(Sung in Kiswahili)
Wapo waliotembea kwa neema yako (There are those who walked in your grace)
Uliwafanya wakubalike kwa wengi (You made find favor by many)
Na walipo simama katikati ya watu (And when they stood among the people)
Uso wao ukang’aa kwa kibali (Their faces shone with favor)
Ah, waliandamwa na wivu wa wengi (Ah, they were pursued by the jealousy of many)
Lakini mipango yao haikusimama (But the jealous plans did not succeed)
Na ukanyanyua vichwa vyao juu (You lifted their heads high)
Kwa sababu mkono ulikuwa nao (For your hand was upon them)
Refrain:
Nipe Neema yako Bwana (Give me Your grace, Lord)
Nikubalike machoni pa watu (To find favor in the eyes of people)
Milango ifunguke mbele yangu (Let doors open before me)
Pasipo nguvu zangu (Without my own strength)
Nipe Neema yako Bwana (Grant me Your grace, Lord)
Fursa zinifuate kila mahali (Let opportunities follow me everywhere)
Wakiinuka kunizuia (When they rise to block me)
Nisimame kwa ushindi (Let me stand in victory)
Wapo walioketi chini kwa muda (There are those who waited for long)
Baadaye wakati wao ukafika (But their time came)
Uliwatoa mahali pa chini (You lifted them from low places)
Na kuwaweka mbele ya wakuu (And placed them before leaders)
Ah, alipopingwa na maneno ya watu (Ah, when they were opposed by people’s words)
Na njama zikapangwa gizani (And schemes were plotted in the dark)
Lakini neema yako ikasema (But Your grace declared)
Hakuna atakaye wazuia (No one will stop them)
(Refrain)
Neema yako initangulie Bwana (May Your grace go before me, Lord)
Kila mahali nimepanga kutafuta (Everywhere I plan to seek)
Neema yako izungumze kwa ajili yangu (Let Your grace speak on my behalf)
Hata kabla sijafika eh (Even before I arrive)
Na Bwana kama yule anayepanga kunizuia eh (And Lord, anyone planning to stop me)
Aone mkono wako juu yangu (Let them see Your hand upon me)
Na yeyote anayehusika kufungua milango, eh (And anyone responsible for opening doors)
Aone kibali chako kimewaka juu yangu, oh (Let them see Your favor shining upon me)
(Refrain)
Discover more from African Gospel Lyrics
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
Leave a comment