Wakati Wangu (My Time) Lyrics by Edith Wairimu ft Young Qualifiers

Leave a comment


(Sung in Kiswahili)

Refrain:
Wakati wa kubarikiwa ni sasa (The time of blessings has come)
Wakati wa kuinuliwa ni sasa (The time of lifting up is now)
Wakati wa kujenga tena, ni sasa (The time of rebuilding has come)
Wakati Mungu amesema ni sasa (The time that God has proclaimed is now)

Kuna wale wazee, Ezekieli anavyosema (There are those elders, as Ezekiel says)
Wanaokaa malangoni mwa nyumba ya Bwana (That sit at the gates to the House of the Lord)
Watungao maovu, na mashauri mabaya (They concoct evil and bad advice)
Wakisema siku ya kujenga nyumba si sasa (Saying that the time to build the house is not now)

Repeat: Wakati wangu ni sasa (My time is now)
Nakataa! Roho ya kizuizi (I refuse the spirit of barriers!)
Nakataa! Mashauri mabaya (I refuse the bad advise)
Nakataa! Unabii wa uongo (I refuse the prophesies of lies)
Nakataa! Roho ya ulaghai (I refuse the spirit of fraud)

(Refrain)

Watu wanapolia, uchumi ni mbaya (When people cry out because of bad economy)
Pesa nazo hakuna, mimi nitafanikiwa (Even when there is no money, I shall succeed)
Maana mwenye haki, huishi kwa amani (For the righteous live by faith)
Wakisema siku ya kuinuliwa si sasa (When others say the time to be lifted has not yet come)

Repeat: Wakati wangu ni sasa (My time is now)
Nakataa! Kupoteza imani (I refuse to lose my faith)
Nakataa! Mifumo ya kushindwa, mimi (I refuse the systems of defeat)
Nakataa! Roho ya umasikini (I refuse the spirit of poverty)
Nakataa! Mimi kuwekwa chini (I refused to be put down)

(Refrain)

Repeat: Wakati wangu ni sasa (My time is now)
Nakataa! Roho ya kuchelewa, eh hapana (I refuse the spirit of delay)
Nakataa! Laana ya kizazi (I refuse the generational curses)
Nakataa! kujithamini chini (I refuse to put myself down)
Nakataa! Kujiona mnyonge (I refuse to see myself as weak)
Nakataa! Kushindwa na magonjwa (I refuse to be defeated by sickness)
Navunja! Laana za aina (I break all the curses)
Nakataa! Kifo cha mapema, la hasha, hapana (I refuse early death, no! Never!)
Nakataa! Roho ya kukataliwa (I refuse the spirit of rejection)

Wakati wa kubarikiwa ni sasa (The time of blessings is now)

Nitasimama! (I will Stand!) Lyrics by Edith Wairimu

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Adui aliomba, anisiagasiage (The enemy prayed to crush me)
Anisiagasiage, kama ngano (To grind me like wheat)
Lakini Yesu aliomba, mimi nisimame (But Jesus asked me to stand)
Mimi nisimame kwa wema weke (Me to stand on His Goodness)
Adui aliitisha, anisiagasiage (The enemy asked to grind me)
Tena anipepete, kama ngano (And then winnow me like wheat)
Lakini Yesu akasimama, akaomba (But Jesus stood, and pleaded on my behalf)
Mimi nisimame kwa wema wake (That I may stand on his Goodness)
Ndio leo nimesimamama (That is is why today I stand)

Refrain:
Nimesimama! Kwa rehema na neema yake (I am still standing! By His Mercy and Grace)
Ile gharama, ya uhai wangu/dhambi zangu (That ransom on my life/ on my sins)
Yesu amelipa yote (Jesus has paid it all)
Mimi sitokufa, sitozimia (I will not die, I will not faint)
Nitasimama kwa wema wake (I will stand upon His Goodness)
Mimi sitokufa, sitozimia (I will not die, I will not faint)
Nitasimama kwa wema wake (I will stand upon His Goodness)

Nilipokaribia, kitini cha enzi (When I came close to the throne)
Shetani alisema “ni mchafu” (Satan said “But she is dirty”)
Yesu akasimama, akasema “ona (Jesus stood, and said “Behold)
Nimelipa gharama yake” (I have paid her ransom”)
Nilipokaribia, kitini cha enzi (When I came close to the throne)
Shetani alisema “huyu hafai” (Satan accused “this one is not worthy”)
Yesu akasimama, akasema “Baba ona (Jesus stood, and said “Father see)
Nimelipa gharama yake” (I have already paid her ransom”)

(Refrain)

Adui alinizika, akasema nimeisha (The enemy buried me, saying I was done for)
Sitoonekana tena kamwe (And will never be seen again)
Yesu alipofika, akaniita (When Jesus arrived, He called me)
Akanipa uhai wake (He gave me His Life)
Adui alinizika, akatangaza nimekufa (The enemy buried me, and announced my death)
Sitoonekana tena kamwe (I will never be seen again)
Yesu alipofika,akasema “toka!” (When Jesus arrived, he said “Be gone!”)
Akanipa uhai wake (And gave me His life)

(Refrain)

Mimi sitokufa, sitozimia (I will not die, I will not faint)
Nitasimama kwa wema wake (I will stand upon His Goodness)
Mimi sitokufa, sitozimia (I will not die, I will not faint)
Nitasimama kwa wema wake (I will stand upon His Goodness) (Repeat)