Advertisements

Mifupa Mikavu (Dry Bones) Lyrics by Christina Shusho ft. Saint Stevoh

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ezekieli akiwa katika Roho (Ezekiel when in a vision)
Bwana akamweka chini (God placed him down)
Katika bonde nalo limejaa mifupa (In a valley full of bones)
Kamwambia Ezekieli “Je mifupa yaweza kuishi?”
(He asked Ezekiel “Is it possible for the bones to live?”)
Naye akajibu, “ee Bwana waijua wewe”
(And he replied, “Oh Lord You know”)
Bwana akamwambia “tabiri juu ya mifupa hii”
(The Lord told him “Prophesy over these bones”)
“Enyi mifupa, lisike neno la Bwana”
(You bones, listen to the word of the Lord)

Refrain:
Mifupa mikavu nakutabiria (Dry bones I prophesy to you)
Kwa jina le Yesu, uwe hai tena
(In the name of Jesus, to become flesh)
(Repeat)

Tabiri kwa upepo na mwili
(Prophesy in the spirit and in the flesh)
Roho wa Mungu aiweke dhahiri
(The Spirit of the Lord to make clear)
Kwa wanadamu waliona jikavu
(For as humans who only saw dry bones)
Kwa Mungu aliona jeshi moja shupavu
(God saw a mighty army)
Kuna wengi wetu tunapambana
(There are many of us who struggle)
Ng’ang’a na maisha yetu ngumu zaidi ya janga
(We wrestle with our tough lives)
But hiyo ni tu ni [.?.] rudisha
(But all that is […], it will be restored)
Position yetu in Christ, more than victorius
(Our position in Christ…)
Help thee, wealth thee and righteous
Maandiko imesema si waridhi wa mfalme
(The scripture says, we are inheriters of the kingdom)
Hautakufa, utaishi na kusimulia wema wa Bwana
(You will not die, but live and tell of the Lord’s Goodness)

(Refrain)

Natabiri juu ya afya yako (I prophesy over your health)
Natabiri juu ya kazi yako (I prophesy over your work)
Vilivyo kufa viwe hai, viwe hai tena
(Whatever was dead to live, to be live again)
Natabiri juu ya ndoa yako (I prophesy over your marriage)
Natabiri juu ya watoto wako (I prophesy over your children)
Vilivyo kufa viwe hai, viwe hai tena
(Whatever was dead to live, to be live again)
Hautakufa, utaishi na kusimulia mema wa Bwana
(You will not die, but live and tell of the Lord’s Goodness)
Vilivyo kufa viwe hai, viwe hai tena
(Whatever was dead to live, to be live again)

(Refrain)

Advertisements

Amenifanyia Amani (He has Granted Me Peace) Lyrics by Paul Clement

Leave a comment


 

(Sung in Swahili)

Refrain:
Amenifanyia amani x2 (He has granted me peace)
Kaondoa huzuni yangu (He removed my sadness)
Kanifanyia amani (And granted me peace)

Nijapopita, kwenye bonde la mauti (Though I walk through the valley of death)
Sitaogopa, maana wewe uko nami (I shall not fear, for You are with me)
Gongo lako na fimbo yako (Your rod and Your staff)
Eh Bwana vyanifariji (Oh Father they comfort me)
Wanifanyia amani (You grant me peace)
Umesema ya kwamba hutaniacha (You said that You would never leave me)
Sababu mimi ni mboni ya jicho lako (For I am the [apple] of your eye)
Bwana wanitazama, asubuhi, mchana, jioni
(Lord You look over me, Morning, afternoon, evening)
Eeh Bwana – kweli Mungu wa baraka
(Oh Lord – You are the God of blessings)

(Refrain)

Amebadilisha uchungu wangu (He turned my pain)
Umekua ni furaha yangu (It has become my joy)
Huyu Yesu amenipa furaha – Kanifanyia amani
(This Jesus gave me joy – granted me peace)
Amebadilisha machozi yangu (He turned my tears)
Yamekuwa ni furaha yangu (To become my joy)
Huyu Yesu amenipa furaha – kanifanyia amani
(This Jesus gave me joy – granted me peace)

(Refrain)

Furaha unipayo siyo kama ya dunia hii
(The joy You give me, is not of this world)
Amani unipayo siyo kama ya ulimwengu huu
(The peace You give me, is not like of this world)
We waniganga moyo nipatapo uchungu
(You encourage me in times of troubles)
Wanifanyia amani (You grant me peace)

Amenifanyia furahax2 (He has granted me joy)
Kaondoa huzuni yangu (He removed my sadness)
Kanifanyia furaha (And granted me joy)

Jina La Yesu (The Name of Jesus) Lyrics by Paul Clement

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Jina lipitalo majina yote (The Name above all other names)
Duniani na mbinguni (On Earth and in heaven)
Tena lenye mamlaka yote (With all the authority)
Humu ulimwenguni (Here on Earth)
Limeinuliwa juu (Jina La Yesu x2) ( ) x2

Refrain:
Jina lako Yesu (Your Name, Jesus) ( )x2
Lina uweza, aaa (Has Might/Power) ( )x2

Kila goti litapigwa (Every knee will bow)
(Kwa jina la Yesu) (In the Name of Jesus)
Na kila ulimi utakiri (And every tongue will confess)
(Kwamba wewe ni Bwana) (That You are the Lord)
Yesu x?(Jesus)

Ninakwita usiyeshindwa (I call You ‘The Undefeated’)
Kifo na kaburi ulivishinda (You defeated death and the grave)
Nguvu zako ziko juu ya dunia yote (Your power is over all the earth)
Umekirimiwa jina lenye uweza wote(You’ve been branded with a name with all the might)
Nguvu ni zako, ufalme ni wako (All power is yours, the kingdom is Yours)
mamlaka ni yako, hata milele (All authority belong to You, forever)
Katika wewe tunapata ushindi, ushindi (In You, we are victorious)

(Refrain)

Limeinuliwa juu (Jina la Yesu x2)(It has been lifted high – the Name of Jesus)
Juu ya mamlaka yoote (Over all other authorities)
Juu ya nguvu zote (Over all other powers)

(Verse 1)

Nikumbushe Wema Wako (Remind Me of Your Goodness) Lyrics by Angel Benard

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ni rahisi kinywa kujawa na lawama tele
(It is easy for the mouth to be filled with blame)
Pale mambo yanapoonekana hayaendi
(Whenever things do not go to plan)
Ni ajabu sana kama moyo unahangaika (kutafuta majibu)
(It is amazing how the hearts frets searching for answers)
Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka
(Amazing how the heart shows doubt)
Ya kwamba japo Mungu anaishi ndani yangu (kuna muda nahofu)
(Even though God lives in me, I am still afraid)
Japo kuwa Mungu anaketi kati yetu, kuna muda na hofu
(Though God sits amongst us, there is time that I doubt)
Nakumbuka wana waIsraeli katika bahari ya shamu
(I remember the Israelits at the Red Sea)
Japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi
(Though they passed in the middle in victory)
Kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwana
(With many songs they sung in praise of the Lord)
Lakini baada kuvuka na kuliiona jangwa (yalibadilika mambo)
(But after crossing and seeing the wilderness, things changed)
Manunguniko yalisimama (Murmurms started)
Na kusahau miujiza alotenda Bwana mwanzo
(And forgetfulness on the miracles the Lord did at the beginning)
Ee Mungu nisaidie (Oh God help me)

Refrain:
Nikumbushe wema wako nisije laumu
(Remind me of Your goodness so I that do not blame)
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
(Remind me of Your greatness in challenging times)
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
(Remind me of you testimonies that I might praise You)
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
(To sing a song of praise in the midst of tears)
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
(To sing a song of praise in the midst of tears)
(Repeat)

Nisaidie kukumbuka Baba ya kwamba umenichora kiganjani mwako
(Lord help me to remember that you have drawn me on your palm)
Kati ya wengi waliopo duniani eh, na mimi umeniona
(In the midst of many on earth, You have seen me)
Nikumbushe Baba, ya kwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa
(Remind me Father, that You healed me when I was ill)
Ya kwamba ni wewe, mlipaji wa ada yangu shuleni
(That it is You, the payer of my school fees)
Ya kwamba kama ungeniacha hatua moja nisingelifika nilipo
(That had you left me even in one step, I would not have been here)
Ee Baba, Umekung’uta mavumbi, kung’uta mavumbi mimi na kuniheshimisha
(Oh Father, you have wiped my dust and honored me)

(Refrain)

Bwana Yesu nakutazama, ninakuabudu
(Lord Jesus I look to You, I worship You)
Mungu wa maisha yangu, nisaidie nisalalamike mbele zako
(God of my Life, help me not to complain before You)
Katika hali zote nijue upo
(In any situation to know that You are there)
Umesema hutaniacha, ee Yahweh
(You have said You would not leave me, Oh Yahweh)
Haya ni maombi yangu (This is my prayer)

Sitabaki Nilivyo (I Shall Not Remain The Same) Lyrics by Joel Lwaga

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Maisha haya, ninapita tu
(I am only passing through this life)
Hali hii ya sasa ni kwa muda tu
(My present condition is only for a time)
Ushindi wangu, U karibu nami (My victory is close)
Mtetezi wangu, yu hai (Because my Defendeer lives)

Refrain:
Sitabaki kama nilivyo
(I shall not remain the same) x4

Silalamiki, wala sikufuru
(I do not complain, nor do I blaspheme)
Najua ni darasa napitishwa
(I know it is a trial I am put through)
Imani yangu ipo kwenye kipimo
(My Faith is is being measured on a scale)
Najua nitapita tu (I know I shall prevail)
Sitamani za wengine wala sijilinganishi
(I do not desire others’, neither do I compare myself)
Najua wakati wangu upo (I know my time is coming)
Siogopeswhi na mapito ninayoyapitia
(I am not afraid of my trials)
Namwamini yule aliyeruhusu nipite
(For I trust He who allowed I pass through this)

(Refrain)

Mtetezi wangu (My Defender lives)
Yu hai (Yu hai) (Lives (is alive)) x3 (Repeat)
Sitabaki kama nilivyo (I shall remain as I am) (Repeat)

(Refrain)

Siteketei (I do not Burn) Lyrics by Angel Benard

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Refrain:
Mi siteketei, siangamii (I do not burn, I do not fall)
Sigharikishwi, upo nami (I am not swept away,  for You are with me)
(Repeat)

Hupimwi kwa siku, Hupimwi kwa miaka (You are not measured by days or years)
Unatafsiri majira, Huzuiwi na muda (You define seasons, You are not bound by time )
Umejawa na nguvu, Ndio maana nakuita Baba (You are filled with power, I call You Father)
Moyoni mwangu, najawa sifa (My heart is filled with praise)
Na ujasiri katika wewe (For my courage is in You)
Hakuna mlima wa kuniangusha (No mountain can cause me to fail)
Ndani yako ninasimama (For I stand in You)

(Refrain)

Nimezungukwa na we kila pande (I have been surrounded on all sides)
Hakuna jambo la kuniangamiza (There is nothing that will cause me to fail)
Majeshi, yalo upande wangu (Your armies, that are on my side)
Ni mengi sana kulika hawa wa dunia (Are more than those in the world)
Hatua zangu zaongozwa nawe (My steps are ordered by You)
Siangamii, siteketei (I do not fall, I do not burn)
Katika wewe, ninasimama (For I stand in You)
Siteketei, na ninadumu (I do not burn, I stand firm)

(Refrain)

Kwako Bwana nasimama (I stand in You, Lord)
Ndiwe mwamba ni salama (You are the Solid Rock)
Kwako Bwana nasimama (I stand in You, Lord)
For they that believe in You
We shall stand firm, forever
Forever

(Refrain)

Ipo Siku (There Is a Day) Lyrics by Goodluck Gozbert

1 Comment


(Sung in Swahili)

Ni mbali nimetoka (I’ve come from far)
Tena ni ajabu kuwa hai (And it’s amazing that I’m still alive)
Maana ningeshakufaga (For I should have died)
Ni mengi nimeona (I have seen many things)
Tena ya kuvunja moyo (Many of them heartbreaking)
Labda ningeshamwacha Mungu (That I should have left God)

Bridge:
Kama ni misongo ya mawazo (If it is pressuring thoughts)
Magonjwa mama, nimepitia, ninazoea (Or illnesses, I’ve been through, I’m used to them)
Maumivu ya kudharauliwa, umasikini (Hurt from contempt, poverty)
Ni kila siku, ninajipa moyo: (Everyday, I encourage myself:)

Refrain:
Ipo siku yangu tu, Ipo Siku (There is my day, a day)
Ipo siku yangu tu (My day)
Nami (Niba niba nibarikiwe) (That I will be blessed as well)
Nami nibarikiwe (nibarikiwe) (That I will be blessed as well)
Nibarikiwe (nibarikiwe) (I be blessed)
Nami nibarikiwe ( nibarikiwe) (I be blessed as well)
Niba, niba, nibarikiwe (I be blessed)

Ingawa kwa sasa wananisema vibaya (Though they currently speak ill of me)
Nami sishangai – najua ni ya wanadamu hayo (I am not dismayed – these are earthly things)
Ingawa sipati na ni kwa muda mrefu (Though lack for a long time)
Siachi kuomba; Mungu si kiziwi (I do not stop praying; God is not deaf)
Binadamu wema, ukiwa nacho (Men are good when you have things)
Kwa sasa waniepuka sina rafiki wa dhati (But now they avoid me, I do not have friends)

(Bridge + Refrain)

Miaka imepita, unaombaga mtoto hupati (Years are past, you’ve prayed in vain for a child)
Vuta subira maana Yeye hachelewi (Be patient, for He’s never late)
Ona biashara imeandamwa mikosi hupati (Your business is followed by misfortunes)
Usimwache Mungu, waganga watakuponza (Do not abandon God, witchcraft will destroy you)
Mpo kwa ndoa ila nyumbani amani hakuna (There is no peace in your marriage)
Msimwache Mungu – michepuko sio jibu (Do not abandon God – separation is not the answer)
Umeugua tumaini la kupona hakuna (You are terminally ill – no hope of survival)
Usimtazame mwanadamu siku yako imekaribia (Do not hope on men, your day is coming)

Najua Ayaya (Ipoa) x? (I know, itwill be well)

Misuko-suko ya ndoa (The travails of marriage)
Mtoto anakusumbua (Your child grieves you)
Giza likiingia unawaza wapi utalala (When darkness comes, you don’t know where to sleep)
Masimango Mashemeji, ati huzai mtoto (Your in-laws mock your barrenness)
Masimango mama wa kambo (Your step-mother mocks you)
Umemchosha nyumbani (She is tired of you)
Usiwaze usiumie, najua yote yatapita (Do not be discouraged, all shall pass)
Siku imekaribia, najua yote yatapita (Your day is near, I know all shall pass)

Nawe ubarikiwe (nibarikiwe) (That you should be blessed)
Ubarikiwe (nibarikiwe) (Be blessed)
Nawe ubarikiwe (nibarikiwe) (That you should be blessed)
Uba, Uba, Ubarikiweee (Be blessed)

Older Entries

%d bloggers like this: