(Sung in Swahili)

Yeye aliyeuteka moyo wangu (The one who captured my soul)
Yeye aliyeujaa moyo wangu (The one who has filled my spirit)
Yeye aliyeifia nafsi yangu mimi (The one who died for me)
Nimekaa natafakari juu ya pendo la kweli (I have reflected on His true Love)
Ninalolipata kwake (That I received from Him)
Nimekaa najiuliza juu ya pendo la kweli (I have sat and reflected on His true Love)
Analonionyesha kwangu, Mungu (That God has shown me)

Aliyebadilisha maisha yangu (The one who changed my life)
Anayepigana na adui zangu (The one who fought against my enemies)
Aliyeweka amani moyoni mwangu (The one who places peace in my heart)
Sitamani mwingine (I desire no other) (Repeat)

Maumivu alinifutia (He wiped my grief)
Kwa maneno ya upendo (With his loving words)
Msalabani alinifia (He died on the cross for me)
Nitampenda milele (I will love Him forever) (Repeat)

Refrain:
Response: Wa roho yangu ni Mungu (Of my Soul is God)
Mpenzi wa roho yangu ni Mungu x4 (The lover of my soul is the Lord)
Wa roho yangu ni Mungu, mimi (Of my soul, mine)
(Repeat)

Thamani ya maisha yangu, anayeijua niye (Only He knows the value of my life)
Thamani ya uzima wangu, anayeijua niye (Only He knows the value of my life)
Gharama ya wokovu wangu, anayeijua niye (Only he knows the cost of my salvation)
Ukiniona nina furaha, yeye furaha yangu (When you see me joyful, He is my joy)
Ukiniona nina uzima, yeye uzima wangu (When you see me alive, He is my life)
Mpenzi wangu, mimi (My Love)

Ananipenda, nami nampenda (He loves me and I love Him)
Ananipenda, tunapendana (He loves me, we love each other)
Nani kama yeye, Mungu hakuna kama ye
(Who is like Him? God there is no one like Him)
Ana pendo la kweli, pendo lake halichuji
(He has true Love: His love does not discriminate)
Ananipenda, nami nampenda (He loves me, and I love Him)
Yupo karibu nami, majira yote (He is near to me all the time)
Tena zaidi hata ya nguo niliyovaa (Closer than even the clothes I wear)

Kwenye ndibwi la penzi lake, sijawahi kujutia
(In the lake of His Love, I have never regretted)
Nimezama kwa pendo lake, ili nisije jutia
(I have sunk into His Love, that I may never regret it)
Ananipenda sana ye, mpenzi wangu
(He loves me so, my Love)
Ninampenda sana ye, mpenzi wa roho yangu
(I love Him so, the lover of my soul)
(Repeat)

(Refrain)