(Sung in Swahili)

Nina haja na we (I need You)

Nimejua nimefanya mahesabu, nime elewa (I know, I have calculated, I have understood)
Bila wewe Bwana sijiwezi kabisa (That without Lord, I am not able)
Changamoto, panda shuka, miiba njiani
(The challenges, the ups and downs and the thorns on my way)
Bila wewe Bwana, siziwezi kabisa (Without You Lord, I am completely unable)

Ndoto zangu, ni wewe utazitimiza Bwana (Lord it is You who would fulfill my dreams)
Maono yangu, ni wewe nategemea Bwana (I depend on You Lord for my visions)
Bila wewe Bwana, nitaaibika kabisa (Without You Lord, I will be shamed)
Oh, Bila wewe, nitashindwa kabisa (Without you, I will fail)

Refrain:
Nina haja na wewe, bila wewe nimeshindwa (I need You, without You I am defeated)
Nimetambua nimejua, bila wewe sina thamani
(I know and acknowledge, that without You I have no value)
Thamani yangu ni wewe tu, msaada wangu ni wewe tu
(My value is in You, my Helper is You only)
Nishikilie, na mimi mwanao (Hold me, Your child) (Repeat)

Nina kiu na wewe Bwana wangu (I am thirsty for You ,my Lord)
Nina haja na wewe, usiku mchana (I need You, night and day)
Kwenye maji ni wewe, maji ya uzima Bwana
(In the waters, Lord You are the waters of Life)
Kwenye mti ni wewe, mti wa uzima, Yesu (You are the Tree of Life, Jesus)
Kwenye mawe ni wewe, jiwe la pembeni litegemewalo
(You are the dependable Rock of Ages)
Kwa wanyama wewe ni Simba wa Yuda (You are the Lion of Judah)

(Refrain)

Nina maswali mengi akilini sipati jibu (I have many unanswered questions)
Uoga mkubwa, moyo unapiga mwendo wa kasi (I am afraid, my heart races)
Ila niende wapi? Bila wewe siwezi (But where would I go without You?)
Ukiniacha, nitajivunia tena nani? (If you leave me, in whom would I boast?)
Wewe ndiwe kiburi yangu, wewe ndiye thamani yangu (You are my pride and worth)
Najaribu kukusanya kwa uwezo wangu wa kukidhi mahitaji
(I have tried to collect all that will satisfy my needs)
Nimetambua, vyote duniani havimalizi kiu yangu
(And have realized all wordly things will not satisfy my thirst)
Ni wewe tu Bwana, ninakuhitaji (Only you my Lord, I need You)

Repeat: Nakuhitaji (I need You)
Kwenye masomo (In my studies)
Kwenye biashara zote (In all business)
Kwenye familia na jamii (In my family and relatives)
Kwenye maono yangu (In my visions)
Siwezi bila wewe, nakuhitaji (I cannot without You, I need You)
Maishani mwangu (In my life)
Kwenye ndoto zangu (In my dreams)
Nakuhitaji Bwana (I need You Lord)
Maana wewe unaweza (For you are able)

Advertisement