Kama Mbaya, Mbaya (If It’s Bad, So Be It) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Kama mbaya mbaya (If It’s Bad, So Be It)
Wacha iwe mbaya (Let it be bad)
Tuliwatendea mema/wema (We did them good)
Wakatulipa mabaya (But they repaid us with evil) (Repeat)

Kama mbaya mbaya (If It’s Bad, So Be It)
Wacha iwe mbaya (Let it be bad)
Tuliwaona wabora (We saw them as better)
Kumbe hawafai(But they are not suitable) (Repeat)

Walitunywesha kikombe cha uchungu (They let us drink from the cup of bitterness)
Na maumivu makali (And great pain)
Wakachukua/wakatwaa nafsi zetu (They took our bodies)
Wakazigonga misumari (And crucified them) (Repeat)

Sasa wameyakanyaga (Now they have been trod on)
Wacha Mungu ashughulike nao (Let God take care of them)
Wamevavanya (They have been tested)
Wacha mbingu zishughulike nao (Let the heavens deal with them) (Repeat)

Kama mbaya mbaya (If It’s Bad, So Be It)
Wacha iwe mbaya (Let it be bad)
Tulitenda mema (We did good)
Wakatulipa mabaya (But they repaid us with evil) (Repeat)

Sasa wameyakanyaga (Now they have been trod on)
Wacha Mungu ahangaike nao (Let God take care of them)
Wamevavanya (They have been tested)
Wacha mbingu zishughulike! (Let the heavens take care of it) (Repeat)

Mene mene… tekeli perez (Mene, mene, tekel, parsin)
Kiganja kimeandika, fukuza upesi (The finger has written, chase it away)
Mkono umeandika, fukuza upesi (The hand has written, chase it away)
Kwenye mawe kimeandika, fukuza upesi (It has written on stone, chase it away)
Ukutani kimeandika, watoke upesi (It has written on the wall, for them to get out quickly)
Ofisini kimeandika, rarua upesi (It has written in the office, to be quickly torn)
Kwa wafalme kimeandika, komesha kabisa (To the kings it has written, to stop them completely)
Kwa wakuu kimeandika, rarua upesi (To the rulers it has written, to be quickly torn)
Kwa wenye nguvu kimeandika, komesha kabisa (To the powerful, it was written, to be stopped completely)

Mene tekeli perezi, fukuza upesi (Mene, tekel, parsin, quickly chase them)
Porini waweka mafisi, wakale manyasi (They have placed hyenas in the forest to eat the grass)
Mene tekeli perezi, fukuza upesi (Mene, tekel, parsin, quickly chase them)
Porini waweka mafisi, wakale manyasi (They have placed hyenas in the forest to eat the grass)

Wapigwe! Wapigwe! Waweka mafisi (Let them be destroyed! The hyena keepers)
Wapigwe! Wapigwe! Wakose nafasi (Let them be destroyed! Let them lose their places) (Repeat)

Kanyaga kanyaga kanyaga kanyaga, kanyaga! (Step on them!)x?

Mzee Wa Kazi (God of Great Works) Lyrics by Voices United Choir

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Mzee wa kazi, wewe ndiwe shujaa (God of Great Works, You are the Champion)
Ni ule mama, nd’o akan’ambia (It is that woman, that told me this)
Shida zote, ‘nazo nilemea (All the troubles that overwhelm me)
Eti ni wewe waweza tatua (That it is You that can solve them)
Mzee wa kazi (God of Great Works)

Mzee kazi, eti we ni mwamba (God of Great Works, You are the Rock)
Ni ule dada, nd’o alinieleza (It is that girl that told me)
Adui wote, wa’nishambulia (All the enemies that attack me)
Wewe ndiwe ‘wezaniokoa (It is You that can save me)
Mzee wa kazi (God of Great Works)

Mzee wa kazi, eti we ni simba (God of Great Works, You are the Lion)
Ni ule babu, nd’o aliyesema (It is that man, that said this)
Nisiogope, nisite shaka (That I should not be afraid, nor doubt)
Simba wa Yuda, we utanilinda (The Lion of Judah, will defend me)
Mzee wa kazi (God of Great Works)

Mzee wa kazi, eti we ni Mfalme (God of Great Works, You are the King)
Ni moyo wangu, aliniambia (It is my heart that told me this)
Mbingu na ardhi zakuinaima (Heaven and earth bow before You)
Kwa ibada, kwani we ni Yahweh (In worship, for You are Yahweh)

Wewe ndiwe, mwenye baraka (You are the One with the blessings)
Wewe ndiwe, mwenye utukufu (You are the One who is Holy)
Wewe ndiwe, mwenye nguvu zote (You are the One with all power)
Wewe ndiwe, Mfalme wa wafalme (You are the King of kings)

Wewe ndiwe, Alfa na omega (You are the Alpha and Omega)
Wewe ndiwe, Muumba wangu (You are my Creator)
Wewe ndiwe, Yesu Mwokozi (You are Jesus the Savior)
Wewe ndiwe, Mwanzo na Mwisho (You are the Beginning and the End)
Mzee wa kazi (God of Great Works)

Mzee wa kazi (God of Great Works)

Mzee wa kazi (God of Great Works)

Uko Sawa (You Remain the Same) Lyrics by Alarm Ministries ft Christina Shusho

3 Comments


(Sung in Swahili)

Refrain:
Uko sawa Mungu wangu (You remain the same my God)
Mchana usiku, wewe uko sawa tu (Morning and evening, You remain the same)
Safarini hukuniacha (You did not abandon me in the journey)
Majaribuni, umenishika mkono (You held my hand) (Repeat)

Mi najua mawazo unayoniwazia (I know the thoughts You have about me)
Ni mawazo ni ya amani, wala si ya mabaya (They are good thoughts, not evil)
Kando ya maji ya utulivu huniongoza (You lead me beside still waters)
Sitaogopa mabaya, wewe u pamoja nami (I shall not fear evil, for You are with me) (Repeat)

(Refrain)

Umeniandalia, meza mbele ya watesi wangu (You have prepared a table before my enemies)
Umenipaka mafuta, kichwani pangu (You have anointed my head with oil)
Umenirehemu (You have mercy on me) (Repeat)

Wema nazo fadhili, zitanifuata mimi (Your Goodness and Mercy, shall follow me)
Nami sitanyamaza (And I shall not be silent)
Nitalisifu jina lako milele (I will praise Your name forever) (Repeat)

(Refrain)

Uko mwema Mungu wangu (You are Good, my God)
Mchana usiku, wewe uko mwema tu (Morning and evening, You are God)
Safarini hukuniacha (You did not abandon me in my journey)
Majaribuni, umenishika mkono (You held my hand) (Repeat)

Mtuliza Bahari (Calmer of Storms) Lyrics by Msanii Music Group

1 Comment


(Sung in Swahili)

Ee Baba tumekuja kwako (Father we have come before you)
Twaomba uturehemu (We ask that You have mercy on us)
Watoto wako, tu miguuni pako (Your children, we are at Your feet)
Tunalia kwa ajili ya mateso (We weep because of our affliction)
Tunayaona, tunapitia dunia hii (That we see, and encounter on earth)
Majirani wametugeuka sisi (Our neighbors have turned against us)
Hata mandugu wamekuwa maadui (Even our brothers have become enemies)
Wanatutesa kila usiku, kila kuchao (They persecute us daily)

Kimbilio letu ni wewe (Our refuge is You)
Kimbilio pekee, ni wewe (The only Refuge, is You)

Refrain:
(Bwana) Mwenye uwezo sisi twakutambua ([Lord] who is able we acknowledge You)
Tukilemewa tunajificha kwako (When we are overcome, we seek refuge in You)
Wewe ni mwamba, na si tu chini yako (You are the Rock, and we are beneath You)
Ukitamka jambo linatendeka (When You speak a word, it is done)
Hata mapepo yote hutawanyika (Even all the demons flee)
Nyosha mkono, Mtuliza Bahari (Stretch Your hand, Calmer of Storms)

Kuna wengi wapepoteza wapendwa wao (There are many who have lost their loved ones)
Kwa sababu ya chuki (Because of hatred)
Wapo wengi wamepoteza mali yao (There are many that have lost their wealth)
Kwa sababu ya wivu (Because of jealousy)
Kuna wengi wamepoteza mifugo (There are many who have lost their livestock)
Wamepoteza mimea yao shambani (They have lost their crops)
Na biashara yao ikaangushwa (And their businesses failed)

Kimbilio letu ni wewe (Our refuge is You)
Kimbilio pekee, ni wewe (The only Refuge, is You)

Siku ya kiyama inarejea (The Judgement Day is near)
Maswali mengi yataulizwa pale (Many questions will be asked there)
“Nilikupa jirani umtunze, mbona ukamtenda?” (“I tasked You to watch over your neighbor, why did you turn against them?”)
Miti na mawe ndio mashahidi (The trees and rocks will stand witness)
Paa la nyumba yaku litakukana (The roof of your house will denounce you)
Likishuhudia, uliyoyatenda (While witness your actions)

(Refrain)

Niseme Nini / Baba NinaKushukuru (What Can I say / Father I Thank You) Lyrics by Dr Ipyana

2 Comments


(Sung in Swahili)

Uliyoyatenda kwangu ni mengi (You have done a lot for me)
Shuhuda zako hazielezeki (Your testimonies cannot be explained)
Umefanya hili, umefanya lile (You have done this, You have done that)
Umenipa jina, Baba ninakushukuru (You have given me a name; Father, I thank You) (Repeat)

Refrain:
Niseme nini? Siwezi kueleza (What can I say? I cannot explain)
Baba ninakushukuru (Father, I give thanks)
Umefanya mengi, siwezi kueleza (You have done so much that I cannot explain)
Baba ninakushukuru (Father, I give thanks)
Nikulipe nini, kwa yote umetenda? (What can I give You, for all You’ve done for me?)
Baba ninakushukuru (Father, I give thanks)
Nikulipe nini, kwa yote umetenda? (What can do to repay You, for all You’ve done for me?)
Baba ninakushukuru (Father, I give thanks)

Baraka zako hazihesabiki (Your blessings cannot be counted)
Wema wako hauzoeleki (Your Goodness cannot be explained)
Umefanya hili, umefanya lile (You have done this, You have done that)
Umenipa jina, Baba ninakushukuru (You have given me a name; Father, I thank You) (Repeat)

(Refrain)

Bali ninakushukuru (But I give thanks) x?

Baba ninakushukuru (Father, I give thanks) x?

Umefanya hili, umefanya lile (You have done this, You have done that)
Umenipa jina, Baba ninakushukuru (You have given me a name; Father, I thank You) (Repeat)

Umefanya hili, umefanya lile (You have done this, You have done that)
Utafanya na lile, Bado ninakuamini (You will do that, Still I trust You) (Repeat)

Older Entries

%d bloggers like this: