(Sung in Swahili)

Usisahau hata kidogo (Never Forget)
Usisahau kumshukuru (Do not forget to thank Him)
Yale yote Mungu aliyo kutendea (For all that God has done for You)
Usisahau kumshukuru Mungu (Do not forget to thank God) (Repeat)

Basi hapo moyo wako wewe (Now do not let your heart)
Usiinuke ukamsahau Mungu wako (Rise up and forget your God)
Aliye kutoa katika nchi ya Misri (That rescued you from Egypt)
Aliye kutoa katika nyumba ya utumwa (That removed you from the house of slavery) (Repeat)

Aliye kuongoza katika jangwa lile kubwa (The one who led you through the great desert)
Lenye vitisho, lenye nyoka za moto (The terrifying land with fiery snakes)
Lenye nge, nchi yenye kiu (Land of scorpions, land of thirst)
Nchi ‘siyokuwa na maji (The land with no water) (Repeat)

Aliye kutolea maji kata mwamba mgumu sana (The One who gave you water from a rock)
Aliye kuongoza njia katika safari yako (The One who led you on the journey)
Aliye kulisha jangwani kwa mana, mana (The One who fed you in the desert with Manna)
Wasio ijua baba zako (Without caring for your origins) (Repeat)

Refrain:
Katika mema yako (In your goodness)
Na katika mafanikio yako (And in your success)
Wala usiseme moyoni mwako “Nguvu zangu (Do not be tempted to say in your heart “It is my strength)
Na uwezo wangu, ndio uliyonipatia (And my might that made it possible)
Utajiri huu” (for these riches”) (Repeat)

Refrain 2:
Bali mkumbuke Bwana wako maana (But remember your Lord for)
Ndiye akupae nguvu za kupata utajiri (He is the giver of the strength  to seek success)
Ili afanye imara (So that He may affirm)
Agano lake Bwana, Mungu (The Lord God’s covenant) (Repeat)

Basi yatupasa kutambua Bwana Mungu ndiye, ndiye (Not it is necessary for us to acknowledge that the Lord God is)
Atanguliaye mbele yako kama moto (The one who goes before you like the fire)
Uteketezao, na kuangamiza (That burns and destroys)
Walio watesi wako (wako, wako, wako!) (Those who torment you (You, you, you!)) (Repeat)

(Refrain + Refrain 2)

Usisahau hata kidogo (Do not forget at all)
Usisahau kumshukuru (Do not forget to thank Him)
Yale yote Mungu aliyo kutendea (For all that God has done for You)
Usisahau kumshukuru Mungu (Do not forget to thank God) (Repeat)

Advertisement