(Sung in Swahili)

Spoken:
Ulimwengu wetu huu kuna anasa nyingi
(In our world there is a lot of pleasures)
Nazo zimewavuta watu wengi
(And they have attracted many people)
Wanaume kwa wanawake, wasichana kwa wavulana
(Men and women, girls and boys)
Hata hawawezi kugundua kuwa mambo haya yatafika mwisho wake
(So much that they do not realize that they have an end)
Tuna mifano hai katika Biblia
(We have living examples from the Bible)
Kama wakati wa Sodoma na Gomora
(Like the time of Sodom and Gommorah)
Watu walitenda maovu, hata wakamchukiza muumba
(People did evil, that they disgusted the Creator)
Muumba naye akashindwa kuwavumilia, akawaadhibu kwa moto
(The Creator could no longer be patient with them, he punished them with fire)
Tunasoma pia wakati wa Nuhu
(We also read about the times of Noah)
Watu walitenda maovu, hadi Mungu akaghadhabika
(People did evil, that God was angered)
Akawaadhibu kwa gharika
(He punished them with the flood)
Kadhalika na ulimwengu wetu huu
(So is the same with our current world)
Watu wanaendelea kutenda maovu
(People continue to do evil)
Hawawezi kugundua kuwa, yatafika mwisho wake
(Without realizing that it has an end)
Lakini ndugu yangu mpendwa,
(But my beloved brother)
Jua kwamba ulimwengu huu utafikia mwisho
(Know that this world has its end)

Wakati ule wa, Nuhu (At the time of Noah)
Watu walimwasi Bwana (People rejected God)
Walitenda kila, dhambi (They committed every sin)
Wakamsahau mu-umba (They forgot their Creator)

Walimchukiza, muumba wao (They disgusted their Creator)
Kwa dhambi zao, nyingi (With their many sins)
Mungu alia-mua kuua (God decided that to wipe)
Kila kiumbe, chote (All creatures from the face of the earth)

Mungu kamwambia, Nuhu kwamba (God told Noah to)
Afanye safina, yenye dumba (Build a wooden ark)
Aifunike ramli, ndani na nje (To cover it with tar inside and out)
Urefu wake, mikono mia tatu (Its height: 300 hands)
Upana wake, mikono hamsini (Its width: 50 hands)
Kwenda juu kwake, mikono thelathini (Its height: 30 hands)

Naye Nu-hu ali-i-jenga safina (And Noah built the ark)
Alipo-maliza kaambiwa ingia (When he finished, he was told “Enter”)
Wewe na mkeo na wato-to wako (“You and your wife and children”)
Pia na, wake za-o nao, waingie (“Also their wives should enter too”)

Mvua nayo ilianza kunyesha bila kukatika (And the rain started without ceasing)
Maji yalieendelea kuongezeka (Water continued to rise)
Kutoka kisiginoni kwenda magotini (From the heel to the knee)
Kutoka magotini kwenda kifuani (From the knee to the chest)
Watu wakakumbuka maneno ya Nuhu, alisema (And people remembered Noah’s words)
Walipanda kwenye milima, hawakupona (They climbed mountains, but did not survive)
Wengine kupanda kwenye miti, hawakupona (Others climbed trees, but did not survive)
Wajuzi wa kuogelea hawakupona (The ones who could swim did not survive)
Wengine waliogelea mpaka kwa Nuhu (Others swam to Noah)
Wakasema Nuhu utufungulie, tunakufa (Asking for him to let them in)

Nuhu aliwaambia sikufunga mimi (Noa told them “I was not the one to close the door”)
Waliangamia wote wakafa kwa maji (They all perished in the water)
Wanyama nao waliangamia, wakafa kwa maji (The animals too, perished in the water)
Ndege waliangamia, wakafa kwa maji (The birds also perished in the water)

Kama ilivyo kwa siku za Nuhu (As was the days of Noah)
Nd’o ilivyo ha-ta sasa (That is how it is today)
Matendo yale yaliyotendeka (All the actions that was taken)
Nd’o yatendeka ha-ta leo (That are being done today) (Repeat)

Ulevi na uchawi zimewafunga wengi (Drunkenness and witchcraft has bound many)
Kutafuta mali kumewafunga wengi (The search for riches has bound many)
Uzinzi na uwongo zimewafunga wengi (Adultery and lies have bound many)
Wengi wamesahau mkombozi wao, wamemwacha (Many have forgotten their savior, and left Him)
Siku ya mwisho hakuna kujitetea (In the final days, there is no advocate)

Wenye haki wote wataingia mbinguni (The faithful ones will enter heaven)
Wenye dhambi wote watatupiwa motoni (The sinful ones will be thrown in the fire)

Advertisement