Chorus:
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote

Verse 1:
Akisema atakubariki, wala usitie shaka
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
Mipango yake ya ajabu, tena haibadiliki
Akisema atakuinua, ndiye mwenye kuinua
Akisema atakupa mtoto, katika umri wowote
Aliwapa Sara na Ana, lipi asiloweza

(Chorus)

Verse 2:
Akisema atakubariki, watoto wako waelimike
Wapate na shahada nyingi, hakuna atakayezuia
Akisema utapona, hakuna atakayezuia
Mama aliyetokwa na damu alipona na kazi(?) yake
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
Atalinda afya yako, maana yeye ndiye mwenye afya

(Chorus)

Verse 3:
Watembelea miguu, hata baisikeli huna
Akisema uendeshe Musso, kesho utaendesha
Waishi nyumba ya matope, huna hata mavazi
Akisema atakubariki, majirani watashangaa
Akisema atakuinua, mbele ya adui zako
Atakuandalia meza ule unywe wakitizama

(Chorus) (repeat)

Advertisements