(Sung in Swahili)

Nafsi yangu usichoke, roho yangu msifu Bwana
(My self do not tire, my spirit praise the Lord)
Alihadi atatenda, mtumanie Bwana
(He promised he will do it, trust in the Lord)
Ahadi zake ni za milele, akiahidi atatenda
(His promises are forever, if he promises he will do it)
Roho yangu nafsi yangu, mtumainie Bwana
(My spirit my self, trust in the Lord)

Chorus:
Kama mvua ishukavyo, toka mbinguni kwenye ardhi
(As the rain pours, from heaven on earth)
Na neno lake kwa kinywa chake, halitarudi bure
(So his words from his mouth, will not return in vain)
Litatimiza mapenzi yake, litatenda alivyo sema
(It will accomplish his will,it will do as he says)
Aliahidi atatenda, mtumainie Bwana
(If he promises he will do it, trust in the Lord)

Verse 2:
Mawazo yake sio yetu, njia zake si kama zetu
(His thoughts are not ours, his ways are not like ours)
Mbingu zilivyo juu ya nchi,mawazo yake ni makuu
(As the heavens are above, his thoughts are great)
Ataagiza fadhili zake, wimbo wake kwangu usiku
(He will instruct his mercies, his song to me at night)
Sifadhaike usiiname, mtumainie bwana
(Do not despair do not falter, trust in the Lord)

(Chorus)