Usife Moyo (Do Not Give Up) Lyrics by Beatrice Mwaipaja and Frank Mwangoka

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Shida na raha binadamu sisi zote tunapitia (As humans we pass through joy and grief)
Ila shida ikizidi (Though when trouble overwhelms us)
Majaribu yanakuwa mengi (Temptations abound)
Wakati mwingine unaweza kufikiri (At times you may think)
Kwamba mungu hakuoni (That God does no see you)
Jinsi unavyopata taabu (How you are passing through misery)
Wakati mwingine unaweza kufikiri (Other times you may think)
Kwamba Mungu hakuoni (That God does not see you)
Ndoa yako inavyoingia doa (And how your marriage is in trouble)

Unaweza kwenda mbele zaidi (You can go far thinking)
Hivi kweli Mungu yupo (and doubting if truly God is there)
Mbona mimi hanisaidii? (Why does He not help me?)
Mara ukaacha na kusali (And you stopped praying)
Na ukahama makanisa (And you left church)
Kwa kuikosa imani (For lack of faith)
Mara ukaacha na kusali (You then stopped praying)
Na ukahama wachungaji (And left your pastors)
Kwa kuikosa imani (For lack of faith)

Mungu yupo, asikia maombi yako (But God is here, he listens to your prayers)
Endelea kumwomba yeye, utapata majibu yako (Continue to pray, You will receive your answers)
(Repeat)

Iko siku na saa iliyoandaliwa kwa ajili yako (There is a day prepared for you) x2
We Usife moyo, we usife moyo (Do not give up, do not lose heart)
Endelea kumwomba yeye, utapata majibu yako (Continue to pray to Him, you will receive your answers)
We Usife moyo, we usife moyo (Do not give up, do not lose hope)
Endelea kumwomba yeye, aijuaye kalenda (Continue to pray to Him who knows the time)

(We) Usife moyo, wakati wako bado (Do not lose heart, your time has not arrived)
Pale unapokataa tamaa (Where you lose hope)
Ndipo hapo Mungu yupo (That is where God is)
Mungu yupo, asikia maombi yako (God is there, He listens to Your prayers)
Endelea kumwomba yeye (Continue to pray to Him)
Utapata majibu yako (You will soon receive your answers) (Repeat)

Ameyatenga majiri, kwa sababu zake (He has set aside time for His cause)
Na kwa utukufu wake, Baba (And for His Glory, as the Father)
Majira ya kulia (Times of tears)
Na majira ya kucheka (And times of laughter)
Kwa makusudi yake (For His purposes)

Kwa nini ukate tamaa (Why should you give up)
Kwa sababu leo (Because today)
Unapitia wakati mgumu? (You are going through troubled times?)
Kwa nini urudi nyuma wewe (Why should you backslide)
Kwa sababu leo (Because today)
Mi majira yako ya kusubiri? (Is your time of wait?)
Kwayo majira ya kusubiri (In the time of waiting)
Mungu anataka kujitolea utukufu (God wants to glorify Himsekf)
Kwa wakati unaolia, (In the times of your tears)
Huo ni wakati wa Mungu (That is the time of God)
Wa kupata heshima yake (To receive His Honor)
Jua ni kwa muda tu unalia (Know that weeping is only for a while)
Jua ni kwa muda tu unasubiri (Know that waiting is just for a time)
Ooh atatenda (Oh, He will do it)

(Refrain)

Mpenzi wa Roho Yangu (Lover of my Soul) Lyrics by Beatrice Mwaipaja

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Yeye aliyeuteka moyo wangu (The one who captured my soul)
Yeye aliyeujaa moyo wangu (The one who has filled my spirit)
Yeye aliyeifia nafsi yangu mimi (The one who died for me)
Nimekaa natafakari juu ya pendo la kweli (I have reflected on His true Love)
Ninalolipata kwake (That I received from Him)
Nimekaa najiuliza juu ya pendo la kweli (I have sat and reflected on His true Love)
Analonionyesha kwangu, Mungu (That God has shown me)

Aliyebadilisha maisha yangu (The one who changed my life)
Anayepigana na adui zangu (The one who fought against my enemies)
Aliyeweka amani moyoni mwangu (The one who places peace in my heart)
Sitamani mwingine (I desire no other) (Repeat)

Maumivu alinifutia (He wiped my grief)
Kwa maneno ya upendo (With his loving words)
Msalabani alinifia (He died on the cross for me)
Nitampenda milele (I will love Him forever) (Repeat)

Refrain:
Response: Wa roho yangu ni Mungu (Of my Soul is God)
Mpenzi wa roho yangu ni Mungu x4 (The lover of my soul is the Lord)
Wa roho yangu ni Mungu, mimi (Of my soul, mine)
(Repeat)

Thamani ya maisha yangu, anayeijua niye (Only He knows the value of my life)
Thamani ya uzima wangu, anayeijua niye (Only He knows the value of my life)
Gharama ya wokovu wangu, anayeijua niye (Only he knows the cost of my salvation)
Ukiniona nina furaha, yeye furaha yangu (When you see me joyful, He is my joy)
Ukiniona nina uzima, yeye uzima wangu (When you see me alive, He is my life)
Mpenzi wangu, mimi (My Love)

Ananipenda, nami nampenda (He loves me and I love Him)
Ananipenda, tunapendana (He loves me, we love each other)
Nani kama yeye, Mungu hakuna kama ye
(Who is like Him? God there is no one like Him)
Ana pendo la kweli, pendo lake halichuji
(He has true Love: His love does not discriminate)
Ananipenda, nami nampenda (He loves me, and I love Him)
Yupo karibu nami, majira yote (He is near to me all the time)
Tena zaidi hata ya nguo niliyovaa (Closer than even the clothes I wear)

Kwenye ndibwi la penzi lake, sijawahi kujutia
(In the lake of His Love, I have never regretted)
Nimezama kwa pendo lake, ili nisije jutia
(I have sunk into His Love, that I may never regret it)
Ananipenda sana ye, mpenzi wangu
(He loves me so, my Love)
Ninampenda sana ye, mpenzi wa roho yangu
(I love Him so, the lover of my soul)
(Repeat)

(Refrain)