(Sung in Swahili)

Yesu aliyesulubiwa (Jesus who was crucified)
Amefufuka anaishi milele (Is risen and lives forever)
Mikononi mwa miguuni mwake (On his hands and feet)
Alama kubwa za misumari (The marks of the nails)
Uso wang’ara kama jua (His face shines like the sun)
Macho kama miale ya moto (His eyes lie tongues of fire)
Mavazi yake meupe yaangaza (His white garments glow)
Kushinda chote kilujulikanacho (Like nothing else in the world)

Wayahudi walimuua Yesu (The Jews killed Jesus)
Wakafikiri yote yamekwisha (And thought all is done)
Jiwe kubwa likabingirishwa (They rolled a large stone)
Mlangoni mwa kaburi kale, lakini (In the front of his tomb, but)

(Refrain)

Askari walinzi wakawekwa (Guards were placed)
Mbele ya lile kaburi (In front of the tomb)
Usiku mchana walilinda (All day they guarded)
Asije akabebwa Yesu, lakini (That Jesus body would not be stolen, but)

(Refrain)

Spoken:
Baada ya Yesu kufa msalabani na kuzikwa kaburini
(After Jesus died on the cross and buried)
Wale wanawake waliondoka asubuhi
(Those women left in the morning)
Wakiwa na manukato, kwenda kuupaka mwili wa Yesu
(With perfume, to anoint Jesus’ body)
Wakalikuta lile jiwe limebingirishwa mbali na lile kaburi
(They found the stone unrolled far from the tomb)
Walipokuwa wamesimama pale na kufadhahishwa na jambo hilo
(When they were standing there despairing of this)
Malaika wawili walitokea na kuwauliza
(Two angels appeared and asked them)
“Mbona mnamtafuta aliye haki kati ya wafu?”
(Why are you looking for the righteous one among the dead?)
“Hayupo hapa, amefufuka!”
(He is not here, He is risen!)

Tetemeko la nchi likazuka (An earthquake appeared)
Malaika toka mbinguni (Angels appeared from heaven)
Askari wakashikwa na hofu (The guards were terrified)
Wakaanguka kama wafu (And fell like the dead)

(Refrain)

Makaburi ya watakatifu (The graves of the righteous)
Yote yalifunguliwa (All were opened)
Wakaonekana na watu wengi (They were seen by many people)
Penye nchi mtakatifu (In the glory land)

(Refrain)