(Sung in Swahili)

Hili ni ombi langu kwako, ee Mungu wangu (This is my prayer to You, my God)
Unitendee jambo jipya (Do something new unto me)
Hii ni sala yangu kwako, ee Baba yangu (This is my prayer unto you, my Father)
Unifanyie jambo jipya (Do something new unto me)
Nimesubiri kuvushwa, toka nilipo (I have waited to be promoted from where I am)
Unitendee jambo jipya (Do something new unto me)
Moyo wangu watumaini, kwamba wewe unaweza (My heart hope that You will)
Unifanyie jambo jipya (Do something new unto me)
Nimeona umetenda kwa wengi, kwenye maisha yao (I have seen you do unto others’ lives)
Nami unitendee jambo jipya (Do something new unto me)
Nimeona umeinua wengi, kwenye maisha yao (I have seen you lifting others’ lives)
Unitendee jambo jipya (Do something new unto me)

Yule mjane wa Naini, aliyefiwa na mwanawe (The widow in Nain, that lost her child)
Ulibadili historia yake (You changed her history)
Lazaro siku nne kaburini, mimi sijamwona kushtuka (Lazarus four days in the grave, we’ve never seen such wonder)
Ulishangaza mafarisayo (You amazed the Pharisees)
Mwanamke aliyetokwa na damu, miaka kumi na miwili (The woman who bled for 12 years)
Ulibadili maisha yake, unitendee (You changed her life, change mine as well)
Aliyepooza yuko kule, anasubiri muujiza wako (The paralytic is there, waiting for your miracle)
Yesu nakuomba, unitendee (Jesus I pray, do unto me)
Maisha yangu yanajaa mapooza, uko wapi nabii? (My life is full of paralysis, prophet, where are you?)
Ubadili maisha yangu (Change my life as well)

Nimechoka kufinyiliwa, nimechoka kukanyagiwa Yesu (Jesus I am tired of being oppressed and stepped on)
Unitendee jambo jipya (Do something new unto me)
Nimesubiri kupandishwa cheo, lakini imetosha (I have waited for promotion, now that is enough)
Unitendee jambo jipya (Do something new unto me)
Nimeajiriwa miaka mingi, kwenye kampuni hii (I have been hired for a long time in this company)
Lakini sijapandishwa cheo (But I have not been promoted)
Walioajiriwa mwaka jana, wengine wamepandisha vyeo (The ones hired last year, some have already been promoted)
Sasa wanaitwa maprofesa (Now they are called professors)

Ombi langu kwako, ombi langu kwako (My prayer to you, my prayer to you)
Sala yangu kwako, naomba unitendee (My prayer unto you, I pray that you do unto me)
Unitendee, inuka unitendee (Do unto me, rise and do unto me)
Yesu nakuomba, unitendee (Jesus I pray, do unto me)

Refrain:
Unitendee, unitendee (Do unto me)
Yesu, nakuomba unitendee (Jesus, I pray that You do unto me)
Unitendee, unitendee (Do unto me)
Fanya jambo jipya, unitendee (Do something new unto me) (Repeat)

Eliya naye alilala, pale chini ya mretemu (Elijah too slept under the juniper tree)
Ulimtuma kunguru kwake (You sent the raven to him)
Alipata nguvu Bwana, ya kushindana na adui zake (Lord his strength was restored to contend with his enemies)
Ulibadili maisha yake (You changed his life)
Mimi ni nani mbele zako? Ulinifia msalabani (Who am I before You? Yet You died on the cross for me)
Hebu badili hatima yangu (Change my future)
Yesu badili historia yangu, badili maombi yangu (Jesus change my history, change my prayer)
Badili maisha yangu, unitendee (Change my life and do unto me)

(Refrain)

Advertisement