Wakati nitajikuta, mbinguni kwa Baba (When I shall find myself in my Father’s heaven)
Nitajua ya ulimwengu nimeshayaacha (I will know that the earth’s is over)
Haleluya nitasifu, kufika mbinguni (Hallelujah I will praise, on getting to heaven)
Hosana! nitaingia kwa shangwe (Hosanna! I will enter with praise)

Refrain:
Nitaingia lango lake na sifa moyoni (I will enter His gates with praises in my heart)
Nitaingia kwa shangwe kuu (I will enter with great praise)
Nitasema ni siku njema bwana ameifanya (I will say it is a good day that the Lord has done)
Nitafurahi kufika mbinguni (I will be glad to reach heaven) (Repeat)

(Refrain)

Nchi nzuri nchi safi, kwa Baba yangu (My Father’s place is good)
Kuna amani kuna furaha, huko ni kusifu (There is peace and Joy, it is all praise there)
Tutakaa na Mungu wetu, nchi ya amani (We shall stay with Our God, in that peaceful place)
Hosana! nitaingia kwa shangwe (Hosanna! I will enter with praise)

(Refrain)

Nitawaona watakatifu, manabii wote (I will see the righteous ones and all the prophets)
Hata mitume nchi hiyo, nitawaona (Even the apostles, I will see them in that place)
Tutakula meza moja, nchi ya amani (We shall all eat at one table, in the peaceful place)
Hosana! nitaingia kwa shangwe (Hosanna! I will enter with praise)

(Refrain)

Advertisement