Verse 1:

Yesu kamwambia, mwanamke msamaria kisimani
Hao wanaume ulio nao hawamalizi kiu, kunywa maji
Ee dada kunywa maji, kunywa maji
Kwani ukinywa haya hamna kiu tena
Minisketi hipster fashioni Hazimalizi kiu kunywa maji

Chorus

Kunywa maji, Kunywa maji,
Kunywa maji, ya uzima

Verse 2:

Mzee mbona kiu, na maji yapo, Kila siku pombe, sigara mdomoni
Leo ni atoti, kesho ni wanjiku, Watakumaliza kunywa maji
Kijana nakwambia usidanganyike, Raha za dunia, hazimalizi kiu
Madawa ya kulevya na dot komu, Hazimalizi kiu kunywa maji

(Chorus)

Verse 3:

Ee mama Kunywa maji uache fitina,
Wivu masengenyo na mashindano
Maji ya uzima, furaha tele
Kila siku mama ni haleluya

(Chorus)

Wacha pombe, Kunywa maji ya uzima

(Chorus)