(Sung in Swahili)

Mwambie Baba shida zako maana yeye atazitatua
(Tell father your troubles for he will solve them)
Ukiwaambia majirani ye, masimango yatakufuata
(If you tell your neighbors, gossip will follow you)
Mwambie Yesu upitiayo maana yeye ayajua yote
(Tell Jesus your troubles for He knows all)
Alishinda kifo Masiya, nini pia asoweza shinda
(The Messiah defeated death, what will thwart him?)

Chorus:
Mwambie, mwambie, mwambie Baba shida zako
(Tell him, tell him, tell the Father your troubles)
Mwambie, mwambie, yote alikusikiza
(Tell him, tell him all he listens)
Mwambie, mwambie, mwambie Baba shida zako
(Tell him, tell him, tell the Father your troubles)
Mwambie, mwambie, Yeye atazitatua
(Tell him, he will solve them)

Ee mama unajisumbua, washika tama una huzuni
(You woman hold your chin in depression)
Unakosema juu ya shida zako we huwaambia majirani
(When you tell of your troubles you tell your neighbors)
Usiende kwa waganga, hawatosimamisha ndoa yako
(Don’t go to the witch-doctors: They won’t help your marriage)
Mwambie Yesu shida zako, waganga wataivunja
(Tell Jesus your troubles, Witch-doctors will break it)

(Chorus)

Usiwaambie walimwengu, yakusumbuayo ndugu yangu
(Don’t tell the world whatever troubles you my brother)
Yesu pekee ndiye aweza kuitatua shida yako
(Jesus only would help solve your troubles)
Mbona wasumbuka bure ukitafuta ushauri mwenzangu
(Why do you trouble yourself looking for solutions?)
Hebu soma hiyo Biblia, ina jawabu kwa kila jambo
(Read that Bible, it has a solution for every question)

(Chorus)

Advertisement