Chorus:

Natafuta ufalme wa Mungu na utakatifu wake
Na vitu vyote vile vizuri, nitaongezewa kama ugali sosa
Huwezi pewa ugali sosa kama bado hujanunua
Basi mwenzangu mtafute Mungu, utaongezewa ugali sosa

Verse 1:

Kuna hoteli ambayo mi huenda, kukamata ugali na supu ya magoti
Mara tu mlima wa ugali ukifika, naanza kufanya test za mluhya
Ya kwanza nafinya ugali, inachomoka pande zote za mkono
Ya pili navumba ugali tupa kwa ukuta, narudi kama tennis
Ya tatu napuliza ugali, na moshi nyeupe inaenda spiral
Ugali inapata certificate, waiter leta sosa

(Chorus)

Verse 2:

Naanza kusakata ugali, namega ugali hapo kwa ngotitsa
Halafu namwona wepukhulu, kumbe alikuwa upande ule wa meza
Waiter anamkaribia anamwuliza nikupe nini Bwana
Wepukhulu anasema, ugali sosa na kadhalika
Waiter anasema excuse me? Wepukhulu anazusha
Mabouncer wakambeba juu, wakamtandika, chonga viazi

(Chorus)

Verse 3:

Sasa wasee iko hivi, tabia mbaya lazima tutawacha
Tunataka baraka zake Mungu, lakini tunakataa Mungu mwenye baraka
Tunataka tupate uponyaji lakini tunakataa Yesu mwenye kuponya
Tunapenda sana miujiza lakini hatumpendi Mungu mwenye kutenda
Ni lazima tutatubu wapendwa, tubadili mienendo tumtafute Mungu
Ukidharau mambo hii nasema, haki roho safi utachonga viazi