Wanyamazishe (Silence Them) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Refrain:
Wazamazishe Bwana, wafunge midomo Yesu (Silence them Lord, Jesus close their mouths)
Wazamazishe Bwana, wafunge midomo Yesu (Silence them Lord, Jesus close their mouths)
Wapofushe macho yao wasinione (Blind their eyes to my presence)
Wakae mbali nami, ah! wasinione (That they stay far from me, oh! that they may not see me)

Kwa kuwa walitangaza msiba juu yangu (For they prophesied tragedy over me)
Wala hawakutaka ipone nafsi yangu (Nor they did not want me to heal)
Wakafanya sherehe kupitia jina langu (They celebrated over my name)
Waliona fahari kutangaza mauti yangu (They saw pride in announcing my death)
Wakachuma na pesa kupitia jina langu (They made money through my name)
Hawakuona vibaya kuumiza familia yangu (They did not see it wrong to hurt my family)
Walifanya dhihaka kudhihaki watoto wangu, ah! (They ridiculed my children, ah!)

Namtuma malaika nyumbani kwao ( I’m sending an angel to their homes)
Atangaze msiba kwenye familia zao (To announce grief in their families)
Namtuma Gabrieli malangoni kwao (I’m sending Gabriel to their gates)
Atangaze msiba malangoni kwao (To announce grief in their gates)
Nawafanye matanga maishani mwao (And they have mourning in their lives)
Natangaza msiba kwenye malango yao (I announce grief in their gates)
Natangaza matanga nyumbani kwao (I call upon mourning in their homes)
Yasikome matanga kwenye familia zao (May their families mourn unceasingly)
Laana, kifo, iwe juu yao (Curses, death, to be over them)
Wala wasiwe salama watoto wao (Nor should their children be safe)
Mauti iwe fungu lao (May death be their portion)
Kushindwa kuwe mbele yao (Defeat be before them)
Kwa kuwa mimi nimekutumaini (For I have depended upon You)

Wanyamazishwe (May they be silenced)
Watayaharishwe (May they be scattered)
Wafedheheshwe (May they be embarrassed)
Wahangaike (May they worry)
Waaibishe (May they be ashamed)
Kwa kuwa mimi nimekutumaini, eh! (For I have trusted in You, eh!)

(Refrain)

Makaeili wa vita, nakutuma kwao (Michael of War, I sent you to them)
Upeleke mafarakano kwao (Take discord to them)
Wasilielewane wao kwa wao (That they may not understand each other)
Nasema wagombane wao kwa wao (I say that they may argue against each other)
Walane watafunane wao kwa wao (They eat and chew each other)
Wavurugane wao kwa wao (That they disrupt each other)
Maadui wapigane wao kwa wao (The enemies to fight each other)
Mungu mwenyezi awe adui yao (God Almighty be their enemy)
Wakitazama kulia wamwone Gabrieli (When they look to the right, they see Garbriel)
Wakitazama kushoto, wamwone Mikaeli (When they look to the left, they see Michael)
Mbele yangu wamwone Rafaeli (Before me, they see the Archangel Rafael)
Wafadhaike (That they may be dismayed)
Watayarie (That they may be scattered)
Wahangaishe (Worry them)
Waburekishe ( ..?..)
Watayahariki, Usiwape nafasi (That they may be scattered, do not give them space)

(Refrain)

Advertisement

Vice Versa Lyrics by Size 8 Reborn and Rose Muhando

1 Comment


(Sung in Swahili)

Nakushukuru Mungu we, ewe Mungu we
(I thank you God, You God)
Nakushukuru Mungu we, nimeona mkono wako
(I thank you God, for I have seen Your Hand)
Kama si wewe Mungu we, ewe Mungu we
(If it wasn’t for You, God)
Kama si wewe Mungu we, singefika hapa nilipo
(If it wasn’t for You, I would not have been where I am)

(Repeat)

Nilipopita kati ya uvuli wa bonde la mauti na kuzimu
(When I pass through the valley of the shadow of death)
Uliniona Yesu (Jesus You watch over me)
Nilipopigwa na maadui, wakanishambulia
(When my enemies target me and attack me)
Uliniona Yesu (Jesus You watch over me)
Shetani aliposimama, ili anifanye mawindo
(When Satan stands so that he hunts me)
Ulinificha Yesu (Jesus You hide me)
Marafiki wangu walitabiri maanguko yangu
(When my friends prophesy my failures)
Umeniinua Yesu (You have lifted me, Jesus)

Wewe Mwamba wangu, wewe nguvu yangu
(You are my rock, You are my strength)
We amani yangu, kimbilio langu
(You are my peace, my Refuge)
Msaada wangu, watosha!
(My Helper, You are enough!)

(Refrain)

Mbwa mwitu walipiga kelele, nikaziba masikio
(When wild dogs howl, and I close my ears)
Nilikuona Yesu (I saw You Jesus)
Walipanga mipango ya uovu, ili niangamie
(They plotted evil plans, that I may perish)
Ukapangua Yesu (You confused the plans, Jesus)

Mipango, mawazo, walionikusudia
(The plans and the thoughts You intend for me)
Wamepanga, umepanguwa, imekwenda vice versa
(They planned, you unplanned them, it has gone vice versa)
(Refrain)

Kama vice versa (Like vice versa)
Uongo vice versa (Falsehoods, vice versa)
Uchawi vice versa (Witchcraft, vice versa)
Fitina vice versa (Intrigues, vice versa)
Masengenyo vice versa (Gossip, vice versa)
Nimeshinda! (I have overcome!)

(Refrain)

Utukuzwe (Be Praised) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ee Mungu utukuzwe, milele na milele (Oh God be praised forevermore)
Tena uinuliwe, katika mataifa yote (And be lifted up in all nations)
Ee Mungu utukuzwe, milele na milele (Oh God be praised forevermore)
Ee Mungu uinuliwe, milele na milele (Oh God be lifted forevermore)
Tena uhimidiwe katika mataifa yote (And be worshiped in all nations)
Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko (Your awesome name; terrifies than a lion) x2
Wala haufanananishwi na chochote (You cannot be compared with anything else)
Jina lako Baba la ajabu (Lord, your name is awesome)

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika) (You hit a rock, and water sprang forth)
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia) (In the desert, you opened a way)
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania) (When confronted, you fought for them)
Wakafika (Kule Kanaani salama) (You led them safely to Canaan) (Repeat)
Usifiwe, utukuzwe (Be praised, be magnified) (x2)
Utukufu ni wako, milele na milele (All glory belongs to you forevermore)(Repeat)

Haya visiwa na viimbe (Let the seas sing)
Mito na ipige makofi (The rivers to clap in praise)
Ndege na waseme amina kubwa (The birds to say a big amen)
Wanyama wa mwitu wasifu (The wild animals to praise) (Repeat)

Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana(The Lord reigns, you Lord)
Heshima na enzi ni vya Bwana (Honor and dominion are the Lord’s)
Utukufu na nguvu ni vya Bwana (Glory and Might are the Lord’s)
Umeketi mkono wenye nguvu (You who sit on the mighty hand) (Repeat)

(Refrain)

Heshima ni yako (milele na milele) (All honor is yours, forevermore)
Utukufu ni wako (milele na milele) (All glory is yours, forevermore)
Heshima ni yako (milele na milele) (All honor is yours, forevermore)
Mamlaka ina wewe (milele na milele) (Dominion is yours, forevermore)
Malaika waimbe (milele na milele) (Let the angels sing, forevermore)
Wazee ishirini na nne waseme (milele na milele) (And the 24 elders say, forevermore)
Na wale wenye uhai waimbe (milele na milele) (Let all the living sing, forevermore)
Na watakatifu waseme (milele na milele) (And all the Holy to say, forevermore)

(Refrain)

Mungu Wa Mapendo (God of Love) Lyrics by Rose Muhando

1 Comment(Sung in Swahili)

Nini kitanitenganisha (na upendo wa Mungu Baba)
(What can separate me, from the Love of God the Father)
Ikiwa ni dhiki au njaa (Havitananitenga naye Baba)
(Neither hardship nor famine, shall separate me from the Father )
Mauti, upanga, na dhihaka (Havitananitenga naye Baba)
(Death, war and danger, will not separate me from the Father)
(Repeat)

Chorus:
Sina hofu sibabaiki (I’m not afraid, not worried)
Kwake yeye nime/nitashinda (I have/shall won/win)
Milele yote nime/nitashinda (Forever I have/will win/won)
Tena zaidi ya kushinda (Even more than win)
Kwake yeye aliyenipenda (In Him who loved me)
(Repeat)

Kwenye zamu yangu nitasimama (When my turn comes I shall stand)
Kwa miguu yangu nitasimama (On my feet I shall stand)
Nione Bwana atakavyonijibu mimi (To see what the Lord shall say to me)
Kwa habari ya kulalamika kwangu (Regarding my persecutions)
Bwana aliniambia neno hili (As the Lord had promised me)
“Usiogope maneno yao (“Do not fear their words,)
Usitetemeke mbele yao, (Do not tremble before them)
usifadhaike mbele yao (Do not despair before them )
Maana imeandikwa, kwa ajili yako ninauawa (As it is written, I was killed for your sake)
kama kondoo wa kuchinjwa, kifo nimehesabiwa (Like a lamb to slaughter, in your death you were counted)
Kifo nimehesabiwa, mimi sibabaiki (In my death I have been counted, I am not worried)

Bridge:
Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue) (Satan, do not bother me)
Wala usinibababishe (Wala usinibababishe) (Do not worry me)
Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke) (Be quiet and begone)
Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke) (Be silent and be gone in the name of Jesus)
Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee) (Be quiet and begone)

(Chorus)

Milele neno la Mungu limehakikishwa (Forever the word of God has been established)
Tena ni ngome kwa wamwaminio (It is a fortresses to the believers)
Tena ni ngao kwa wamwitao Baba (Also a shield for those who call him Father)
Kabla ijawa misingi ya dunia, (Before the foundation of the world)
Yeye huyu alikuweko (He was here)
(?), muumba wa utukufu ([?], Creator of glory)
Na utakaso wa dhambi, (?) (And the cleansor of sin, (?))
Nami kwake ni wa mwana x2, ni wa mwana (I belong to the son)

(Bridge) + (Chorus)

Asifiwe Mungu wa mapendo (God of love be praised)
Asifiwe Mungu wa huruma (God of mercy be praised)
Asifiwe Mungu wa amani (God of peace be praised)
Asifiwe Mungu wa mapendo (God of love be praised)

Asifiwe Mungu wa mapendo (God of love be praised)
Ametenda maajabu, (He has done amazing things)
dunia ishangilie (Let the world rejoice)
Visiwa(?) vitoe nyimbo, (All islands  give praise)
Asifiwe Mungu wa mapendo (God of love be praised)

Mungua chukua heshima yako (Gpd receive your honor)
Mungu chukua utukufu wako (God receive your praise)

Asifiwe Mungu wa mapendo (God of love be praised)
Ametenda maajabu, (He has done amazing things)
dunia ishangilie (Let the world rejoice)
Visiwa(?) vitoe nyimbo, (All islands  give praise)
Asifiwe Mungu wa mapendo (God of love be praised)
(Repeat)

Utamu wa Yesu (The Sweetness of Jesus) Lyrics by Rose Muhando

5 Comments(Sung in Swahili)

Lile lile…

Acheni muone utamu wa Yesu we (Let me show the sweetness of Jesus)
Mama we onjeni utamu wa Yesu we (Come and taste the sweetness of Jesus)
Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we (I have tasted the sweetness of Jesus)
Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we
(See my joy, I have tasted the sweetness of Jesus)
Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we
(I’m not crazy, it is the sweetness of Jesus)
Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we
(I am not mad, but it’s the sweetness of Jesus)
Utamu we, nimeonja utamu we x2 (The sweetness, I have tasted the sweetness)

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2 (The sweetness, I have tasted the sweetness)
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2 (The sweetness of Jesus)
Utamu we, utamu x3 (The sweetness)
Utamu wa Yesu we, he (The sweetness of Jesus)
Mwemere, mwemere x4 (?)

Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti (A lot of pleasures lead to death)
Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio (A lot of pleasures lead to tears)
Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio (Others are pleasurable but lead to tears)
Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri (Are pleasurable but end in bitterness)
Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu (Are pleasurable but end with disease)
Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we (The are pleasurable, but only fleetingly)
Acheni niuseme utamu wa Yesu we (Let me testify on the sweetness of Jesus)
Wacheni nisifu utamu wa Yesu we (Let me praise the sweetness of Jesus)
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
(It has separated us from sin, the sweetness of Jesus)
Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we
(It cannot be compared to honey, the sweetness of Jesus)
Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we
(It’s value exceeds that of a diamond, the sweetness of Jesus)
Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani he
(It is a rare jewel that cannot be bought)
Bali kwa njia ya msalaba tumepewa utamu wa Yesu we
(But by the way of the cross, we have been given the sweetness of Jesus)
Mbinguni tunakwenda bure, uzima tunapata bure
(To heaven we go for free, we are given eternal life for free)
Wokovu tumepata bure, amani tunapata bure
(We have been given free salvation, peace we find for free)
Utamu we, nimeonja utamu we x2 (The sweetness, I have tasted the sweetness)

(Chorus)

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
(It has separated us from sin, the sweetness of Jesus)
Usione tuna raha, tumeonja utamu wa Yesu we
(We are joyful as we have tasted the sweetness of Jesus)
Usione tunacheka, tumeonja utamu wa Yesu we
(We laugh as we have tasted the sweetness of Jesus)
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we
(It has separated us from sin, the sweetness of Jesus)
Umetusogeza karibu na Mungu, utamu wa Yesu we
(brought us close to God, the sweetness of Jesus)
Dhambi zetu zimewekwa mbali na Mungu, utamu wa Yesu we
(Our sins are forgiven, the sweetness of Jesus)
Walio chini wameinuliwa, utamu wa Yesu we
(The last are first, the sweetness of Jesus)
Badala ya kilio ni kicheko, utamu wa Yesu we
(Joy instead of tears, the sweetness of Jesus)
Badala ya aibu utukufu, utamu wa Yesu we
(Praise instead of shame, the sweetness of Jesus)
Mito ya baraka inatiririka, utamu wa Yesu we x2
(The springs of blessings flow, the sweetness of Jesus)
Utamu we, nimeonja utamu we (The sweetness, I have tasted the sweetness)

(Chorus)

Mkitaka magari mazuri, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be blessed with cars, taste first the sweetness of Jesus)
Mkitaka majumba mazuri, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be blessed with houses, taste first the sweetness of Jesus)
Mkitaka kubarikiwa, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be blessed, taste first the sweetness of Jesus)
Mkitaka kuinuliwa, onjeni utamu wa Yesu we
(You want to be lifted, taste first the sweetness of Jesus)
Utamu we, nimeonja utamu we (The sweetness, I have tasted the sweetness)

(Chorus)

Sing’oki ng’o, kwa Yesu sing’oki ng’o x4 (No, I will not leave Jesus)
Utamu we, utamu x3 (The sweetness)
Utamu wa Yesu we (The sweetness of Jesus)

Older Entries

%d bloggers like this: