Gharama (The Cost) Lyrics by Guardian Angel ft Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

li li la la la la…

Kile unapanda utavuna wewe (What you sow, you shall also reap)
Ukipanda mazuri, utavuna wewe (If you sow goodness, that is what you’ll reap)
Kile unapanda utavuna wewe (What you sow, you shall also reap)
Ukipanda maovu, utavuna wewe (If you sow evil, that is what you shall reap)

li li la la la la…

Katika maisha yako jifunze kuwa na kumbukumbu
(In your life, teach yourself to have remembrance)
Lolote ufanyalo, lazima kuweka kumbukumbu
(In everything you do, remember it)
Mema na mabaya, lazima uandike kumbukumbu
(Goodness and evil, you must remember)
Basi, yale uliyopanda jana, ndivyo unavyoishi leo
(For what you sowed yesterday, that is your life today)
Na yale unayopanda leo, kesho utalipa gharama
(And what you sow today, you shall pay for it tomorrow)
Ikiwa mmebana mabaya, lazima utalipa gharama
(If you have forbidden evil, you must pay the price)
Gharama, gharama, gharama! (The cost, the cost, the cost!)
Gharama, gharama, gharama!

li li la la la la…

Na ipo/ninalipa gharama flani ya mambo/vitu flani nilifanya
(There is a price for some things I did)
Gharama ya choices, decisions, conflictions nilimake
(The cost of choices, decisions and conflicts that I caused/made)
Ninajutia makosa nilifanya, mami
(I regret the mistakes I made) (Repeat)

Kumbuka dunia haisemi uongo, ni lazima utalipa
(Remember the world does not lie, there is a cost for everything)
Usije beba mawe ukaumiza mgongo, ukaharibu future
(So that you would not be like Sisyphus, hurt your back and destroyed your future)
What would I go, what would I do?
Maji yakimwagika hayazoleki
(Spilled water cannot be collected)
What you should do, mwombe Mungu
(You should pray to God)
Akishasamehe, wala hakumbuki
(For when he forgives, he no longer remembers)

li li la la la la…

Advertisement

Malaika (Angels) lyrics by Msanii Group

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Kisa cha Mafarisayo chashangaza (The case of the Pharisees is amazing)
Walimshika Yesu, wakamsulubisha (They arrested Jesus, and crucified Him)
Wakamlaza kaburini, kisha wakaweka jiwe kubwa (They laid Him in a grave, and placed a large rock)
Wakajua yamekwisha (And thought that it was finished)
Ndivyo watu wengi, maadu zetu (That is similar to many people – our enemies)
Wanayaweka mawe, wakidhani wamezifunga njia (They put rocks thinking they have blocked our way)
Wanaiweka mitego, ili tuanguke (They place traps, so that we fall)
Wasilo lijua: tumezungukwa na malaika (What they do not know: we are surrounded by angels)
Wasilo lijua: tumezungukwa na malaika, wa nuru (What they do not understand: we have been surrounded by an angel of light)

Refrain:
Ni malaika aliondoa jiwe kaburini (It is an angel who removed the stone blocking the grave)
Mwana wa Mungu asiye na hatia kainuliwa (Son of God with no sin was lifted up)
Jaribu linaweza kuwa kubwa kwetu (Temptations maybe many to us)
Ila Mungu huleta mlango wa kutokea (But God opens doors for us to escape)
Jaribu linaweza kuwa kubwa kwetu (Though the temptations may be great for us)
Ila Mungu huleta mlango wa kutokea (But God brings new exits for us)

Walimuua Yesu, kisha wakaweka jiwe (They killed Jesus, and placed a rock)
Kubwa, asiweze kufufuka (A large rock, that He should not rise)
Asikari nao walikesha kule (The guards kept a night vigil)
Mwili wake usipate kuibiwa (So that His body would not be stolen)
Maadui hata wakeshe, neno la Mungu linatimia (Even if our enemies keep a vigil, the world of God will be fulfilled)
Mipango yake hukamilika, ahadi zake hazichelewi (His plans will be completed, and His promises are never late)
Ni mwaminifu Mungu wetu, ni mwaminifu (Our God is faithful, He is faithful)
Ni mwenye Nguvu Mungu wetu, yeye hashindwi (Our God is powerful, He cannot be defeated0)

(Refrain)

Nimepakwa (I Have Been Anointed) Lyrics by Kestin Mbogo

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Tazama! Nimepewa nguvu, mamlaka
(Behold! I have been given the power, authority)
Ya kukanyaga nguvu za giza
(To trample on the powers of darkness)
Tena, nimejazwa na Roho Mtakatifu
(Also, I have been filled by the Holy Spirit)
Nimo ndani yake, Yesu ndani yangu
(I am in Him, Jesus is in me)

Walio upande wangu (Those who are with me)
Ndio wengi kuliko maadui (Are more numerous than my enemies)
Siwezi shindwa, siwezi zimia (I cannot be defeated, I will not faint) (Repeat)

Nimepakwa mafuta mabichi (I have been anointed with fresh oil)
Pembe yangu umeiinua (My horn, you have exalted)
Ndio maana, nina uhakika (That is why I have assurance)
Nitashinda, mimi nimshindi (I shall win, I am an overcomer) (Repeat)

(From the Top)

Nitashinda, mimi nimshindi (I shall win, I am an overcomer) x?

Tazama! Umepewa nguvu, mamlaka
(Behold! You have been given the power, authority)
Ya kukanyaga nguvu za giza
(To trample on the powers of darkness)
Tena, umejazwa na Roho Mtakatifu
(Also, You have been filled by the Holy Spirit)
Yuko ndani yako, Yesu ndani yako
(You are am in Him, Jesus is in you)

Walio upande wako (Those who are with you)
Ndio wengi kuliko maadui (Are more numerous than your enemies)
Huwezi shindwa, huwezi zimia (You cannot be defeated, I will not faint) (Repeat)

Amenichekesha (He Has Given Me Laughter) Lyrics by Kelsy Kerubo

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Marafiki zangu ketini, nina neno kwenu
(Sit  my friends, I have a word for you)
Wapenzi wangu-marafiki zangu, ketini niwaambie
(My loves-my friends, sit and let me tell you)
Mnakumbuka siku moja niliwaambianga?
(Do you remember the day that I told you?)
Kuna Jina moja baba na mama wanapenda kuliita
(There is a name that my father and mother loved to call)
Wakati wa kulala, kuamka, saa nane za usiku wanalika
(In the times of sleep, in raising up and during the middle of the night they call it)

Na mimi siku moja nikaamua, kuungana nao kuliita
(And one day I decided, to join them in calling the Name)
Wakipiga magoti chini, na mimi napiga o
(When they kneel, I also kneel with them)
Jina hilo ni Yesu, Yesu, Yesu (That name is Jesus, Jesus, Jesus)
Toka na mimi niliite jina hilo (From the time I called that name)
Mambo yangu yamefunguka (My things have opened up)
Toka na mimi niite jina hilo (From the time I called that Name)
Ona sasa napendeza (Look at how I am beautiful)
Yamenikuta mwenzenu, Yamenikuta na mimi
(It has arrived to me, it has arrived for me)
Nimekutanana naye, Yesu mwana wa ‘Zareti (I have met Jesus of Nazareth)
Amenipa kicheko zaidi hasara (He has given me delight instead of loss)

Refrain:
Amenichekesha, amenichekesha na mimi
(He has given me laughter, He has delighted me)
Amenichekesha, Ndio maana leo naimba
(He has given me laughter, that is why I sing today)

Repeat: Refrain
Ona leo nacheka tena (Look at how I laugh again today)
Amenichekesha kwa furaha (He has made me laugh with delight)
Waliocheka kwa dharau sasa (The ones who laughed at me with derision)
Amenichekesha huyu Yesu (He has delighted me, this Jesus)
Amenichekesha na mimi (He has given me laughter)

Mwanadamu, mwanadamu, jamani, hatoshelezi
(Human, man, is truly not enought)
Kuna m’dalili (?) wambia: mwanadamu habadiliki
(I tell you that a man does not change)
Moyo kama nyama (Their heart is of flesh)

Wameweka vituo vya kuchekeshwa (They have placed fake places of laughter)
Wakikuchekesha unabaki na shida (They make you laugh but your issues remain)
Kirudi nyumbani, machozi utalia, utalia tena
(When you return home, you will weep again)
Ila ukikutana na huyu yesu, utacheka daima,
(But if you encounter Jesus, you will laugh forever)
Furaha, amani, hayatakatika maishani mwako
(Joy, peace, will not depart from your life)
Sarah kasema, “umenifanyizia kicheko”
(Sarah said, “He has given me laughter”)
Na mimi nasema, amenivalisha kicheko
(And I also say, he has adorned me with laughter)

Repeat: Refrain
Huyu Yesu we (Oh, This Jesus)
Leo nacheka jamani (Look at how I laugh today)
Machozi niliyoyalia siku nyingi amepangusa (He has wiped the tears that I have cried for many days)
Wabaya wangu wanashangaa sana (My detractors have been surprised)

Bridge:
Oh, unalia sana ndugu, mama, baba (Oh, You weep a lot my brother, mother,  father)
Kuja kwa Yesu, utacheka tena (Come to Jesus, you will laugh again)
Kitengo ya maisha chekechea (My section of life is still new)
Atakutua, na wewe utacheka (He will remove your burdens, and You will also laugh)
Ona amenichekesha (Look at how He has made me laugh)

Repeat: Refrain
Huyu Yesu we (This Jesus)
Niliyekuwa ombaomba na mimi ninaombwa (The one who was a beggar, I am now a lender)
Niliyekopa mavazi leo nakopeshana (The one who borrowed clothes, today I am a lender)
Amenichekesha kwa baraka, eh (He has delighted me with blessings)
Amenichekesha kwa amani (He has delighted me with peace)
Hajashindwa, kuja na wewe atakuchekesha (He is not unable to also make)
Marafiki zangu, Yesu amenichekesha (My friends, Jesus has given me laughter)
Ndugu zangu, ona Yesu amenichekesha (By brethren, look at how Jesus has given me laughter)

Damu (The Blood) Lyrics by Kestin Mbogo ft. Essence of Worship

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Damu iliyo mwagika, pale msalabani Kalvari x2
(The blood that was shed, at the cross in Calvary)
Hiyo damu yanitosheleza, hiyo damu yake Mwokozi x2
(That blood satisfies me, the blood of the Savior)

Nimesamehewa, nimeoshwa dhambi
(I have been forgiven, my sins have been cleansed)
Hiyo damu yake Mwokozi (Through the Savior’s Blood)
Nimekombolewa, tena nimesahabika (I have been ransomed, and counted)
Hiyo damu yake Mwokozi (Through the Savior’s blood) (Repeat)

(Refrain)

Yesu aliingia, pahali patakativu (Jesus entered, the Holy Place)
Kwa damu yake mwenyewe (By His own blood)
Na sisi tumefanyika, wakuhani na wafalme (And we have been made priests and kings)
Kwa damu yake Mwokozi (By the Savior’s blood) (Repeat)

(Refrain)

Pale pale, pale pale msalabani (Right there on the Cross)
Pale pale, ndipo nimetulia (That is where I am at peace) (Repeat)

Nimetwika, pale pale (I have unburdened myself, there)
Nimejificha, pale pale (I have hidden, there)
Chini ya msalaba, Pale pale, ndipo nimetulia (Under the Cross, that is where I am at peace) (Repeat)

Older Entries

%d bloggers like this: