Advertisements

Sikuachi Tena (I Won’t Leave You Again) Lyrics by Zabron Singers

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Tunaishi kwa nguvu ya Mungu, Ye ndo katuweka hapa
(We live by God’s Power, He placed us here)
Kila hatua tunapitia, ye ndiye mlinzi wetu
(He guards all the steps we take)
Asubuhi ifikapo, hujua siku itaenda vipi
(When morning comes, he knows how the day will go)
Je n’tavuka salama, mchana jioni hata usiku
(Will I cross safely the, morning, evening and night?)
Kwa dakika,sekunde hujua siku itaenda vipi
(By minutes and seconds, he knows how the day will go)
Kupata na kokosa, ajua mimi n’tapata nini
(Receiving and Losing, He knows what I will get)
Kulala, kuamka, ajua mi n’taamka vipi
(Sleeping, and rising, he knows how I will wake)
Maisha yetu yote, Mungu ndiye anazo siri zetu
(The Lord knows the secret of all our lives)

Refrain:
We ni Mungu wangu, sikuachi tena
(You are my God, I will not leave You again)
Nikuwepo leo ni rehema zako zaniwezesha
(Me being here today, is through Your Mercies)
Sina haki mimi, kujisifu tena
(I do not have the right to boast of myself)
Kwani bila wewe hakika mimi singekuwa hivi
(For Without You, truly I would not be this way) (Repeat)

Mwanga wangu wa njia na nyota katika maisha yangu
(The Light to my path and the Star in my life)
Ye ni Mungu wa nuru, ushindi hata vitu vyote vyake
(He is the God of light, victory and all things are His)
Upatacho shukuru, ni Mungu ndiye kakuweka hapo
(Be thankful for what you get, it is God who placed you there)
Usisahau kumtumikia bado ungali hai
(Do not forget to serve Him, while you are still alive)

Kumbuka kuna siku utadaiwa kwa matendo yako
(Remember there is a day you will give account for your actions)
Iwe jema, kwa baya, watu pia umewatenda vipi?
(For good or for ill, How have you treated others?)
Je wazitumiaje baraka ulizopewa na Mungu?
(How are you using the blessings you were given by God?)
Suluhisho pekee, ni Mungu tumpe maisha yetu
(The only solution, is to give God our lives)

(Refrain)

Advertisements

Kama Si Wewe (If Not For You) Lyrics by Goodluck Gozbert

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Na wala sio sababu ya jina langu (It is not because of my name)
Wala sio sababu ninavaa (Neither is it because of how I dress)
Najua sio sababu ya sadaka zangu (I know it is not because of my offerings)
Oh, maana ndio ninashangaa (Oh, that is why I am amazed)
Nilijua kwamba nimeshapoteza nafasi (I knew I had lost my space)
Mimi ni nani kwani? Nakosa neno kusema (For who am I? I am lost for words)
Unisamehe, sikujua unanipenda hivi (Forgive me, I did not know you loved me thus)
Umefanya bure, sawa upendavyo (You have made it free, according to your will)
Umeruhusu niwe, vile upendavyo (You have permitted me to be, the way you will it)

Refrain:
Nitakushukuru tu, kwa neema (I will thank You, for the Grace)
Asante tu, kwa wema (Thank you, for the Goodness) (Repeat)
Maana kama si wewe (For if it was not for You)
Kama si wewe ningekuwa wapi? (If not for You, where would I be?) (Repeat)
Wacha machozi yanitirike tu (Let my tears fall)
Wacha kilio nikulilie Mungu (Let my cry be to You, Lord)

Natafuta cha kunitenga nawe, bado sijaona (I have yet to find what could separate us)
Nilishakatwakatwa moyo na kupondwa na wanadamu (I have been heart broken by people)
Wao wataniambia nini, nikiwa nawe? (But what can they tell me, if I am with You?)
Leo wataniambia nini, nikiwa nawe? (what can they tell me today, if I am with You?)
Pesa huitwa sabuni, ila maji ni wewe (Money is called the soap, but You are the water)
Unioshe Bwana, nitakase (Wash me Lord, cleanse me)

(Refrain)

Hata Hili Litapita (This Too Shall Pass) Lyrics by Dr Ipyana Ft. Paul Clement

Leave a comment(Sung in Swahili)

Nitayainua macho yangu nitazame, milima
(I will lift up my hills to the mountains)
Msaada wangu utatoka wapi?
(Where my does my help come from?)
Msaada wangu ni katika wewe (My help is in You)
Usiyeacha nipotee (Who will not let me go astray)
Chini ya msalaba wako (Beneath Your Cross) (Repeat)

Refrain:
Hata hili litapita (This too shall pass)
Kama yale yalivyopita (As the other ones passed)
Chini ya msalaba wako (Beneath Your Cross) (Repeat)

Chini ya uvuli wako najisitiri (I hide myself under your shadow)
Mbali nazo shida za maisha (Far away from life’s troubles)
Nifunike na Pendo Lako (Cover me with Your Love)
Chini ya msalaba wako (Beneath Your Cross) (Repeat)

(Refrain)

Way Maker Swahili Medley Covers by Angel Magoti

1 Comment


(Languages: English, Swahili)

Kuliko Jana Cover
Bwana ni mwokozi wangu (The Lord is my Savior)
Tena ni kiongozi wangu (He is also my Shepherd)
Ananipenda leo, kuliko jana (He loves me today, even more than yesterday)
Baraka zake hazikwishi (His blessings are unending)
Si kama binadamu, habadiliki (He is not like a man to change)
Ananipenda, leo kuliko jana (He loves me today, more than yesterday)

Way maker Cover
You are here, moving in our midst
I worship you, I worship You
Uko hapa, umetuzingiria — Repeated in Swahili
Nakuabudu, nakuabudu

Refrain:
Mtengeneza njia (Way Maker)
Mfanya miujiza (Miracle worker)
Mtunza ahadi (Promise keeper)
Mwanga kwenye giza (Light in the darkness)
Ndivyo ulivyo (That is who You Are) (Repeat)

You are here, touching every heart
I worship You, I worship You
Uko hapa, waponya wenye shida — Repeated in Swahili
Nakuabudu, nakuabudu

Excess Love Cover
Jesus You love me too much oh
Jesus You love me too much oh
Jesus You love me too much oh
You love is kind, Your love is Strong
Nakusifu, nakuabudu (I praise You, I worship You)
Natukuza Jina lako (I glorify Your Name)

(Refrain)

In Your name we overcome
In Your Name there’s victory
Jina lako lina nguvu nyingi (Your Name is Powerful)

The Name of Jesus, Higher than other names
King of all kings, no other name like His
Jina la Yesu, kubwa kuliko yote (The Name of Jesus, Higher than other names)
Mwanzo na mwisho, hakuna kama yeye (The beginning and the end, there is none like Him)
Hakuna kama yeye (There’s none like Him)

Mighty Man of War / My Beautifier Covers
Mighty man of war, Lion Judah
We bow down and worship You
My beautifier, You’ve taken away my shame
You’ve taken away my pain
You’ve made me just like You

The Name of Jesus Cover
I call Your Name, Jesus
Call His Name, Jesus
The Healing Name, Jesus
Oh, Jesus
Anaitwa nani? Yesu (What is His Name? Jesus)
Mfalme wa wafalme, Yesu (King of kings, Jesus)
Mwanzo tena mwshisho, Yesu (The beginning and the end, Jesus)
Mponyaji, Oh Yesu (Healer, Oh Jesus)

Your Name is so Powerful, Jesus
The healing Name, Jesus
The mighty Name, Jesus
Call His Name, Jesus
In every situation, Jesus
It doesn’t matter what You’re passing through. Jesus
Call His Name, Jesus
Oh Jesus

I Surrender Lyrics by Angel Benard

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Sikupi mipaka tena (I will not set boundaries on You again)
Chukua nafasi Bwana (Take the space, Lord)
Miliki kila chumba ndani yangu (Occupy every room in me)
Sikupi mipaka tena (I will not set boundaries on You again)

Panga na pangua (Arrange and re-arrange)
Yape yote sura yako (Make everything to be like You)
Acha nifurike wewe (Let me overflow with You)
Wewe tu (Only You)

Panga na pangua (Arrange and rearrange)
Yape yote sura yako (Everything to be like You)
Siwezi bila wewe (I cannot without You)
I surrender, I surrender
Sikupi mipaka tena (I will not set boundaries on You again)
I surrender

Umenijua toka kale (You have known me from before)
Kabla kuumbwa kwangu (Before I was even created)
Nitawezaje bila wewe? (How can I succeed without You?)

Hatua zangu bila wewe (My steps without You)
Ni bure nataishia (Is useless, and I will end up)
Uharibifuni (In destruction)
Ninakuhitaji (I need You)

I surrender, I surrender
Sikupi mipaka tena (I will not set boundaries on You)
I surrender (Repeat)

I surrender, I surrender
Sikupi mipaka (I do not set boundaries on You)

Unaniona (You See Me) Lyrics by Walter Chilambo

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Kama Mungu angechangua watu wake (If God selected His people)
Mimi singekuwepo duniani (I would not be here on earth)
Kama Mungu angechagua watakatifu (If God selected the Holy ones)
Mimi singekuwepo duniani (I would not be here on earth)

Refrain:
Mimi binadamu, wala si malaika (I am but a human, not an angel)
Mengi nimekosea na kukuchukiza (I have wronged and offended You)
Mi nafanya mambo yasiyo stahili (I have done things I should not have)
Nimevuruga vuruga mipango yako (I have disrupted Your plans)
Wanihurumia (Yet You have mercy on me)
Mbele ya macho ya wanadamu (Before human eyes)
Nilikuwa nikijificha (I was hiding)
Kumbe wewe waniona (But You see me)
Kwa kujifanya mtakatifu (By pretending to be Holy)
Tena bingwa mkarimu (And a generous victor)
Nilikuwa/(Kwenye ibada) mnyenyekevu (I was/in worship humble)
Tena mpole sana (Also submissive) (Repeat)

Kumbe Mungu, unaniona/unionae (Truly God You see me/who sees me)
Macho yako, yanitazama/yanitazamae (Your eyes gaze at me/sees me)
Sikio lako, yanisikia (Your ear, hears me)
Siwezi jificha (I cannot hide) (Repeat)

Sasa nimetambua, mbivu na mbichi ni zipo (I have now learned to differentiate)
Sasa ninaelewa, njia salama ni wapi (Now I know where the true path lies)
Na nimejua bila ya wewe sifiki (And have understood, without You I will not arrive)
Hata nikila pasipo neno lako sishibi (Even if I eat without Your word, I am not satisfied)

Neema yako, ila kwa neema yako (Your Grace, it’s only by your Grace)
Upendo wako, kwa upendo wako (Your Love, by Your Love)
Rehema zako zimeniimarisha tena (Your mercies reestablishes me) (Repeat)

(Refrain)

U mwendo Gani Nyumbani? (How Far from Home?) Lyrics – A Hymn

Leave a comment


(Sung in Swahili – A Hymn)See Notes below

U mwendo gani nyumbani? (How Far from Home?)
Mlinzi akanijibu (The watchman spake)
“Usiku sasa waisha (“The long, dark night is almost gone)
Macheo karibu (The morning soon will brea.)
Usihuzunike tena (Then weep no more)
Bali ulemee mwendo (But speed thy flight)
Hata ushike ufalme (Till thou shalt reach the realms of light)
Kule mwangani juu (In everlasting day)
Na tena niliuliza (I asked again)
Nchi yote ikajibu (The earth with one voice, made reply)
“Sasa mwendo watimia (“Time’s wasting sands are nearly run)
Milele karibu (Eternity is nigh)
Usihuzunike tena (Then weep no more)
Ishara kuu zasonga (Portentous sights are thick’ning round)
Na viumbe vyangojea (The whole creation, waiting, groans)
Sauti ya Bwana (To hear the trumpet sound)

Nikamuuliza shujaa (I asked the warrior on the field)
Ndivyo kanitia moyo (This was his soul-inspiring song)
“Shikilia mapigano (“With courage bold, the sword I’ll wield)
Kitambo yaisha (The battle is not long)
Usihuzinike tena (Then weep no more)
Kazi ifanywe kwa moyo ( But well endure the conflict)
Tumeahidiwa na tunu (For this we know, the prize is sure,)
Tuishaposhinda” (When victory is won.”)

Siyo mbali na nyumbani (Not far from home! )
Fikara tamu njiani (O blessed thought!)
Latupoza roho nalo (The trav’ler’s lonely heart to cheer)
Lafuta machozi (Which dried the mourner’s tear )
Usihuzunike tena (Then weep no more)
Kitambo tutakutana (Since we shall meet)
Wenye furaha kamili (Our joys complete)
Nyumbani mwa Baba (Safe in our Father’s home)

Usihuzunike tena(Then weep no more)
Kitambo tutakutana (Since we shall meet)
Wenye furaha kamili(Our joys complete)
Nyumbani mwa Baba (Safe in our Father’s home)

Notes:
The English Hymn was modified to match the Swahili translation.
Original Hymn Lyrics by Annie Rebekah Smith (1853)

Older Entries Newer Entries

%d bloggers like this: