(Sung in Swahili)

Anatupenda (He loves us) x3

Maisha ya mwanadamu (The life of a human)
Kuishi kwake huwa mara moja (Their living is only for one time)
Yakishapita, huwezi kuyarudisha (Once it is over, it cannot be redone)
Mbona twaishi, twaishi kwa nguvu za Mungu pia uwezo wake (The way we live, is by His Power and Might)
Tumkumbuke Mungu, siku za uhai wetu (Let us remember God, in the days of our lives)
Kama unataka muujiza, ni huu hapa sasa (If You need miracles, then here it is)
Wa wewe kuamka (For You to rise up)

Je ni wangapi wamelala, wameshindwa kuamka (How many have slept, unable to rise)
Kwani we ni nani? (For who are You?)
Au unafikiri uzuri wako, umekufanya uwe hai (Or do you think ir is your goodness that has spares you)
Au ni daktari wako (Or it is your doctor)

Si kwa nguvu zangu mimi, wala nguvu zako wewe (It is not by my might or your might)
Ni kwa nguvu zake Mungu (It is through God’s might)
Ndio maana tupo hai, anazidi kutulinda (That is why we live, he continues to care for us)
Ameonekana kwetu (He shows himself to us)

Refrain:
Nifundishe kukutegemea (Teach me to rely upon You)
Kwa hali zote ninazopita (In all my situations)
Hata kwa magumu yote (Even in times of hardship)
Wewe ndiwe kimbilio langu, na ngome yangu (You are my refuge and fortress)
Halleluya (Hallelujah) (Repeat)

Wanijua Baba (You know me Father) x3

Alisema giza liwe, nalo likawa (He commanded darkness, and it came to be)
Kwa fimbo, Musa bahari akaligawa (With his staff, Moses divided the sea)
Tanuru aliwaacha midomo wazi (At the fire, they were left amazed)
Mtu wa nne katoka wapi? (Where did the fourth person come from?)
Kwa kuguza pinde, yule mama kapona (By touching the hem, the bleeding woman was healed)
Batimayo naye, kapona kwa mate na tope (Bartimaeaus was healed by spit and mud)
Hajaanza jana, na wala haishii leo (He did not start yesterday, and will not stop today)
Ni Mungu wa Yakobo, Daudi, milele amina (He is the God of Jacob, David, forever Amen)

Hebu fikiria imani yako hivyo ndogo (Think about your little faith)
Na matendo yako bado, anakulinda bado (And even with your actions, He still cares for you)
Ni dhahiri kuwa Mungu wetu huyu (It is clear that our God)
Anatupenda, anatupenda, anatupenda (He loves us, He loves us)
Anakupenda ulivyo wewe (He loves us the way you are)
Anatupenda, anatupenda, anatupenda (He loves us, He loves us)

(Refrain)

Anatupenda (He loves us) x3

Anakupenda ulivyo, ulivyo wewe (He loves you, just as you are)
Ikiwa shwari mimi ninaimba (When it is all calm, I will sing)
Halelluya, Halelluya, Halelluya (Hallelujah! )
Hata kwenye vikingi nitaimba (Even in times of troubles, I will sing)
Halelluya, Halelluya, Halelluya (Hallelujah! )
Ikiwa shwari mimi nitaimba (When it is all calm, I will sing)
Usifiwe, usifiwe, usifiwe (Be praised, be praised, be praised)

Advertisement