Chorus:
Mungu amekusudia kukubariki
Mungu amekusudia kukubariki
Verse 1:
Je unaweza kungojea kidogo
Kwani bwana yesu amekusudia kukubariki
Mateso unayopitia siku ya leo
Hayalinganishwi na utukufu utakaopata
(chorus)
Verse 2:
Je unajua kucheleweshwa si kunyimwa
tena kungojea huzaa kuvumilia
Kuvumilia huzaa kukomaa
Heri kukomaa kuliko kuwa mtoto
(Chorus)
Verse 3:
Kumbuka Hana alimgojea Bwana
Akabarikiwa na nabii Samweli
Huyo Mungu aliyemkumbuka
Siku ya leo atakukumbuka
(Chorus)
Verse 3:
Iburahimu allimgojea Mungu
Miaka mia moja Mungu hakumsahau
Anyeshaye mvua jangwani
Atakuinua watu washangae
(Chorus)
Verse 4:
Nakuhakikishia ewe rafiki yangu
Kwamba Mungu wangu ni mwaminifu
Usihangaike mngojee Bwana
Ahadi zake hazivinjiki milele
Leave a Reply