Nasonga Mbele (I’m Pressing On) Lyrics by Kelsy Kerubo ft. Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Nimeshapata (I have received) x2

Tangazo, tangazo kwa mapepo na wajumbe wako (Announcement to the devil and his messengers)
Mimi sirudi nyuma kamwe (I will never turn back)
Mmapetuli nao nawapa habari (I have an announcement to the detractors)
Walisema sitasonga, mi nasonga mbele (They said I will be stuck, but I’m pressing on)
Huyu Yesu, ni mwache niende kwa nani? (This Jesus, if I leave Him, where would I go?)
Huyu Yesu, mimi namtazamia juu juu (This Jesus, I will continually look up to Him)

Refrain:
Nasonga mbele, kama mgambo (I’m pressing onward, like a ranger)
Sirudi nyuma, sirudi nyuma kamwe (I do not turn back, never do I turn back)
Nainua macho yangu juu (I lift up my eyes)
Mawazo yangu yote juu (All my thoughts are of on high)
Kila kitu changu chote juu kwake (All my plans are on Him)
Ananipenda! (For He loves me!)

Hivi ni nini kitachonifanya nimwache Mungu (For what can lead me to abandon God?)
Mbele nisiendelee, nigeuke nyuma nimwache? (To stop moving forward, to turn back and leave him?)
Ikiwa ni dhiki, magonjwa, vifungo havitaweza (Neither distress, nor sickness, nor sentencing will make me)
Aliye ndani yangu ni mkuu, ataniwezesha (For the One who lives within me will make me successful)

Hakuhesabu udhaifu wangu (He did not count my weaknesses)
Hakuchukulia tena kwa hasira (He was not angered by me)
Yeye alinibariki bado (He still blessed me)
Hakuwasikiza wal’o leta mashitaka yangu kwake (And did not listen to my accusers)
Kama Ayubu, alitetea bado (Like Job, he defended me)
Yeye Hakimu wa kweli (For He is a just judge)
Hapewi rushwa anajua haki zangu (He cannot be bribed, he knows my rights)

(Refrain)

Sifikirii kushindwa (I do not ponder my defeat)
Sina ndoto ya kuchoka (I do not dream of my exhaustion)
Ataniwezesha (For He will enable me)

Wapo wengi wenye chuki na kero (There are many with hatred and annoyance)
Waliponikera, yeye akapigana (When they troubled me, He fought for me)
Wapo wengi walinipa masaa (There are many that counted my days)
Kwenye wokovu leo wanashangaa (They are now surprised with my salvation)
Kweli kweli alisema, ataandaa meza yangu (Truly He said, He will prepare my table)
Mbele yao maadui, leo wanaboba (Before my enemies, now they are confused)

(Refrain)

Watasubiri wangojee (They will wait and wait)
Watangoja washangae (The will wait and be surprised)
Kwani yeye Bwana (For the Lord)
Atanipeleka juu (Will take me higher)

Advertisement

Kama Mbaya, Mbaya (If It’s Bad, So Be It) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Kama mbaya mbaya (If It’s Bad, So Be It)
Wacha iwe mbaya (Let it be bad)
Tuliwatendea mema/wema (We did them good)
Wakatulipa mabaya (But they repaid us with evil) (Repeat)

Kama mbaya mbaya (If It’s Bad, So Be It)
Wacha iwe mbaya (Let it be bad)
Tuliwaona wabora (We saw them as better)
Kumbe hawafai(But they are not suitable) (Repeat)

Walitunywesha kikombe cha uchungu (They let us drink from the cup of bitterness)
Na maumivu makali (And great pain)
Wakachukua/wakatwaa nafsi zetu (They took our bodies)
Wakazigonga misumari (And crucified them) (Repeat)

Sasa wameyakanyaga (Now they have been trod on)
Wacha Mungu ashughulike nao (Let God take care of them)
Wamevavanya (They have been tested)
Wacha mbingu zishughulike nao (Let the heavens deal with them) (Repeat)

Kama mbaya mbaya (If It’s Bad, So Be It)
Wacha iwe mbaya (Let it be bad)
Tulitenda mema (We did good)
Wakatulipa mabaya (But they repaid us with evil) (Repeat)

Sasa wameyakanyaga (Now they have been trod on)
Wacha Mungu ahangaike nao (Let God take care of them)
Wamevavanya (They have been tested)
Wacha mbingu zishughulike! (Let the heavens take care of it) (Repeat)

Mene mene… tekeli perez (Mene, mene, tekel, parsin)
Kiganja kimeandika, fukuza upesi (The finger has written, chase it away)
Mkono umeandika, fukuza upesi (The hand has written, chase it away)
Kwenye mawe kimeandika, fukuza upesi (It has written on stone, chase it away)
Ukutani kimeandika, watoke upesi (It has written on the wall, for them to get out quickly)
Ofisini kimeandika, rarua upesi (It has written in the office, to be quickly torn)
Kwa wafalme kimeandika, komesha kabisa (To the kings it has written, to stop them completely)
Kwa wakuu kimeandika, rarua upesi (To the rulers it has written, to be quickly torn)
Kwa wenye nguvu kimeandika, komesha kabisa (To the powerful, it was written, to be stopped completely)

Mene tekeli perezi, fukuza upesi (Mene, tekel, parsin, quickly chase them)
Porini waweka mafisi, wakale manyasi (They have placed hyenas in the forest to eat the grass)
Mene tekeli perezi, fukuza upesi (Mene, tekel, parsin, quickly chase them)
Porini waweka mafisi, wakale manyasi (They have placed hyenas in the forest to eat the grass)

Wapigwe! Wapigwe! Waweka mafisi (Let them be destroyed! The hyena keepers)
Wapigwe! Wapigwe! Wakose nafasi (Let them be destroyed! Let them lose their places) (Repeat)

Kanyaga kanyaga kanyaga kanyaga, kanyaga! (Step on them!)x?

Tuipakue (Let us Serve it) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Asali ya Mungu Baba (The honey of Father God)
Tuipakue (Let us serve it)
Asali ya kanani (The honey of Canaan)
Tuipakue, tuipakue-pakue (Let us serve it)

Tumewaacha na maboga yao (na maboga) (We have left them with their vegetables)
Ona wamebaki na matango yao (na matango) (Look they are left with their pumpkins)
Hao Wamisiri na pilau lao (na pilau) (The Egyptians with their pilau)
Tumewaacha na uchawi wao (na uchawi) (We have left them with their witchcraft)
Ona wamebaki na miungu yao (na miungu) (Look they are left with their gods)
Tumewaacha na ushamba (na ushamba) (We have left them with their old ways)
Ona wamebaki na ushamba (na ushamba) (Look, they have remained with their old ways)
Tumewaacha mbali sana (mbali sana) (We have left them far behind)

Wakichungulia, hawatuoni (When they peep at us, they don’t see us)
Wakitutafuta, hawatuoni (When they look for us, they don’t see us)
Hata kwa tunguri, hawatuoni (Even by magic, they don’t see us)
Hata kwa tunguri, hawatuoni (Even by scrying, they don’t see us)
Hata kwa Uchawi, hawatuoni (Even by witchcraft, they don’t see us)
Hale-Halelujah

Moto umewaka, vita vimekwisha (The fire has started, the war is over)
Ushindi tumepata, mbingu zimefunguka (We have won, the heavens have opened)
Tumepiga Kambi, tunataka ushindi (We have set our camp, We want Victory)
Sisi hatushindwi, Mungu wetu ni fundi (We are not defeated, Our God is a tactical expert)

Repeat: Tuipakue, tuipakue-pakue (Let us serve it)
Asali tumeiona (We have seen the honey) x2
Tuipakue na masega yake (Let us serve with its honeycomb)
Wachungaji njooni (Servants of God, come)
Twende tuteke mateka (Let’s go and take captives)
Wayunani wamekimbia (The Greeks have run away)
Wahitti wamekimbia (The Hittites have run away)
Ona Wakanani wamekimbia (The Cannanites have run away)
Waamori wamekimbia mbali (The Amorites have run away)
Twende tuteke mateka sana (Let us take captives)
Ona asali tumeona (We have seen the honey)
Mungu ametushindia (God has won for us)
Mungu ametutendea (God has done for us)

Repeat: Teremka! (Descend!)
Kajua kali, jua kali (Warm sunshine)
Amani ile (The peace)
Furaha tele, furaha tele (Abundant joy)
Ona uzima ule (The everlasting life)
Maziwa yale (The milk)
Asali tele (Abundant honey)
Mafanikio tele (Abundant prosperity)
Ushindi ule (The victory)
Uzima ule (The everlasting life)

Asali tumeiona (We have seen the honey)
Leteni na masufuria (Bring the pots)
na vikombe (And cups)
Na tujilambe (We can lick our fingers)
Masahani yako wapi? (Where are the plates?)
Akina mama mko wapi? (Women, where are you?)
Kina baba twendeni? (Men, shall we go?)
Asali na tujilambe (Abundant honey, we can lick our fingers)

Repeat: Teremka! (Descend!)
Kajua kali, jua kali (Warm sunshine)
Amani ile (The peace)
Furaha tele, furaha tele (Abundant joy)
Ona uzima ule (The everlasting life)
Maziwa yale (The milk)
Asali tele (Abundant honey)
Mafanikio tele (Abundant prosperity)
Ushindi ule (The victory)
Uzima ule (The everlasting life)

Hainidhuru (I Will Not Be Harmed) Lyrics by Irene Robert ft Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Hainidhuru kama nasafiri kwenye bahari (I’m not harmed though I sail)
Ya mawimbi kwani Yesu ni nahodha wangu (On stormy seas, for Jesus is my captain)
Atanifikisha bandarini (He will guide me safely to the harbor)
Japo misukosuko yaniandama (Though troubles follow me)
Hainidhuru kwani nahodha yuko kwenye chombo (They do not harm me, for the pilot is in the ship)
Sikatai, kodi ya nyumba nimekosa (I do not deny that I do not have any money for rent)
Na watoto, ada shuleni walifukuzwa (The children were sent from school for lack of fees)
Na maadui wakiongezeka wakinijia (Though my enemies increase in number)
Bado hainidhuru, nitakuwa salama (I am not harmed, I shall be safe)

Najua niko doro mfuko wangu zero, hainidhuru bado (I know I no purpose and money; but I am not harmed)
Bado nazichangachanga pesa, mambo yatakuwa sawa (I am still struggling to raise money, it shall be well)
Usiku ukiwa mrefu, asubuhi yaja (Though the night is long, dawn arrives)
Shida hazikwamishi safari yangu (Troubles do not hinder my way)
Ushindi wangu uko mbele yangu, naamini (I believe that my victory is ahead of me)

Refrain:
Repeat: Bado, bado hainidhuru (Yet I will not be harmed)
Japo shida nyingi zinanikumba (Though I encounter many troubles)
Matatizo mengi natahadhika (Many problems follow me)
Nahodha wangu Yesu, yuko kwenye chombo (My pilot Jesus, is on duty)
Ananiongoza, atanifikisha (He leads me, he will get me there)

Ingawa ni jioni, lazima nifike kule (Though it is night, I shall arrive there)
Yesu mtuliza barahi atanifikisha kule (Jesus the calmer of seas will get me there)
Baraka zangu lazima nishike nimiliki mie (I must claim my blessings)
Sivurugwi, nasema sitishwi (I am not troubled, I am not disturbed)
Kwa mateso sivurugwi, kwa kelele bado sitishwi (I am not disturbed by troubles and shouts)

Kwa giza ije mishale, ije mateso yaje, potelea mbali (Though arrows and troubles come by night)
Magonjwa nayo kusongwa sana havitabadilisha, ukweli wa mambo (Though sickness and troubles come, they’ll change nothing)
Sivurugwi, na tena sitishwi (I am neither troubled nor distrurbed)
Kwa mateso sivurugwi, kwa kelele tena sitishwi ( am not disturbed by troubles and shouts)

Namwamini namwamini, Mungu wa ajabu (For I believe the Awesome God)
Ananipeleka, ananipeleka, Eh Kanani (The one who will guide me unto Caanan) (Repeat)

(Refrain)

Siki na Sifongo (Vinegar and Sponge) Lyrics by Rose Muhando

1 Comment


(Sung in Swahili)

Refrain:
Siki na sifongo (Vinegar and sponge)
Aliteswa, imekwisha (He was persecuted, it is finished) (Repeat)
Eloi, eloi, eloi (My God, my God, My God)
Sabakhtani? imekwisha (Why have You forsaken me? It is finished) (Repeat)

Ee Mungu wangu, mbona (Oh my God, why) x2
Umeniacha? (Have You forsaken me?)
Ile kazi uliyonituma Baba (The task you set me Father)
Kazi ya kubeba msalaba (The work of carrying the cross)
Imekwisha (It is finished)
Ile kazi uliyonituma Baba (Father, the task you set for me)
Kazi ya kukomboa ndugu zangu (The work of saving my brethren)
Bwana imekwisha (Lord, it is finished)
Hebu tazama vidonda vyangu (Look at my wounds)
Tazama na maumivu yangu (Look at my pain)
Imekwisha (It is finished)

Kati ya mashtaka ya ulimwengu (In the midst of the world’s accusation)
Ila mtenga binadamu na Mungu (And the separator of man and God)
Ilichorwa kwa kalamu nyekundu (That was written in red ink)
Nimeifuta kwa damu yangu (I have erased with my blood)
Leo imekwisha (Today it is finished)
Mikononi mwako, naiweka roho yangu (In your hands, I have placed my spirit)
Sasa imekwisha (Now it is finished)
Nimeunyima nini ulimwengu? (What have I held from the world?)
Ufalme wangu si wa ulimwengu (My kingdom does not belong to the world)
Ona imekwisha (Look, it is finished)
Sasa ninawaleta ndugu zangu (Now I bring with me my brethren)
Mimi nakwenda kwa Baba yangu (I go to my Father)
Kazi imekwisha (My work is finished)

(Refrain)

Nimekwisha wakomboa ndugu zangu (I have saved my brethren)
Mimi nimeushinda ulimwengu (I have defeated the world)
Imekwisha (It is finished)
Mimi ndimi njia kweli na uzima (I am the way the truth and the life)
Nakwenda kwangu sitaki lawama (I go to my home blameless)
Kazi imeisha (My work is finished)
Wenye shida na magonjwa inukeni (Those with troubles and illness arise)
Nasema kwangu njooni (I say come to me)
Nitawapumzisha (And I shall give you rest)
Wacha pazia za hekalu zipasuke (Let the curtains of the temple tear)
Watatifu wasalimike (For the saints to be spared)
Kazi imekwisha (The work is finished)
Nakutangazaia msamaha Yuda (I declare forgiveness to you, Judah)
Kwa kifo changu nilikupenda (In my death I loved you)
Ona imekwisha (See, it is finished)

(Refrain)

Older Entries

%d bloggers like this: