(The Shepherd’s Psalm – Psalm 23)

Bwana mchungaji wangu, sitapungukiwa
katika malisho ya majani, mabichi hunilaza
Kwa maji matulivu, yeye huniongoza
Kwa uvuli wa mauti, sitaogopa kamwe

Chorus:
Umeniandalia, meza mbele yangu
Machoni pa watesi wangu, Bwana huniongoza
Huisha nafsi yangu, katika njia za haki
Kwa ajili ya jina lako, wewe upo nami

Nimekukimbilia, Baba Mungu wangu
Nisiaibike, mbele za watesi wangu
Wewe upo nami, gongo na fimbo yako
vyanifariji Baba, Sitaogopa kamwe

(Chorus)

Umenipaka mafuta, kichwani mwangu
Kikombe kinafurika, machoni pa watesi wangu
Wema nazo fadhili, zitanifuata
Siku zote za maisha yangu, nyumbani mwako milele