(Sung in Swahili)

Refrain:
Kishindo cha wakoma (The roar of the lepers)
Kiliwakimbiza Washami (Caused the Arameans to flee)
Kishindo cha wakoma (The roar of the lepers)
Kiliwakimbiza Washami (Caused the Arameans to flee)
Mungu akiwa upande wetu (When God is on our side)
Ni nani aliye juu yetu? (Who can be above us?)
Mungu akiwa upande wetu (When God is on our side)
Ni nani aliye juu yetu? (Who can be above us?)

Njaa ilipowakabili (When hunger overwhelmed them)
Wenye ukoma waliotengwa (The lepers who were separated)
Wakasema “Kuliko tufe hapa kwa njaa (They resolved that “Rather that we die of hunger)
Ni bora twende kambi la Washami (It is better to go to the Aramean camp)
Ni maadui zetu siku zote (They have been our enemy for all day)
Twendeni tuombe chakula (Let us go and borrow food)
Na tena huenda tuka uwawa (There is likelihood of being killed)
Lakini bora kambi la Washami “ (But better the Aramean camp”) (Repeat)

Walipokaribia kambi la Washami (When they came near the Aramean camp)
Washami wakasikia kishindo cha magari (The Aramean heard a roar of chariots)
Kishindo cha magari ya Waisiraeli (A roar of Isralite chariots)
Na kumbe zilikuwa nyayo za wakoma (But it was only the lepers footprints)
Zilizojawa uwezo wa Mungu (That was filled with the might of God) (Repeat)

(Refrain)

Wahitaji msaada ndugu? (Brethren do you need aid?)
Je, watambua kwamba yuko Mungu (Do you know that there is a God)
Awezae kurahisisha magumu tusiyoyaweza? (That would ease your heavy burden?) (Repeat)

Waweza kumwita El Shaddai (You can call Him El Shaddai)
Waweza kumwita Adonai (You may call Him Adonai)
Waweza kumwita Elohimu (You may call Him Elohim)
Mungu aliye karibu na watu (God with us) (Repeat)

Na hata sasa Bwana ametupigania (And even now God has fought for us)
Pigania kwa ushindi (Fought with victory)
Na tutashinda zaidi ya kushinda (And we shall be more than victorious)
Kwa yeye aliyetupenda x3  (In Him that loves us) (Repeat)