(Sung in Swahili)

Nawatangazia mganga wangu Yesu, Ayeyeyeye
(I declare to you, that my healer is Jesus)
mganga wa kweli eh, njoni niwaonyeshe
(The true healer he, let me show you)

Chorus:
Mimi nimemwona (mganga), nimemwona (mganga)
(I have seen Him (the physician), I have seen Him (the physician)
Nimemwona (Mganga wa waganga ni Yesu).
(I have seen Him (the Great Physician is Jesus)

Nasema nimemwona. Mganga wa waganga
(I say I have seen the Great Physician)
Anayeinamiwa na waganga wote hata na wachawi pia
(That is worshipped by all physicians and even witch-doctors)
Wanaleta madawa yao hata na hirizi
(They bring their medicine, and even their charms)
Na wanatangaza maovu yote walotendea wanadamu
(And they confess the evil they did to men)
Huyu mganga, kazaliwa Bethlehemu
(This Great Physician was born in Bethlehem)
Kalelewa na  na zarati la ajabu ni mwana wa bikira
(And came by a great miracle – he is the son of a virgin)

(Chorus)

Jina la huyu mganga, kwa kweli lanishangaza
(The name of this Physician, is awe inspiring)
Kwa maana linalo nguvu nyingi kama mganga mwenyewe
(Because it has as much power as the Physician Himself)
Lilipotajwa na Petero, Tabitha akafufuka
(When it was said by Peter, Tabitha was raised from the dead)
Kiwete njiani akatembea kwa ajili la hilo jina
(The cripple by the road walked because of that name)
Paulo na Sila wakasifu kwa hilo jina
(Paul and Silas worshiped by that name)
Milango ya gereza ikafunguka kwa jina la mganga Yesu
(The doors of the jail opened because of the Physician Jesus)

(Chorus)

Nguo za huyu mganga, hata nazo zina nguvu
(This Physician’s clothes, have power too)
Mama aliyevuja damu alipenya katitati ya umati
(The woman with bleeding passed through the crowd)
Nguvu za upinde wa nguo, damu ikakatika
(Through the power of the hem, the bleeding stopped)
Yesu akamwambia imani yako ndiyo imekuponya
(Jesus told her that her faith was what healed her)
Baada ya kusulubiwa, nguo za huyu mganga
(And after his cricifixion, this Physician’s clothes)
Hazingepasuliwa kwa bei yake ikapigiwa kura
(Because of its value would not be torn; instead they cast lots for it)

(Testimony)

(Chorus)

Advertisement