(Sung in Swahili)

Uko wapi, eh Mungu wangu? (Where are You, Oh my God?)
Uko wapi? Njoo uniokoe (Where are You, come and save me) (Repeat)

Mawimbi yanataka kuniangamiza (The waves threaten to drown me)
Misukomisuko yaniandama (Troubles follow me)
Dhoruba na majaribu havikomi kwangu (Storms and temptations do not cease)
Uko wapi? Fanya hima niokoe (Where are You, make haste and save me)
Uko wapi, eh Mungu wangu? (Where are You, Oh my God?)
Uko wapi? Njoo uniokoe (Where are You, come and deliver me)

Refrain:
Uko wapi, Ee Bwana? (Lord, Where are You?)
Uko wapi, mbona ni kama umeniacha? (Why does it feel like You’ve abandoned me?)
Usifiche uso wako, ee Bwana (Do not hide Your Face from me, Oh Lord)
Usifiche uso nipoonapo rehema (Do not hide Your Face once I see compassion)
Mwili huu ni wa nyama (This body is of flesh)
Unachoka pekee yangu sitaweza  (It tires, I cannot by myself) (Repeat)

Nimegubikwa wimbi la huzuni na mawazo (I have been overwhelmed by depression)
Amani kwangu ni kama ndoto (Faith to me, is like a dream)
Ole wangu, nikifurahi siku moja (Woe unto me, if I am happy one day)
Siku sita nitalia wiki ipite (For six days I will weep, the week to pass)
Magumu yangu nikisimulia kwa ndugu zangu (When I talk of my difficulties to my brothers)
Waniambia utajijua na Mungu wako (They tell me to take it with Your God)
Nikielezea magumu yangu kwa wapendwa (When I tell of my difficulties to my loved ones)
Wananiambia tumechoka kukufariji (They tell me they are tired of comforting me)
Wakati mwingine natamani, heri nife (Other times, I desire to die)
Kuliko kuishi, ninyanyasike hivi (Rather than to live and suffer like this)

Uko wapi ee Mungu wa Eliya (Where are You, Oh God of Elijah?)
Uko wapi ee Mungu Wa Ibrahimu (Where are You, Oh God of Abraham?)
Uko wapi ee Mungu Wa isaka (Where are You, Oh God of Isaac?)
El Shaddai, Fanya hima uniokoe (God Almighty, make haste and deliver me)

(Refrain)

Nina neno juu yako, Ee mpendwa (I have a word for You, beloved)
Usilie kwa Magumu uliyo nayo (Do not cry of your hardships)
Usitazame jaribu ulilo nalo (Do not Look at the trials you have)
Inia macho msalabani umtazame Yesu (Lift Your eyes to the cross and look to Jesus)
Japo ndugu wakikutenga na kukuacha (Though brothers isolate and leave you)
Yesu, atakukumbatia (Jesus will embrace You)
Majaribu ipo siku yatakoma (There is a day that the temptations shall end)
Utasahau shida zote ulizopata (And you shall forget all your past difficulties) (Repeat)