Ombi Langu (My Prayer) Lyrics by Magena Main Youth Choir

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ombi langu Bwana nifike kwako (My prayer Lord, is to reach to You)
Ijapo njia zangu ni nyembamba (Though my paths be narrow)
Nitembee nawe Yesu Mwokozi wangu (To walk with You, Jesus my savior)
Dhoruba zijapo nitazishinda (I shall conquer the storms that come my way)

Refrain:
Mtakatifu Mungu mwenyezi (Holy God Almighty)
Alfajiri sifa zako tutaimba (We will sing Your praises at dawn)
Malaika wengi wanakuabudu (Host of Angels worship You)
Elfu maelfu wanakusujudu (Thousands and tens of thousands bow before You)
Ingawa giza linatuficha (Though the darkness hide us)
Fahari tusione (We should not be proud)
Wewe utatuwezesha mbinguni (For You will lead us unto heaven)
Makao ya raha (The home of joy)

Nitembee nawe Mungu (To walk with You God)
Unene nami kwa upole (Speak to me gently)
Ingawa njia sioni (Though I do not see the path)
Maana dhoruba baharini (For the sea is stormy)
Mitego ya miguu elfu (And there are traps for a thousand lengs)
Ukinishika mkono (But if You hold my hands)
Anasa kwangu hasara (Earthly luxuries for me are meaningless)
Tautika msalaba (I shall carry the cross)
Hata mji wa Zayuni (Until the city of Zion)
(Mimi) Nitapata pumziko (Where I shall find rest)

Repeat: (Mimi) Nitapata pumziko (Where I shall find rest)
Ule mji wa Zayuni (In that City of Zion)
Kwetu mji wa Zayuni (Our City of Zion)

(Refrain)

Mungu Wangu (My God) Lyrics by Magena Main Youth Choir

1 Comment


(Sung in Swahili)

Mungu wangu mbona umeniacha? (My God why have You forsaken me?)
Mbona u mbali na kuugua kwangu, Baba? (Father, Why are You far from my groaning?)
Wote wana-oniona hunicheka (All who see me mock me)
Nakulilia, nakusihi unijibu (I cry unto You, I plead for You to answer me)
(Repeat)

Refrain:
Najua mtetezi yu hai (I know my Redeemer lives)
Kamwe sitakata tamaa (I shall never give up)
Aijua njia niendayo (He knows my path)
Ataniongoza milele (He will guide me forever)
Akisha n’tatatoka dhahabu (After my test, I shall emerge as gold)
Baada ya dhiki nitamwona muumba wangu (After my trials, I shall see my Creator)
(Repeat)

Mashtaka yangu yana uchungu mwingi (My complaint is full of bitterness)
Laiti ningelifika kwa Mungu wangu! (If only I could reach my God!)
Hakika ningenena na Mwenyezi Mungu (Truly I would speak to the Almighty God)
Ningeliweka dua langu mbele yake (I would state my case before Him)

(Refrain)

Hema za wabukonyi zafanikiwa Baba (Father, the tents of the wicked are prosperous)
Wasindao(?) hunawiri Bwana (Lord, those who provoke you are successful)
Mipango ya wenye dhambi nayo hunawiri (The plans of the wicked prosper)
Basi tumaini langu liko wapi? (Where then is my hope?)
(Repeat)

(Refrain)

<span>%d</span> bloggers like this: