Niloweshe (Drench Me) Lyrics by Sarah K

Leave a comment

(Sung in Swahili)

Refrain:
Niloweshe, niloweshe, Roho mtakatifu
(Drench me, Holy Spirit drench me)
Niloweshe, niloweshe, nakuomba Roho, niloweshe
(Drench me, Spirit I pray that you may drench me)

Roho mtakatifu, niloweshe (Holy Spirit, drench me)
Kwa maombi, na kufunga, niloweshe (In my prayers and fasting, drench me)
Nisipungukiwe, nisijue nikakauka (That I may not lack, that I may not be dry)
Nakuomba Roho, niloweshe (Spirit I pray that you may drench me)

(Refrain)

Roho mtakatifu, niloweshe (Holy Spirit, drench me)
Kwa upako wako, niloweshe (Drench me with Your anointing)
Nisipungukiwe, nisijue nikakauka (That I may not lack, that I may not be dry)
Nakuomba Roho, niloweshe (Spirit I pray that you may drench me)

Roho mtakatifu, niloweshe (Holy Spirit, drench me)
Kwa ushirika wako, niloweshe (Drench me with Your Fellowship)
Nisipungukiwe, nisijue nikakauka (That I may not lack, that I may not be dry)
Nakuomba Roho, niloweshe (Spirit I pray that you may drench me)

(Refrain)

Advertisement

Yote Mema (All Good) Lyrics by Joel Lwaga

Leave a comment(Sung in Swahili)

Mema (Good) x4 (Repeat)

Ni rahisi kukusifu (It is easy to praise You)
Wakati wa mazuri (In good times)
Ni rahisi kukushukuru (It is easy to thank You)
Yanapotokea mema (When good happens)
Ila ni ngumu kuamini (But it is difficult to believe)
Kuwa hata na magumu (To be in tough times)
Nawe Mungu umeyaruhusu (God You have allowed them)
Kwa kuniwazia mema (For thinking well of me)

Refrain 1:
Umeruhusu mazuri (You have permitted good)
nifurahi tena nikushukuru (For me to rejoice and to be thankful)
Na mabaya ili niwe hodari (And bad times that I may be strong)
Na tena nikusifu (And to praise You as well)
Mbele umeniwekea fahari (You have saved my triumph for me)
Haya ni ya muda tu (This is only temporary)
Macho yangu yatazama mbali (My eyes see ahead)
Uliko utukufu (Where there is holiness)

Refrain 2:
Yote mema (It is all well) x2
Hata magumu yana sababu (Even my difficulty has a reason)
Yote mema (It is all well) x2
Sitala humu, sitakufuru (I shall not eat here, I shall not blaspheme)

Sasa nimejua kuwa (I have now understood)
Wewe uliyenipa samaki (That the one who provides fish for me)
Ndiwe pia umetaka wakati mwingine (You also want other times )
Nipate nyoka (To receive a snake)
Tena nimejua kuwa wewe (I have also understood that You)
Uliyenipa mkate (Who provided bread for me)
Ndiwe pia umetaka (You are the same who wants)
Wakati mwingine nipate jiwe (For me to receive stones some times)

(Refrain 1 + 2)

Nimejifunza kuwa na shibe tena (I have taught myself to be satisfied again)
Nimeju kuwa na njaa tena (I have taught myself to be hungry again)
Kuwa nacho hata kutokuwa nacho (To have and not to have)
Najua yote yanafanya kazi (I know that all have a purpose)
Ili kunipatia mema (For good for me)
Yamefanyika kama ngazi iiamini kupanda (They have been fashioned like a ladder to be climbed by faith)

(Refrain 2)

Mema (It is well) x4 (Repeat)

Nikumbushe Wema Wako (Remind Me of Your Goodness) Lyrics by Angel Benard

Leave a comment

(Sung in Swahili)

Ni rahisi kinywa kujawa na lawama tele
(It is easy for the mouth to be filled with blame)
Pale mambo yanapoonekana hayaendi
(Whenever things do not go to plan)
Ni ajabu sana kama moyo unahangaika (kutafuta majibu)
(It is amazing how the hearts frets searching for answers)
Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka
(Amazing how the heart shows doubt)
Ya kwamba japo Mungu anaishi ndani yangu (kuna muda nahofu)
(Even though God lives in me, I am still afraid)
Japo kuwa Mungu anaketi kati yetu, kuna muda na hofu
(Though God sits amongst us, there is time that I doubt)
Nakumbuka wana waIsraeli katika bahari ya shamu
(I remember the Israelits at the Red Sea)
Japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi
(Though they passed in the middle in victory)
Kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwana
(With many songs they sung in praise of the Lord)
Lakini baada kuvuka na kuliiona jangwa (yalibadilika mambo)
(But after crossing and seeing the wilderness, things changed)
Manunguniko yalisimama (Murmurms started)
Na kusahau miujiza alotenda Bwana mwanzo
(And forgetfulness on the miracles the Lord did at the beginning)
Ee Mungu nisaidie (Oh God help me)

Refrain:
Nikumbushe wema wako nisije laumu
(Remind me of Your goodness so I that do not blame)
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
(Remind me of Your greatness in challenging times)
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
(Remind me of you testimonies that I might praise You)
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
(To sing a song of praise in the midst of tears)
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
(To sing a song of praise in the midst of tears)
(Repeat)

Nisaidie kukumbuka Baba ya kwamba umenichora kiganjani mwako
(Lord help me to remember that you have drawn me on your palm)
Kati ya wengi waliopo duniani eh, na mimi umeniona
(In the midst of many on earth, You have seen me)
Nikumbushe Baba, ya kwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa
(Remind me Father, that You healed me when I was ill)
Ya kwamba ni wewe, mlipaji wa ada yangu shuleni
(That it is You, the payer of my school fees)
Ya kwamba kama ungeniacha hatua moja nisingelifika nilipo
(That had you left me even in one step, I would not have been here)
Ee Baba, Umekung’uta mavumbi, kung’uta mavumbi mimi na kuniheshimisha
(Oh Father, you have wiped my dust and honored me)

(Refrain)

Bwana Yesu nakutazama, ninakuabudu
(Lord Jesus I look to You, I worship You)
Mungu wa maisha yangu, nisaidie nisalalamike mbele zako
(God of my Life, help me not to complain before You)
Katika hali zote nijue upo
(In any situation to know that You are there)
Umesema hutaniacha, ee Yahweh
(You have said You would not leave me, Oh Yahweh)
Haya ni maombi yangu (This is my prayer)

Tabu zangu (My Troubles) lyrics by Rose Muhando & Annastazia Mukabwa

13 Comments(Sung in Swahili)

Haleluya naitazamia mbingu mpya na nchi mpya
(Halelujah I look to the new heaven and earth)
Huko nitapumzika milele (There I will rest forever)

Taabu zangu zikiisha, nitamwona Bwana wangu
(When my troubles are over, I will see my Lord)
Akinikaribisha kule, karibu upumzike
(When he welcomes me there, “welcome to the rest”)
Hapa ndipo nyumbani kwako, hapa ndipo mahali pako
(“Here is your home, this is your place”)
Hapa ndipo makao yako, karibu upumzike
(This is your home, welcome to the rest)

Haleluya nitaketi kwa furaha, nitapumzika kwa mungu, nitapumzika
(Halelujah I will sit with joy, I will rest with my God, I will rest)

Nitavikwa mavazi meupe, nitavikwa taji ya ushindi
(I will be clothed with white garments, I will be crowned victorious)
Taabu zote na mateso yote, hakika vitakoma
(All my troubles and tribulations, will end for sure)
Nitaungana na malaika, maserafi na makerubi
(I will join with the angels, the Seraphim and Cherubim)
Tukiimba nyimbo za ushindi, haleluya usifiwe
(While we sing songs of victory, Halelujah be praised)

Naona mbingu zimefunguka, na Yesu yu mkono wa kuume
(I see the heavens open, and Jesus sitting at the right hand)
Akinitazama kwa upole, kwa macho yenye huruma
(Looking at me with compassionate eyes) x2

Tatazama vidonda vyangu, tatazama makovu yangu
(He will take care of my wounds, He will take care of my scars)
Niloumizwa duniani, na watu wa ulimwengu
(That I was hurt in the world, by the worldly) x2

Tachukua kitambaa, atanifuta machozi
(He will take a cloth, and wipe my tears)
Akisema pole mwanangu, Yesu tanikumbatia
(Saying I’m sorry my child, Jesus will embrace me)

Bado kitambo kidogo, nitapumzika
(Just for a little while, then I will rest)

Yesu atanipeleka, kwenye kijito cha uhai
(Jesus will take me, to the wellspring of life)
Huko taniosha mwili wangu, nitapewa mwili mpya
(There he will wash my body, and be given a renewed one)
Nami nitaimba hosana, hosana ndiye mbarikiwa
(And I will sing Hosannah, Hosannah is the blessed one)
Nitaruka kama ndama, milele hata milele
(I will jump like a calf , forevermore) x2

Tavumilia, kwa ajili yako Baba
(I will persevere for your sake father)

Yatosha walivyokuonea, Yatosha walivyokudhulumu
(Enough of the oppression, enough of the persecution)
Yatosha walivyokupiga, karibu upumzike
(Enough of the beating, welcome and rest) x2

Yatosha walivyokuudhi, Yatosha walivyokutukana
(Enough of the hurt, enough of the insults)
Yatosha walivyokuzomea, karibu upumzike
(Enough of the rebukes, welcome and rest) x2

Haleluya, mateso yangu yakiisha nitauona uso wa Mungu
(Hallelujah, when my persecutions end, I will see the face of God)
Nitamwona Yesu niliyepigwa kwa ajili yake
(I will see the Jesus I was beaten because)

Yatosha walivyokuonea, Yatosha walivyokudhulumu
(Enough of the oppression, enough of the persecution)
Yatosha walivyokupiga, karibu upumzike
(Enough of the beating, welcome and rest) x2

Yatosha walivyokuudhi, Yatosha walivyokutukana
(Enough of the hurt, enough of the insults)
Yatosha walivyokuzomea, karibu upumzike
(Enough of the rebukes, welcome and rest) x2

Yesu atanipeleka, kwenye kijito cha uhai
(Jesus will take me to the wellspring of life)
Huko taniosha mwili wangu, nitapewa mwili mpya
(There he will wash my body, I will be given a new one)

Baada ya taabu, ni furaha
(After troubles is joy)

Zinzilela Lyrics by Annastazia Mukabwa ft. Rose Muhando with English Translation

Leave a comment

Nzilenzilela makata na muye, nzilenzilela nzilenzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Ee Bwana nakuinua, nikikumbuka ulikonitoa
(Oh Lord I lift you up, when I remember where you saved me from)
Kwenye maisha ya aibu, na kunifanya wa thamani
(From the life of shame, and made me valuable)
Ee Bwana nakuinua,nikikumbuka ulikonitoa
(Oh Lord I lift you up, when I remember where you saved me from)
Kwenye maisha ya aibu, na kunifanya wa thamani
(From the life of shame, and made me valuable)
Kama si wewe ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani
(Where would I be if not for you, What would I be called?)
Ningelikuwa nimekufa mimi, kwenye shimo la uharibifu
(I would have been lost, in the hole of corruption)
Kama si wewe ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani
(Where would I be if not for you, What would I be called?)
Ningelikuwa nimekufa mimi, kwenye shimo la uharibifu
(I would have been lost, in the hole of corruption)

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Ni wengi niliyowajua, wenye mapesa na utajiri
(I knew a lot of people with money and riches)
Wenye majumba ya kifahari, lakini leo hawako tena
(With elaborate mansions, but they are not there today)
Ni wengi niliyowajua, wenye mapesa na utajiri
(I knew a lot of people with money and riches)
Wenye majumba ya kifahari, lakini leo hawako tena
(With elaborate mansions, but they are not there today)
Lakini mimi wanilinda bure, si kwamba nimetenda mema baba
(But you freely secure me, not because I have done good works father)
Bali ni kwa neema yako, ndio maana mimi naishi
(But I live because of your grace)
Sio ni kwamba nimetenda mema baba, ila ni kwa neema yako
(Not because I have done good works father, but because of your grace)
Ndio maana mimi naishi, Wacha nikutuze wewe
(That is why I am alive, so let me praise you)

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Siwezi kukulipa baba, kwa yale umenitendea
(I cannot repay you father, for all you have done for me)
Bali naomba moyoni mwangu, nipe moyo wa kukupenda
(But I pray in my heart, that you would give me a loving heart)

Niondolee kiburi baba, nipe moyo mnyenyekevu
(Remove pride from me father, give me a humble heart)
Ili nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu
(So that I live for you, all the days of my life)
(Remove pride from me father, give me a humble heart)
Ili nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu
(So that I live for you, all the days of my life)

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela
Zinzilela makata na muye, zinzilela zinzilela

Older Entries

%d bloggers like this: