Utamu wa Yesu (The Sweetness of Jesus) Lyrics by Rose Muhando

4 Comments(Sung in Swahili)

Lile lile…

Acheni muone utamu wa Yesu we (Let me show the sweetness of Jesus)
Mama we onjeni utamu wa Yesu we (Come and taste the sweetness of Jesus)
Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we (I have tasted the sweetness of Jesus)
Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we
(See my joy, I have tasted the sweetness of Jesus)
Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we
(I’m not crazy, it is the sweetness of Jesus)
Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we
(I am not mad, but it’s the sweetness of Jesus)
Utamu we, nimeonja utamu we x2 (The sweetness, I have tasted the sweetness)

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2 (The sweetness, I have tasted the sweetness)
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2 (The sweetness of Jesus)
Utamu we, utamu x3 (The sweetness)
Utamu wa Yesu we, he (The sweetness of Jesus)
Mwemere, mwemere x4 (?)

Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti (A lot of pleasures lead to death)
Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio (A lot of pleasures lead to tears)
Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio (Others are pleasurable but lead to tears)
Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri (Are pleasurable but end in bitterness)
Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu (Are pleasurable but end with disease)
Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we (The are pleasurable, but only fleetingly)
Acheni niuseme utamu wa Yesu we (Let me testify on the sweetness of Jesus)
Wacheni nisifu utamu wa Yesu we (Let me praise the sweetness of Jesus)
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
(It has separated us from sin, the sweetness of Jesus)
Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we
(It cannot be compared to honey, the sweetness of Jesus)
Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we
(It’s value exceeds that of a diamond, the sweetness of Jesus)
Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani he
(It is a rare jewel that cannot be bought)
Bali kwa njia ya msalaba tumepewa utamu wa Yesu we
(But by the way of the cross, we have been given the sweetness of Jesus)
Mbinguni tunakwenda bure, uzima tunapata bure
(To heaven we go for free, we are given eternal life for free)
Wokovu tumepata bure, amani tunapata bure
(We have been given free salvation, peace we find for free)
Utamu we, nimeonja utamu we x2 (The sweetness, I have tasted the sweetness)

(Chorus)

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
(It has separated us from sin, the sweetness of Jesus)
Usione tuna raha, tumeonja utamu wa Yesu we
(We are joyful as we have tasted the sweetness of Jesus)
Usione tunacheka, tumeonja utamu wa Yesu we
(We laugh as we have tasted the sweetness of Jesus)
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
(It has separated us from sin, the sweetness of Jesus)
Umetusogeza karibu na Mungu, utamu wa Yesu we
(brought us close to God, the sweetness of Jesus)
Dhambi zetu zimewekwa mbali na Mungu, utamu wa Yesu we
(Our sins are forgiven, the sweetness of Jesus)
Walio chini wameinuliwa, utamu wa Yesu we
(The last are first, the sweetness of Jesus)
Badala ya kilio ni kicheko, utamu wa Yesu we
(Joy instead of tears, the sweetness of Jesus)
Badala ya aibu utukufu, utamu wa Yesu we
(Praise instead of shame, the sweetness of Jesus)
Mito ya baraka inatiririka, utamu wa Yesu we x2
(The springs of blessings flow, the sweetness of Jesus)
Utamu we, nimeonja utamu we (The sweetness, I have tasted the sweetness)

(Chorus)

Mkitaka magari mazuri, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be blessed with cars, taste first the sweetness of Jesus)
Mkitaka majumba mazuri, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be blessed with houses, taste first the sweetness of Jesus)
Mkitaka kubarikiwa, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be blessed, taste first the sweetness of Jesus)
Mkitaka kuinuliwa, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be lifted, taste first the sweetness of Jesus)
Utamu we, nimeonja utamu we (The sweetness, I have tasted the sweetness)

(Chorus)

Sing’oki ng’o, kwa Yesu sing’oki ng’o x4 (No, I will not leave Jesus)
Utamu we, utamu x3 (The sweetness)
Utamu wa Yesu we (The sweetness of Jesus)

Nipishe Nipite (Let Me Pass) by Rose Muhando

2 Comments(Sung in Swahili)

Nakuuliza shetani umepata wapi mamlaka
(I ask you devil, where did you get the permission)
Ya kukamata akili za watu ah! (To mess with people’s minds)
Wewe umeleta balaa umeingia makanisani
(You’ve brought trouble, you have gotten into churches)
Umekamata wababa wanabaka watoto wao
(You have made fathers to rape their children)
Umekamata vijana umewatwika ulevi
(You have caught young men, and saddled them with alcoholism)
Bila kusahau kina mama, vikao vya masengenyo
(Not forgetting mothers, and their gossip)
Sasa nimechoka na mambo yako (I’m tired of your work)
Ewe shetani, nipishe nipite (You Satan, let me pass)

Chorus:
Wewe ulimwasi Mungu, nipishe nipite (You who defied God, let me pass)
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite
(You deceived Adam and Eve, move and let me pass)
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako
(The world is destroyed, for your cunning)
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite (You who defied God, let me pass)
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite
(You deceived Adam and Eve, move and let me pass)
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako
(The world is destroyed, for your cunning)
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu (
You Satan you’ve been ordered, the host of hell)
Sasa nipishe nipite (Now let me pass)

Hebu nipishe nipite, ninachelewa njiani (Let me pass, I’m getting late)
Yesu yu karibu kurudi, kulichukua kanisa
(Jesus is almost returning to take his church)
Kanda unayo nionyesha yote yamepitwa na wakati
(Whatever you show me has been passed by time)
Huna ujanja (You can’t fool me)
Kumbuka miaka elfu mbili iliyopita zamani (Remember 2000 years ago)
Yesu aliposhuka kuzimu, akakunyanganya funguo
(When Jesus descended to hell, and took the keys)
Funguo za mamlaka (The keys of authority)
Nasema nimechoshwa na mambo yako (I say I am tired of you)
Wewe shetani nipishe nipite (You devil, let me pass)

(Chorus)

Nakuamuru shetani wewe, nipishe nipite (I order you Satan, let me pass)
Wewe umekuwa ni kikwazo kwangu, Kufika mbinguni
(You have been my barrier to heaven)
Muda wako umeshakwisha, songea nipite (Your time is up, let me pass)
Sasa haleluya naenda mbinguni, hakuna mashaka
(Now Hallelujah I’m going to heaven, no worries) (Repeat)

Wewe ulishaaniwa, laana milele (You have been cursed forever)
Ulinyanganywa mamlaka na Yesu, Huna ujanja ee
(You’re authority was taken by Jesus, you have no more cunning)
Simba wa yuda aliponguruma, mafuriko kuzimu
(When the Lion of Judah roars, there is flood in hell)
Sasa haleluya twaenda mbinguni, hatuna mashaka
(Now hallelujah we are going to heaven, no worries) (Repeat)

(Chorus)

Heshima (Respect) Lyrics by Annastazia Mukabwa And Rose Muhando

2 Comments(Sung in Swahili)

Refrain:
Wanaokudharau siku moja watakusalimia kwa heshima
(Those who despise you, one day will greet you with respect)
(repeat)

Mateso yako ni ya muda tu, Mungu akuandalia ushuhuda
(Your troubles are only for a time, God is preparing a testimony for you)
Daudi Alikuwa mchunga kondoo, Mungu akamwinua kuwa mfalme
(David was a shepherd, God lifted him to be a king)
Leo unaitwa ombaomba, kesho utaitwa mbarikiwa
(Today you are called a beggar, tomorrow you will be called blessed)
Licha unatembea kwa miguu, kesho utaendesha gari
(Inspite of walking, tomorrow you will drive a car)

Chorus:
Nasema watakusalimia, kwa heshima (I say they will greet you, with respect)
Watakusalimia, kwa heshima (They’ll greet you with respect)
Wakati wako wako wa kuinuliwa, ukifika (When your time to be lifted, has come)
Watakusalimia, kwa heshima (They will greet you, with respect)
Wakati wako wa kubarikiwa, ukifika (When your time to be blessed, arrives)
Watakusalimia, kwa heshima (They’ll greet you with respect)
Wakati wako wa kukumbukwa, ukifika (When your time to be remembered arrives)
Watakusalimia, kwa heshima (They’ll greet you with respect)

Wanaosema hautaolewa, watashuhudia ndoa yako
(Those who say you will not be married, will witness your wedding)
Pale utakapovalishwa pete, watashikwa na kigugumizi
(When you are given a ring, they will be speechless)
Wanaosema wewe ni tasa, watakuona ukinyonyesha
(Those who say you are barren, will see you breastfeeding)
Na Mungu alimkumbuka Sara, hata wewe utakumbukwa
(God remembered Sarah, he will remember you as well)

(Chorus)

Wakuu wa Mungu wetu ni Ebeneza, hata sasa yupo
(Our great God is Ebenezer, even now he is here)
Msaada wetu wa karibu, mwite ataitika
(Our close help, call him and He’ll answer)

Jifunze kuwa na subira, utafanikiwa
(Teach yourself to be patient, and you will succeed)
Sana siku sio gani mama, atakuinua
(Not for much longer mother, he’ll lift you up)
Ona leo wanakuita kikaragosi, kesho watakuita bosi
(Look today they call you useless, tomorrow they’ll call you boss)
Aliyekunyima kadi za harusi, kesho wataomba shela yako
(Those who denied you an invitation, tomorrow will beg for crumbs)
Ona leo wanakupiga kibuti, kesho watakupigia saluti
(Today they kick you out, tomorrow they’ll salute you)

Watakusalimia, kwa heshima (They’ll greet you with respect)
Watakupigia magoti, ukifika (They’ll kneel before you, when you arrive)
Watakusalimia, kwa heshima (They’ll greet you with respect)
Walikuona ukilala jalani, ukifika (They saw you sleeping on rubbish, when you arrive)
Kesho watakupata ofisini, kwa heshima (Tomorrow they’ll find you in your office with respect)
Watakusalimia, ukifika (They’ll greet you when you arrive)
Watakusalimia, kwa heshima (They’ll greet you with respect)
Watakupigia saluti, watakusalimia kwa heshima.
(They’ll salute you, they’ll greet you with respect)

Zinzilela Lyrics by Annastazia Mukabwa ft. Rose Muhando with English Translation

Leave a comment


Nzilenzilela makata na muye, nzilenzilela nzilenzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Ee Bwana nakuinua, nikikumbuka ulikonitoa
(Oh Lord I lift you up, when I remember where you saved me from)
Kwenye maisha ya aibu, na kunifanya wa thamani
(From the life of shame, and made me valuable)
Ee Bwana nakuinua,nikikumbuka ulikonitoa
(Oh Lord I lift you up, when I remember where you saved me from)
Kwenye maisha ya aibu, na kunifanya wa thamani
(From the life of shame, and made me valuable)
Kama si wewe ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani
(Where would I be if not for you, What would I be called?)
Ningelikuwa nimekufa mimi, kwenye shimo la uharibifu
(I would have been lost, in the hole of corruption)
Kama si wewe ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani
(Where would I be if not for you, What would I be called?)
Ningelikuwa nimekufa mimi, kwenye shimo la uharibifu
(I would have been lost, in the hole of corruption)

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Ni wengi niliyowajua, wenye mapesa na utajiri
(I knew a lot of people with money and riches)
Wenye majumba ya kifahari, lakini leo hawako tena
(With elaborate mansions, but they are not there today)
Ni wengi niliyowajua, wenye mapesa na utajiri
(I knew a lot of people with money and riches)
Wenye majumba ya kifahari, lakini leo hawako tena
(With elaborate mansions, but they are not there today)
Lakini mimi wanilinda bure, si kwamba nimetenda mema baba
(But you freely secure me, not because I have done good works father)
Bali ni kwa neema yako, ndio maana mimi naishi
(But I live because of your grace)
Sio ni kwamba nimetenda mema baba, ila ni kwa neema yako
(Not because I have done good works father, but because of your grace)
Ndio maana mimi naishi, Wacha nikutuze wewe
(That is why I am alive, so let me praise you)

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Siwezi kukulipa baba, kwa yale umenitendea
(I cannot repay you father, for all you have done for me)
Bali naomba moyoni mwangu, nipe moyo wa kukupenda
(But I pray in my heart, that you would give me a loving heart)
Siwezi kukulipa baba, kwa yale umenitendea
(I cannot repay you father, for all you have done for me)
Bali naomba moyoni mwangu, nipe moyo wa kukupenda
(But I pray in my heart, that you would give me a loving heart)
Niondolee kiburi baba, nipe moyo mnyenyekevu
(Remove pride from me father, give me a humble heart)
Ili nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu
(So that I live for you, all the days of my life)
(Remove pride from me father, give me a humble heart)
Ili nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu
(So that I live for you, all the days of my life)

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Nyota ya Ajabu lyrics by Rose Muhando

1 Comment


ILe nyota ya ajabu, yaonekana mashariki
Imejaa ishara zote, za kuzaliwa mfalme
Mamajuzi wako nyuma, kuifuata nyota ile
walifika Yerusalemu, nao wakauliza (repeat)
Yuko wapi yeye aliyezaliwa,
mtawala wa wayahaudi ili tumsujudie

Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana

Walikuwako na wachungaji, waliokaa makondeni
Wakilinda kundi lao kwa zamu usiku
Malaika kawatokea, kawambia msiogope
Maana leo katika Yuda, amezaliwa messiah

(Chorus)

Walipokwisha kusema haya, Malaika wa bwana
Waliimba wimbo ule, wimbo usio na mwisho
Utukufu juu kwa Mungu mbinguni
Duniani we amani kwa aliowaridhia

(chorus)

Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana
Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana

(chorus)

Older Entries Newer Entries

%d bloggers like this: