Mtuliza Bahari (Calmer of Storms) Lyrics by Msanii Music Group

1 Comment


(Sung in Swahili)

Ee Baba tumekuja kwako (Father we have come before you)
Twaomba uturehemu (We ask that You have mercy on us)
Watoto wako, tu miguuni pako (Your children, we are at Your feet)
Tunalia kwa ajili ya mateso (We weep because of our affliction)
Tunayaona, tunapitia dunia hii (That we see, and encounter on earth)
Majirani wametugeuka sisi (Our neighbors have turned against us)
Hata mandugu wamekuwa maadui (Even our brothers have become enemies)
Wanatutesa kila usiku, kila kuchao (They persecute us daily)

Kimbilio letu ni wewe (Our refuge is You)
Kimbilio pekee, ni wewe (The only Refuge, is You)

Refrain:
(Bwana) Mwenye uwezo sisi twakutambua ([Lord] who is able we acknowledge You)
Tukilemewa tunajificha kwako (When we are overcome, we seek refuge in You)
Wewe ni mwamba, na si tu chini yako (You are the Rock, and we are beneath You)
Ukitamka jambo linatendeka (When You speak a word, it is done)
Hata mapepo yote hutawanyika (Even all the demons flee)
Nyosha mkono, Mtuliza Bahari (Stretch Your hand, Calmer of Storms)

Kuna wengi wapepoteza wapendwa wao (There are many who have lost their loved ones)
Kwa sababu ya chuki (Because of hatred)
Wapo wengi wamepoteza mali yao (There are many that have lost their wealth)
Kwa sababu ya wivu (Because of jealousy)
Kuna wengi wamepoteza mifugo (There are many who have lost their livestock)
Wamepoteza mimea yao shambani (They have lost their crops)
Na biashara yao ikaangushwa (And their businesses failed)

Kimbilio letu ni wewe (Our refuge is You)
Kimbilio pekee, ni wewe (The only Refuge, is You)

Siku ya kiyama inarejea (The Judgement Day is near)
Maswali mengi yataulizwa pale (Many questions will be asked there)
“Nilikupa jirani umtunze, mbona ukamtenda?” (“I tasked You to watch over your neighbor, why did you turn against them?”)
Miti na mawe ndio mashahidi (The trees and rocks will stand witness)
Paa la nyumba yaku litakukana (The roof of your house will denounce you)
Likishuhudia, uliyoyatenda (While witness your actions)

(Refrain)

Advertisement

Bwana U Sehemu Yangu (Lord, You are My Everlasting Portion) Hymn Lyrics by Msanii Music Group (Tenzi 116)

Leave a comment


(Sung in Swahili – A Hymn)

Bwana, u sehemu yangu (Lord, You are my everlasting portion)
Rafiki yangu, wewe (More than a friend to me)
Katika safari yangu (In my pilgrim journey)
Tatembea na wewe (Let me walk with You) (Repeat)

Pamoja na wewe (Together with You)
Pamoja na wewe (Closer to You)
Katika safari yangu(In my pilgrim journey)
Tatembea na wewe (Let me walk with You)

Mali hapa sikutaka (I do not seek worldly pleasures)
Ili niheshimiwe (That I be respected)
Heri nikute mashaka (Even if I encountered suffering)
Sawasawa na wewe (I’m safe as long as You’re with me) (Repeat)

Pamoja na wewe (Together with You)
Pamoja na wewe (Closer to You)
Na yanikute mashaka (Even if I encountered suffering)
Sawasawa na wewe (I’m safe as long as You’re with me)

Niongoze safarini (Lead me on the journey)
Mbele unichukue (And bear me there)
Mlangoni mwa mbinguni (At the gate of heavens)
Niingie na wewe (May I enter with You) (Repeat)

Pamoja na wewe (Together with You)
Pamoja na wewe (Closer to You)
Mlangoni mwa mbinguni (At the gate of heavens)
Niingie na wewe (May I enter with You)

Katika safari yangu(In my pilgrim journey)
Tatembea na wewe (Let me walk with You)
Heri nikute mashaka (Even if I encountered suffering)
Sawasawa na wewe (I’m safe as long as You’re with me)
Mlangoni mwa mbinguni (At the gate of heavens)
Niingie na wewe (May I enter with You)

Mbinguni ni Furaha (In Heaven there is Joy) Lyrics by Msanii Music Group

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Mbinguni ni furaha (In Heaven there is joy)
Hakuna matatizo (There are no more troubles)
Yesu ndiye mambo yote (Jesus is over all)
Tutaishi naye (And we shall live with Him) (Repeat)

Refrain:
Kule juu (Up above)
Mbinguni mwa Baba (At Father’s heaven)
Furaha tele tele (There is abundant joy)
Kwa walio wake (For those who belong to Him)(Repeat)

Jicho halijawahi kuona (No eye has ever seen)
Ndewe halijasikia (No ear has heard)
Yale Kristo kaandaa (What Christ has prepared)
Kwa walio wake (For those who belong to Him) (Repeat)

(Refrain)

Na we mwenzangu tubu leo (And You, my friend confess today)
Yesu haachi kuitana (Jesus will not stop calling)
Unayo nafasi leo (You have an opportunity today)
Njoo kukutana naye (Come and encounter Him) (Repeat)

(Refrain)

Nyoosha Mkono Wako (Stretch Out Your Hand) Lyrics by Msanii Music Group

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Kila siku twazidi kuwa wapotovu (Everyday we are corrupted)
Kwamba maadili Mungu alivyoagiza (By the standards God imparted us)
Tunatamani kuwa wakamilifu (We desire to be as perfect)
Kama mitume wa zamani (Like the apostles of old) (Repeat)

Refrain:
Nyoosha mkono wako, tufani zavuma (Stretch out Your hands, thunderstorms are intense)
Tuma malaika wako, tupe nguvu zako (Send Your angels to grant us Your strength)
Sisi tu wenye dhambi, Bwana turehemu (We are sinners, have mercy upon us)
Nyoosha mkono wako, tuweze kushinda (Stretch out Your hand, that we may win)
Nyoosha mkono wako, tuweze kushinda (Stretch out Your hand, that we may win) (Repeat)

Ulinzi wako uwe pamoja nasi (May Your protection surround us)
Ili tuweze kushinda majaribu (That we may overcome temptations)
Hatua kwa hatua, utupe ushindi( Step by step, grant us victory)
Tuongoze katika haki (Lead us into righteousness) (Repeat)

(Refrain)

Pengine Milimani (Perhaps to the Mountains) Lyrics Sung by Msanii Music Group

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Refrain:
Pengine milimani, utanituma niende (Perhaps You will send me to the mountains)
Pengine mabondeni, wataka nipeleke neno (Perhaps You intend for me to preach in the valleys)
Dhahiri sitakataa, wito wake Bwana Mungu (Certainly I will not refuse the call of the Lord God)
Niko hapa, nitume niende leo! (Here I am, send me today!)

Bwana ninaomba, hivi leo uniongezee nguvu (Lord I pray, that You increase my strength today)
Kwa maana sijui wataka niende wapi (For I do not know where You intend for me to go)
Ili jambo moja ni hakika, wala kamwe sina shaka (But one thing I know, and I will never doubt)
Unanitaka niende, nikahubiri neno lako (You want me to go and spread Your Gospel)
Unanitaka niende, nikahubiri neno lako (You intend for me to go and preach Your Word)

(Refrain)

Kwanza nitaanza hapa hapa kwa majirani zangu (I will begin right here with my neighbors)
Kwani nuru hii lazima, kwanza iangaze karibu (For this light must shine close)
Na ndipo hatua kwa hatua, shinde nitasonga mbele (And then step by step I will move forwards)
Kadri uniwezeshavyo, nilipeleke neno lako (According to how You enable me to spread Your Word)
Kadri uniwezeshavyo, nilipeleke neno lako (According to how You enable me to spread Your Word)

(Refrain)

%d bloggers like this: