(Sung in Swahili)

Toka mwanzo nilijua, Mungu atafanya (From the beginning I knew God will do)
Sababu najua, Hashindwi (For I knew He cannot be defeated)
Ila nilidhani, Mungu atafanya (But I thought that God will do)
Sawasawa na mawazo yangu (According to my thoughts)
Kumbe ninavyowaza, ni tofauti (But what I thought was different)
Na Mungu anavyoniwazia (From what God desired for me)
Leo amenishangaza Bwana (Today my God has surprised me)
Amefanya zaidi ya niliyo waza (By doing more than I ever thought)

Refrain:
Baraka, kanipa zaidi ya nilivyo omba (Blessings, He gave me more than I prayed for)
Amenipa kicheko (He has given me laughter)
Watoto, kanipa zaidi ya nilivyo omba (Children, He gave me more than I prayed for)
Amenipa kicheko (He has given me laughter)
Afya, kanipa zaidi ya nilivyo omba (Health, He gave me more than I prayed for)
Amenipa kicheko (He has given me laughter)

Ametenda zaidi ya mawazo yangu (He has done more than my thoughts)
Bwana amenipa kicheko (The Lord has given me laughter) (Repeat)

(Refrain)

Anasema anajua ninayohitaji (He says that He knows what I need)
Hata kabla sijaomba (Even before I pray)
Kuna vitu ninadhani sihitaji (There are things I think I do not need)
Ila yeye anajua ninahitaji (But He knows that I need them)
Nikimwomba mkate, ananipa na maji (When I pray for bread, He gives me water too)
Anajua nitapata kiu tu (For He knows I will be thirsty)
Nisiyo yajua, ye anayajua (What I do not understand, He knows)
Hata kama ni mambo madogo tu (Even if they are minor things)
Mahitaji yangu leo, mahitaji yangu kesho (My needs for today and tomorrow)
Leo amenishangaza Bwana (The Lord has amazed me today)
Amefanya zaidi ya niliyo waza (For doing more than I thought)

Ametenda zaidi ya akili/mawazo yangu (He has done more than my thoughts)
Bwana amenipa kicheko (The Lord has given me laughter) (Repeat)

(Refrain)

Ahsante Yesu x3 (Thank You Jesus)
Umenipa zaidi x2 (You have given me more)
Amenipa kicheko (He has given me laughter)

Advertisement