Ugali Sosa Lyrics by Man Ingwe

Leave a comment


Chorus:

Natafuta ufalme wa Mungu na utakatifu wake
Na vitu vyote vile vizuri, nitaongezewa kama ugali sosa
Huwezi pewa ugali sosa kama bado hujanunua
Basi mwenzangu mtafute Mungu, utaongezewa ugali sosa

Verse 1:

Kuna hoteli ambayo mi huenda, kukamata ugali na supu ya magoti
Mara tu mlima wa ugali ukifika, naanza kufanya test za mluhya
Ya kwanza nafinya ugali, inachomoka pande zote za mkono
Ya pili navumba ugali tupa kwa ukuta, narudi kama tennis
Ya tatu napuliza ugali, na moshi nyeupe inaenda spiral
Ugali inapata certificate, waiter leta sosa

(Chorus)

Verse 2:

Naanza kusakata ugali, namega ugali hapo kwa ngotitsa
Halafu namwona wepukhulu, kumbe alikuwa upande ule wa meza
Waiter anamkaribia anamwuliza nikupe nini Bwana
Wepukhulu anasema, ugali sosa na kadhalika
Waiter anasema excuse me? Wepukhulu anazusha
Mabouncer wakambeba juu, wakamtandika, chonga viazi

(Chorus)

Verse 3:

Sasa wasee iko hivi, tabia mbaya lazima tutawacha
Tunataka baraka zake Mungu, lakini tunakataa Mungu mwenye baraka
Tunataka tupate uponyaji lakini tunakataa Yesu mwenye kuponya
Tunapenda sana miujiza lakini hatumpendi Mungu mwenye kutenda
Ni lazima tutatubu wapendwa, tubadili mienendo tumtafute Mungu
Ukidharau mambo hii nasema, haki roho safi utachonga viazi

Ee Bwana ninakupenda (Oh Father I love You) Lyrics by New Life Crusade Choir

2 Comments


Ee bwana ninakupenda nakupenda, Ninayo kila sababu baba ya kukupenda
(Oh Father I love You, I have every reason to love You)
Umenitendea mengi ya ajabu, Hata kulipa siwezi baba pokea sifa
(You have done many amazing things, that I cannot repay you, Father receive praise Father) (Repeat)

Chorus:
Nakupenda Baba, nakupenda (I love You Father, I love You)
Kila ninapokutafakari mimi natetemeka (Everytime I ponder on it, I tremble)
Kwanini unidhamini mimi mwanadamu (Why did you value me a mere human?)
Ninajua ni kwa neema tu umenipenda ( I know it is by Grace that you love me)(Repeat)

Upendo wako kwangu ni maalum, siwezi kulinganisha kamwe nao mwingine
(Your love to me is special, I cannot compare to another one)
wewe ni wa thamani maishani, Nisaidie nisikuache nisonge mbele
(You are valuable to my life, help me to not leave you in my journey) (Repeat)

(Chorus)

Asubuhi ninaona fadhili zako, Na mchana ninashuhudia upendo wako
(In the morning I see your goodness, and during the day I witness your love)
Na usiku ninaona kupumzishwa, Kila wakati mimi naona kufarijika
(At night I see your rest, everytime I am comforted) (Repeat)

(Chorus)

Nakaza Mwendo (I Press On) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


Verse 1:
Nafurahia mateso yangu, nafurahia mateso yangu
(I rejoice in my persecutions)
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba
(Though this body be destroyed, I’ll get another from the Father)
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba
(Though this body be destroyed, I’ll get another from the Father)

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni (I press on to reach heaven)
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana (I give my life to the Lord)
Nauone, uzuri wa bwana (That I may see his goodness) x2

Taabu na matatizo, hakuna (No more troubles and trials)
Kiu wala njaa, hakuna (No more thirst or hunger) x2

Verse 2:
Lakini mji ule taa yake, ni mwana kondoo (But in the city its light is the lamb)
Milele mji ule hauitaji, jua wala mwezi (Forever it does not need the sun or the moon)

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida (I know life is a burden, to die is to gain)

(Chorus)

Verse 3:
Lakini waongo na wazinzi, hawataingia (But the liars and fornicators, shall not enter)
wala waabudu sanamu, hawataingia (Neither will the idolaters enter) x2

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida (I know life is a burden, to die is to gain)

(Chorus)

Yesu Nakupenda (I Love You Jesus) lyrics by Rose Muhando

3 Comments


(Sung in Swahili)

Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda(My Lord Jesus I love you) x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda (As you loved me first, I love you)
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda(Then again you gave up your life, I love you)
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda (As you loved me first, I love you)
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda(Then again you gave up your life, I love you)
Yesuuuu, yesu (Jesus)

Msalabani dhambi zangu ulichukua,(You took my sins at the cross)
Kufika kalivari Bwana ulizitua(At calvary Lord you relieved me)
Nami niwekwa huru ninakwimbia,(Now I am free I praise you) (Repeat)

Nikufananishe na nani mwokozi wangu,(Who do I liken you to my saviour?)
Naona fahari mimi ninakuimbia(I am priviledged to praise you)
Nani asimame badala yako,(Who can stand in your stead?)
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako(There’s no one but you) (Repeat)

Nafahamu Yesu anipenda mimi (I know that Jesus loves me)

(Chorus)

Nilipokuwa kwa shetani niliugua,(When I was of the devil I suffered)
Ndugu na jamaa zangu walinikimbia(My family and friends ran away from me)
Lakini yesu wa huruma ukanihurumia,(But merciful Jesus was merciful to me)
Nikufananishe na nani mwokozi wangu,(Who do I liken you to my saviour?)
Naona fahari mimi ninakuimbia(I am priviledged to praise you)
Nani asimame badala yako,(Who can stand in your stead?)
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako(There’s no one but you)

Nafahamu Yesu anipenda mimi (I know that Jesus loves me)

(Chorus)

Kwimake eeh, kwimake weh,Kwimake weeh, kwimake eh
Kwimake mundewa Yesu,oh kwimake eh
kunilapa kwe ruhoma baba, oh kwimake weh
kunilapa kwe ruhoma baba, oh kwimake weh
Kwimake baba, kwimake baba, Kwimake baba, kwimake baba
Kwimake mundewa baba,oh kwimake eh
Jaga kyala, jaga kyala, jaga kyala baba, jaga kyala
Asante mwokozi wangu, uh asante eh,Asante mwokozi wangu, uh asante eh

Umeniandalia Meza (You Have Prepared a Table) lyrics by Marion Shako

1 Comment


(Sung in Swahili: The Shepherd’s Psalm – Psalm 23)

Bwana mchungaji wangu, sitapungukiwa (The Lord is my Shepherd, I shall not Want)
katika malisho ya majani, mabichi hunilaza (He makes me to lie down in green pastures)
Kwa maji matulivu, yeye huniongoza (He leads me beside the still waters.)
Kwa uvuli wa mauti, sitaogopa kamwe (Though I walk through the valley of the shadow of death, I shall not be afraid)

Repeat:
Umeniandalia, meza mbele yangu (You have prepared a table before me)
Machoni pa watesi wangu, Bwana huniongoza (Before my enemies, Lord )
Huisha nafsi yangu, katika njia za haki (He leads me in the paths of righteousness)
Kwa ajili ya jina lako, wewe upo nami (For His name’s sake, You are with me) (Repeat)

Nimekukimbilia, Baba Mungu wangu (I have run to You, Father my God)
Nisiaibike, mbele za watesi wangu (That I may not be ashamed before my enemies)
Wewe upo nami, gongo na fimbo yako (You are with me, Your rod and Your Staff)
Vyanifariji Baba, Sitaogopa kamwe (Comfort me Father, I shall not be afraid)

(Refrain)

Umenipaka mafuta, kichwani mwangu (You anoint my head with oil)
Kikombe kinafurika, machoni pa watesi wangu (My cup runs over, in front of my enemies)
Wema nazo fadhili, zitanifuata (Surely goodness and mercy shall follow me)
Siku zote za maisha yangu, nyumbani mwako milele (All the days of my life; In Your House forever)

Older Entries Newer Entries