bwana (All people, lift up your voices and praise the Lord)
Viumbe vyote, sifuni Bwana astahili (All creatures, praise God he is worthy)
Kwa vifijo, na kwa shangwe, vigelegele, sifu Bwana (With shouts, praise and ululation, praise the Lord)
Kwa vifijo, na kwa shangwe, vigelegele, sifu Bwana (With shouts, praise and ululation, praise the Lord)

Malangoni mwako naingia na shukrani (I enter his gates with thanksgiving)
Nyuani mwako sifa nitaimba (Within your walls I will sing praise)
Nitashuku nitahimidi jina lako (I wall thank and lift your Name)
Jina lililo kuu kuliko yote (The name that is above all names)

(chorus)

Let everything that has breath praise the Lord
Let everything that has breath praise the Lord
Let everything that has breath praise the Lord
Let everything, let everything

(chorus)

Advertisement

Maneno (Words) Lyrics by Betty Bayo

3 Comments(Sung in Swahili)

Chorus:
Maneno, ya kinywa changu (The Words of my mouth)
Wacha yatawaliwe, na wewe Bwana (Let them be ruled by you Lord)
Maneno, ya kinywa changu (The Words of my mouth)
Wacha yatawaliwe, na wewe Bwana (Let them be ruled by you Lord)

Verse 1:
Ninaponena, juu ya maisha yangu (When I speak of my life)
Ninene ya baraka, si kulaani (Let me speak for blessings not curses)
Nimebarikiwa, imeinuliwa (I have been blessed, I have been lifted up)
Maana kunayo nguvu, katika maneno (Because there is power in words)
Ingawaje, hali nilioko (Even though my current situation)
Ni ya kuhuzunisha, na kuhangaisha (Is pitiful and desperate)
Nitabiri mema, tena mazuri (Let me prophesy good things)
Maana kunayo nguvu, katika maneno (Because there is power in words)

(Chorus)

Verse 2:
Kazi, ya mikono yangu (The work of my hands)
Wacha ibarikiwe, na wewe Bwana Let it be blessed by you Lord)
Niamkapo, na nilalapo (When I awake, and when I sleep)
Wacha nilindwe, na wewe Bwana (Let me be guarded by you Lord)

(Chorus)

Verse 3:
Bwana naomba, yote nisemayo (Lord I pray, that all I say)
Uwe umenipaka, yawe baraka (Should be annointed, and be a blessing)
Uimbaji wangu, utawaliwe nawe (My singing, Let it be ruled by you)
Ninene yote, yawe baraka (So that all I say, will be a blessing)

(Chorus)

Wewe Pekee (You Alone) by Alice Kamande

3 Comments

Nafungua kinywa changu, nikusifu Baba (I open my mouth, to praise you father)
Umenitendea nimefika sasa hapa (You have done good for me so far)
Wewe kweli ni rafiki, Unaniongoza ninapopotea (You are my friend, leading me when I am lost)
Upendo wako niufananishe na nani baba  (What can I compare your Love to?)

Taabu nyingi kweli nilipitia (I passed through a lot of troubles)
Hadi nikajipata nikikushuku (Until I found myself doubting you)
Sikujua mpango wako kwangu Baba (I was not aware of your plans for me father)
Ulijua yote nikiyapitia (You knew everything I passed through)
Mkono wako ulikuwa umenishikilia nisianguke (Your hand was holding me so I could not fall)
Wewe kimbilio langu (You are my salvation)

Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako (There is no other, just you)
Mbele hata nyuma, ni wewe pekee (Ahead or behind me, just you)
Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako (There is no other, just you)
Mbele hata nyuma, ni wewe pekee (Ahead or behind me, just you)

Tafuta tafuta hutampata kama yeye (Search and search, you will not find like him)
Alinitoa toka tope la dhambi (He saved me from the mud of sin)
Kama sitaona haya ya kumsifu mungu wangu (Therefore I am not afraid to praise my God)
Siku zote nitamuimbia Baba (All my days I will sing for my father)

Taabu nyingi kweli nilipitia (I passed through a lot of troubles)
Hadi nikajipata nikikushuku (Until I found myself doubting you)
Sikujua mpango wako kwangu Baba (I was not aware of your plans for me father)
Ulijua yote nikiyapitia (You knew everything I passed through)
Mkono wako ulikuwa umenishikilia nisianguke (Your hand was holding me so I could not fall)
Wewe kimbilio langu (You are my salvation)

Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako (There is no other, just you)
Mbele hata nyuma, ni wewe pekee (Ahead or behind me, just you)
Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako (There is no other, just you)
Mbele hata nyuma, ni wewe pekee (Ahead or behind me, just you)

Ebenezer by Angela Chibalonza

20 Comments

(Languages: Swahili, Lingala)

Umbali tumetoka, na mahali tumefika
(Thus far we have come from, and where we are now)
Ndio maana ninatambua, kwamba wewe ni ebeneza
(It is why I confess, that you are Ebenezer)
Sio kwa uwezo wangu,ila ni kwa uwezo wako
(It is not because of my might, but by yours)
Mahali nimefika, acha nikushukuru
(Thus far I have reached, let me thank you)
EE Bwana umenisaidia, nifike mahali nimefika
(Oh Lord you have helped me, to reach where I am)
Bwana wewe ni ebeneza, maishani mwangu oo
(Lord you are the Ebenezer in my life)

Refrain:
Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako
(I want to build on you Ebenezer)
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu
(I want you Ebenezer to be my foundation)
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana
(My cornerstone, I desire you so much)
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana
(My precious rock, I need you so much)
Oo Ebeneza, jiwe langu (Oh Ebenezer, my rock)

Ninataka maisha yangu, yajengwe juu yako
(I want my life, to be founded on you)
NInataka ndoa yangu, ijengwe juu yako baba
(I want my marriage, to be founded on you)
Ndoa zilizojengwa juu yako yahwe, hazivunjiki kamwe
(because marriages built on you, can never be broken)
Nyumba zilizojengwa juu yako yahweh hazivunjiki kamwe
(Homes founded on you Yahweh, can never be broken)
Ninataka uimbaji wangu baba, ujengwe juu yako
(I want my singing Father, to be founded on you)
Maana wewe ni sauti yangu, wewe ni uzima wangu
(For you are my voice, you are my life)

(Refrain)

Ebeneza na nga (My Ebenezer)
Libanga na ngai ya talo (My Precious Stone)
oleki diamant mpe wolo papa eh kati na bomoyi na ngai
(You are worth more than diamonds and gold, Father, in my life)
Nzambe nakumisi yo (Lord, I praise You)
Moko te akokani na yo oh oh (No one compares to You)
Bisika nakomi lelo Yawe ezali nse na makasi na yo
(It is thanks to You that I am where I am today)
Aleluya Nzambe na ngai (Alleluia, My Lord)

(Refrain)

Ebenezer ni jiwe langu, jiwe langu la msingi
(Ebenezer is my rock, my cornerstone)
Mahali nimefika leo, Ni kwa ajili yako ebeneza
(Thus far I have come, is because of you Ebenezer)
Mawe mengi yako hapa chini ya jua
(There are a lot of rocks under the sun)
kuna dhahabu, kuna almasi Kuna mawe hata sijui majina yake
(There is gold, there is diamond, and others I can’t name)
Lakini hakutawahi kuwa jiwe kama ebeneza
(But there will never be a rock like Ebenezer)

Nainua Macho Yangu (I Lift My Eyes) by Masha Mapenzi

2 Comments(Sung in Swahili)

Chorus:
Nainua macho yangu, niitazame, nitazame milimani
(I lift up my eyes and look to the hills)
Msaada, msaada wangu we watoka wapi Ee ni kwa baba, ni kwa baba
(Where does my help come from? From the Father)
Nainua macho yangu, niitazame, nitazame milimani
(I lift up my eyes and look to the hills)
Msaada, msaada wangu we watoka wapi Ee ni kwa baba, ni kwa baba
(Where does my help come from? From the Father)

Asema njoo, njoo, asema njoo upate pumziko
(He says come, come to my rest)
Asema njoo, jongea, asema njoo upate pumziko
(He says come, come to my rest)
Fadhili zangu ni za milele, huba langu halina kikomo
(My mercies and love are forever)
Mimi ndimi simba wa yuda, mimi ndimi ngome yako
(I am the Lion of Judah, and your stronghold)

(Chorus)

Heri awe nawe, awe nawe, heri awe nawe, mambo yote shwari
(It is good for him to abide in you, and everything will be peaceful)
Heri awe nawe, awe nawe, mambo yote shwari, mikononi mwake
(It is good for him to abide in you, and everything in his hand will be peaceful)
Viumbe vyote vyamtukuza, Mchana kutwa usiku kucha
(All creation praise him, day and night)
Yeye ndiye muweza yote, hakuna limshindalo Mola
(He is all in all, nothing defeats God)

(Chorus)

Older Entries

%d bloggers like this: