(Sung in Swahili)

Kisa cha Mafarisayo chashangaza (The case of the Pharisees is amazing)
Walimshika Yesu, wakamsulubisha (They arrested Jesus, and crucified Him)
Wakamlaza kaburini, kisha wakaweka jiwe kubwa (They laid Him in a grave, and placed a large rock)
Wakajua yamekwisha (And thought that it was finished)
Ndivyo watu wengi, maadu zetu (That is similar to many people – our enemies)
Wanayaweka mawe, wakidhani wamezifunga njia (They put rocks thinking they have blocked our way)
Wanaiweka mitego, ili tuanguke (They place traps, so that we fall)
Wasilo lijua: tumezungukwa na malaika (What they do not know: we are surrounded by angels)
Wasilo lijua: tumezungukwa na malaika, wa nuru (What they do not understand: we have been surrounded by an angel of light)

Refrain:
Ni malaika aliondoa jiwe kaburini (It is an angel who removed the stone blocking the grave)
Mwana wa Mungu asiye na hatia kainuliwa (Son of God with no sin was lifted up)
Jaribu linaweza kuwa kubwa kwetu (Temptations maybe many to us)
Ila Mungu huleta mlango wa kutokea (But God opens doors for us to escape)
Jaribu linaweza kuwa kubwa kwetu (Though the temptations may be great for us)
Ila Mungu huleta mlango wa kutokea (But God brings new exits for us)

Walimuua Yesu, kisha wakaweka jiwe (They killed Jesus, and placed a rock)
Kubwa, asiweze kufufuka (A large rock, that He should not rise)
Asikari nao walikesha kule (The guards kept a night vigil)
Mwili wake usipate kuibiwa (So that His body would not be stolen)
Maadui hata wakeshe, neno la Mungu linatimia (Even if our enemies keep a vigil, the world of God will be fulfilled)
Mipango yake hukamilika, ahadi zake hazichelewi (His plans will be completed, and His promises are never late)
Ni mwaminifu Mungu wetu, ni mwaminifu (Our God is faithful, He is faithful)
Ni mwenye Nguvu Mungu wetu, yeye hashindwi (Our God is powerful, He cannot be defeated0)

(Refrain)