Love on Fire Lyrics by Walter Chilambo

Leave a comment


(Languages: Swahili, English)

Hivi nakupendaje? (How much do I love You!)
Hata mwenyewe sijielewi (So much that even I cannot understand myself)
Ninakupendaje? Namna hii Bwana (How much do I love You, like this)
Hivi umenipokeaje? (The way You have received me)
Maana nasikia raha sana (I am filled with joy)
Umenipokeaje? (Namna hii Bwana) (The way You have received me)
I deserve Nothing (Nothing)
Lord you give me everything
You never disappoint me
Oh Lord in any way

Bridge:
Yaani hata mi nikianguka, Bado (Even when I fall, Still)
Mkono wangu unanishika, Bado (You hold my hand, Still)
Kwenye mitego ya Muovu, Bado (In the snare of the evil one, Still)
Baba yangu unanivusha, Bado (Father You still ferry me, Still)

Refrain:
Tarararira, Jesus your my desire
Tarararira Your Love is on fire
Tarararira What did I do-did I do
Tarararira, Nistahili upendo wako wee? (To deserve Your Love?)

Nami nitatii, amri zako Daddy (I will listen to Your commands, Father)
Nifanye safi, mwili na roho Daddy (To cleanse my body and Spirit, Father)
Usiniache kabisa (Usiniache kabisa) (Do not leave me)
Maana kwa wengine mi ni takataka (For to others I am rubbish)
Kwako mi dhahabu (But to You I am like gold)
Maana umeniosha mi nawaka waka (For You have washed me until I gleamed)

(Bridge + Refrain)

Ninaringa unanipenda (I boast of Your Love)
Unanilinda (You guard me)
Wanitunza (You care for me)
Eeh Bwana wangu (Oh my Lord)
Nzambe na ngai (My God)
Shammah (The Lord is There)
El Shaddai (Lord Almighty)

(Refrain)

Unaniona (You See Me) Lyrics by Walter Chilambo

1 Comment


(Sung in Swahili)

Kama Mungu angechangua watu wake (If God selected His people)
Mimi singekuwepo duniani (I would not be here on earth)
Kama Mungu angechagua watakatifu (If God selected the Holy ones)
Mimi singekuwepo duniani (I would not be here on earth)

Refrain:
Mimi binadamu, wala si malaika (I am but a human, not an angel)
Mengi nimekosea na kukuchukiza (I have wronged and offended You)
Mi nafanya mambo yasiyo stahili (I have done things I should not have)
Nimevuruga vuruga mipango yako (I have disrupted Your plans)
Wanihurumia (Yet You have mercy on me)
Mbele ya macho ya wanadamu (Before human eyes)
Nilikuwa nikijificha (I was hiding)
Kumbe wewe waniona (But You see me)
Kwa kujifanya mtakatifu (By pretending to be Holy)
Tena bingwa mkarimu (And a generous victor)
Nilikuwa/(Kwenye ibada) mnyenyekevu (I was/in worship humble)
Tena mpole sana (Also submissive) (Repeat)

Kumbe Mungu, unaniona/unionae (Truly God You see me/who sees me)
Macho yako, yanitazama/yanitazamae (Your eyes gaze at me/sees me)
Sikio lako, yanisikia (Your ear, hears me)
Siwezi jificha (I cannot hide) (Repeat)

Sasa nimetambua, mbivu na mbichi ni zipo (I have now learned to differentiate)
Sasa ninaelewa, njia salama ni wapi (Now I know where the true path lies)
Na nimejua bila ya wewe sifiki (And have understood, without You I will not arrive)
Hata nikila pasipo neno lako sishibi (Even if I eat without Your word, I am not satisfied)

Neema yako, ila kwa neema yako (Your Grace, it’s only by your Grace)
Upendo wako, kwa upendo wako (Your Love, by Your Love)
Rehema zako zimeniimarisha tena (Your mercies reestablishes me) (Repeat)

(Refrain)

Asante (Thank You) Lyrics by Walter Chilambo

1 Comment


(Sung in Swahili)

Asante Mungu, wewe ni mwema (Thank You God, You are good)
Umenipa uzima, na kunipenda (You have given me life and loved me)
Moyoni mwangu nina amani tena (I have peace in my heart once again)
Nimeacha yote niliyoyatenda (I have abandon all I did before)

Nimeamua nikufuate maana we ni salama (I have resolved to follow you for You are a refuge)
Mbele yako najinyenyekeza eh Mungu wa huruma (I humble myself before you, Oh God of Mercy)
Nimeamua nikufuate kwa maana we ni salama (I have resolved to follow you for You are a refuge)
Nang’ang’ania nisikuache Mungu wangu (I struggle that I may not abandon you My God)

Response: Oh Mungu (Oh God)
Asante kwa kunipenda (Thank You for loving me)
Asante kwa kunilinda (Thank You for protecting me)
Milele nitaimba sifa zako (I will forever sing Your Praises)

Niende wapi, niukimbie uso wako? (Where can I go to run away from Your presence?)
Niende wapi, nijiepushe na roho yako (Where can I go to hide from Your Spirit?)
Kwako Bwana, Bwana umenichunguza na kunijua (In You Lord: You have searched me and known me)
Nakushukuru kwa wema wema wako Bwana (Lord I thank You for Your Goodness)

Unilinde na mabaya yote yasinipitie (Protect me that I may not encounter evil)
Unioshe Bwana, kwa damu yako nisiangammie (Wash me Lord, with your blood that I should not perish)
Unilinde na mabaya yote yasinipitie (Protect me that I may not encounter evil)
Unioshe Bwana, kwa damu yako nisiangammie (Wash me Lord, with your blood that I should not perish)

Asante, asante, asante (Thank You, thank You, thank You)
Bwana Asante, asante Bwana (Lord thank You, thank You Lord)
Kwa kunipenda (For loving me)

(Refrain)

Asante, asante, asante (Thank You, thank You, thank You)
Mungu wangu (My God) (Repeat)

%d bloggers like this: