Mwema (Good) Lyrics by Paul Clement ft. Bella Kombo

4 Comments


(Sung in Swahili)

Wema wako, si kwa wakati wa furaha tu
(Your Goodness, is not only present in times of joy)
Wema wako, pia wakati hata wa majonzi
(Your Goodness is also present in times of grief)
Wema wako, haupimiki, kwa majira fulani tu
(Your Goodness cannot be measured in time)
Wema wako, ni kila wakati, na kila nyakati
(Your Goodness is present at all times, in all seasons)
Hata sasa ni mwema, tunapoimba ni mwema
(Even now He is Good; when we sing He is Good)
Tunapolia ni mwema, tunapocheka ni mwema
(When we weep, he is Good; when we laugh, He is Good)
Tunapopanda ni mwema, tunapovuna ni mwema
(When we plant, He is Good; When we harvest, He is Good)

Refrain:
Wewe ni mwema, u mwema, wewe ni mwema
(You are Good, You are Good, You are Good)
Wewe ni mwema, u mwema, wewe ni mwema (Repeat)
(You are Good, You are Good, You are Good)
Unatupenda x2 Wewe ni mwema (Repeat)
(You love us x2 You are Good)

Wema wako, ni kama mchanga, siwezi kuhesabu
(Your Goodness is like the soil; I cannot count it)
Wema wako, ni kama maji, yanayomiminika bila kukoma,
(Your Goodness is like the water; that flows without ceasing)
Mtu akinge, ama asikinge, hayataacha kutoka
(Should someone obstruct it or not, it will not cease)
Hata sasa ni mwema, tunapoimba ni mwema
(Even now, He is Good; When we sing He is Good)
Tunapolia ni mwema, tunapocheka ni mwema
(When we weep, He is Good; when we laugh, He is Good)

(Refrain)

Siogopi (I’m Not Afraid) Lyrics by Paul Clement

1 Comment


(Sung in Swahili)

Siogopi kuchelewa (I’m not afraid of being late)
Sababu Mungu wangu hachelewi, wala hawai
(Because God does not delay, nor does he ever)
Siogopi mateso yangu (I’m not afraid of my tribulations)
Sababu ye ananipeleka, kwenye ukuu wangu
(For He is taking me to my greatness)
Siogopi kudharauliwa (I’m not afraid of being despised)
Maana ndiko kunakonipa heshima yangu
(Because there is where I receive my honor)
Siogopi adui zangu (I’m not afraid of my enemies)
Maana najua ni adui wa Mungu wangu
(For I know that they are the enemies of my God)
Siogopi hivi vita vyangu (I’m not afraid of my battles)
Maana ndivyo vinaivyonipa ushindi wangu
(For they are they that will bring me my victory)

Refrain:
Siogopi, Siogopi! (I’m not afraid)
Siogopi, Siogopi! (I’m not afraid)
I’m not afraid, I’m not afraid!
I’m not afraid, I’m not afraid! (Repeat)

Nimepewa mamlaka (I have been given authority)
Siogopi nge na nyoka (I’m not afraid of the scorpion or the snake)
N’tawakanyaka vichwa vyao (I shall crush their heads)
Haitanidhuru sumu zao, yaani maneno yao (Their poison will not harm me, meaning their words)
Siogopi kutembea kwenye giza (I’m not afraid of walking in the darkness)
Maana mi ni nuru ninaangaza (For I am the light that lights the way)
Siogopi kusimama juu ya mlima (I’m not afraid if standing on the hill)
Maana najua siwezi sitirika (For I know I shall not be hidden)
Siogopi moto, moto sababu (I am not afraid of the fiery fire, because)
Sababu, lazima nipite mimi dhahabu (I have to pass through to be refined as gold)
Ili nisimame, niwe imara, niwe kinara (So that I can stand, firmly, to be a rock)
Siogopi moto, moto sababu (I’m not afraid of the fiery fire, because)
Sababu, lazima nipite mimi dhahabu  (I have to pass through to be refined as gold)
Niwe hodari, niwe jasiri, niwe kamili! (To be strong, to be brave, to be complete!)

(Refrain)

Siogopi, Mungu uko na mimi (I’m not afraid, for God you are with me)
Mungu uko na mimi, Mungu uko na mimi
(God You are with me, You are with me God)
Siogopi, Baba uko na mimi (I’m not afraid, Father You are with me)
Baba uko na mimi, Baba uko na mimi
(Father You are with me, You are with me Father)
Uko na mimi, uko na mimi
(You are with me, You are with me)

Yuko Mungu (There is God) Lyrics by Alice Kimanzi ft Paul Clement

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Spoken:
Mungu anaweza kufanya njia jangwani (God can make a way in the jungle)
Na mito ya maji nyikani (And rivers in the desert)
Kama alifanya masika na kiangazi (Like he created Spring and Summer)
Anaweza kubadili majira, pia na wakati (He can change seasons and time)

Giza, totoro yanizingira (Deep darkness surrounds me)
Miale haijanifikia (The rays (of sunshine) does not reach me)
Ilhali kumekucha, pambazuka (Even though it is dawn, there is light)
Imani, yashuka yadidimia (My faith drops and weakens)
Amani nayo yafifia (And peace flees from me)
Eloi, Lamasabaktani (Elo, Lamasabakhtani?)

Refrain:
Yuko Mungu, anayeweza (There is God who is able)
Yuko Mungu, anayetenda (There is God able to do)
Mwamini Yeye! (Trust in Him!)
Mwamini Yeye, utoaibika (Trust in Him, you will not be ashamed)

Giza likiwa ni nzito (When darkness is heavy)
Bwana atawasha taa (The Lord will shine a light)
Sababu Mungu mwenye Amandla (Because God is the one with the Strength)
Atarejesha amani, (He will restore your peace)
Atarejesha furaha (He shall restore your joy)
Ulivyovipoteza kwa muda mrefu (The one you’ve lost for a long time)
Atarejesha Amandla (The Powerful one will return it)

(Refrain)

Repeat: Mungu pekee Ndiye awezaye (Only God is able)
Pale ninaposhindwa, nani wa kuniwezesha? (When I am unable, who grants me strength?)
Nikiwa vitani, nani wa kunishindia? (When I’m in battle, who is my champion?)
Napokuwa mdhaifu, nani wa kunipa nguvu? (When I am weak, who gives me strength?)
Ninapotia shaka nani wa kuniongoza (When I am doubtful, who leads me?)

Yuko Mungu, Mungu Yupo (There is God, God is there)
Oh…

(Refrain)

Atainyosha Njia Yako (He Shall Straighten Your Path) Lyrics by Paul Clement ft. Calvin John

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Atainyosha njia yako (He shall straighten your path)
Atainyosha njia yako (He shall straighten your path)
Ina mabonde mengi (It truly has many valleys)
Ina vikwazo vingi (It has many obstacles)
Atainyosha njia yako (He shall straighten your path) (Repeat)

Bridge:
Njia yako ina mabonde (Your paths has many valleys)
Mapito nayo mengi, ila usiogope (Many obstacles, but do not fear) (Repeat)

Usiogope, usiogope (Do not be afraid, do not fear)
Mungu anainyosha njia yako (God will straighten your path)

(Bridge + Refrain)

Hata Hili Litapita (This Too Shall Pass) Lyrics by Dr Ipyana Ft. Paul Clement

Leave a comment(Sung in Swahili)

Nitayainua macho yangu nitazame, milima
(I will lift up my hills to the mountains)
Msaada wangu utatoka wapi?
(Where my does my help come from?)
Msaada wangu ni katika wewe (My help is in You)
Usiyeacha nipotee (Who will not let me go astray)
Chini ya msalaba wako (Beneath Your Cross) (Repeat)

Refrain:
Hata hili litapita (This too shall pass)
Kama yale yalivyopita (As the other ones passed)
Chini ya msalaba wako (Beneath Your Cross) (Repeat)

Chini ya uvuli wako najisitiri (I hide myself under your shadow)
Mbali nazo shida za maisha (Far away from life’s troubles)
Nifunike na Pendo Lako (Cover me with Your Love)
Chini ya msalaba wako (Beneath Your Cross) (Repeat)

(Refrain)

Older Entries

%d bloggers like this: