(Sung in Swahili)

Refrain:
Siki na sifongo (Vinegar and sponge)
Aliteswa, imekwisha (He was persecuted, it is finished) (Repeat)
Eloi, eloi, eloi (My God, my God, My God)
Sabakhtani? imekwisha (Why have You forsaken me? It is finished) (Repeat)

Ee Mungu wangu, mbona (Oh my God, why) x2
Umeniacha? (Have You forsaken me?)
Ile kazi uliyonituma Baba (The task you set me Father)
Kazi ya kubeba msalaba (The work of carrying the cross)
Imekwisha (It is finished)
Ile kazi uliyonituma Baba (Father, the task you set for me)
Kazi ya kukomboa ndugu zangu (The work of saving my brethren)
Bwana imekwisha (Lord, it is finished)
Hebu tazama vidonda vyangu (Look at my wounds)
Tazama na maumivu yangu (Look at my pain)
Imekwisha (It is finished)

Kati ya mashtaka ya ulimwengu (In the midst of the world’s accusation)
Ila mtenga binadamu na Mungu (And the separator of man and God)
Ilichorwa kwa kalamu nyekundu (That was written in red ink)
Nimeifuta kwa damu yangu (I have erased with my blood)
Leo imekwisha (Today it is finished)
Mikononi mwako, naiweka roho yangu (In your hands, I have placed my spirit)
Sasa imekwisha (Now it is finished)
Nimeunyima nini ulimwengu? (What have I held from the world?)
Ufalme wangu si wa ulimwengu (My kingdom does not belong to the world)
Ona imekwisha (Look, it is finished)
Sasa ninawaleta ndugu zangu (Now I bring with me my brethren)
Mimi nakwenda kwa Baba yangu (I go to my Father)
Kazi imekwisha (My work is finished)

(Refrain)

Nimekwisha wakomboa ndugu zangu (I have saved my brethren)
Mimi nimeushinda ulimwengu (I have defeated the world)
Imekwisha (It is finished)
Mimi ndimi njia kweli na uzima (I am the way the truth and the life)
Nakwenda kwangu sitaki lawama (I go to my home blameless)
Kazi imeisha (My work is finished)
Wenye shida na magonjwa inukeni (Those with troubles and illness arise)
Nasema kwangu njooni (I say come to me)
Nitawapumzisha (And I shall give you rest)
Wacha pazia za hekalu zipasuke (Let the curtains of the temple tear)
Watatifu wasalimike (For the saints to be spared)
Kazi imekwisha (The work is finished)
Nakutangazaia msamaha Yuda (I declare forgiveness to you, Judah)
Kwa kifo changu nilikupenda (In my death I loved you)
Ona imekwisha (See, it is finished)

(Refrain)