(Sung in Swahili)

Maisha magumu sana nimepitia ( I’ve passed through struggles in life)
Nikajaribu kutafuta msaada sikupata (I looked in vain for help)
Nikaendea wanadamu mwisho wakanidharau( I asked people until they despised me)
Kumbe msaada wa mwanadamu unatoka kwa Mungu(But our help is from God)
Nilijua ya kuwa wenye haki ya kubarikiwa( I thought the righteous will be blessed)
Kumbe baraka ni haki ya kila mmoja(But blessings is everyone’s right)
Nibebadili wazo langu namwelekea Mungu(My thoughts have changed towards Him)
Kwake msaada wangu unapatikana( There my help will be found)
Msaada wa mwanadamu ni wa muda mfupi(Man’s help is only for a short tim)
Nami zamu yangu wa kubarikiwa ee( It’s my turn to be fully blessed)

Chorus:
Wakati huu wa kubarikiwa ( This is the time of blessings)
Zamu ni yangu, sasa kupokea( It is my turn to receive blessings)
Nimechoshwa, na shida za dunia ( I am tired of the world’s troubles)
Napokea kwako, Ee Bwana kwako x2( So I receive from you, Lord)
Napokea kwako, Yesu napokea kwako( I receive from you Jesus)
Napokea kwako, Baba napokea kwako( I receive from you Father)

Nimeamua kwenda zaidi na zaidi ( I have decided to continually pursue)
Nimejipanga hadi nione matunda yake( I will keep on until I see his fruits)
Yale Mungu amewekeza ndani yangu (That which God has planted in me )
Najua Mungu yuko kazini kunikamilisha(I know God is working for its fruition )
Akisema nimebarikiwa, nimebarikiwa tu (If He says I’m blessed, then I’m blessed )
Hata ukipinga wewe leo mimi nimebarikiwa tu(Even if you deny is, I’m still blessed )
Mlima gani kuu sana usioung’oa?(What mountain is too great for You to uproot? )
Jaribu gani gumu sana usiloliweza?(What trials too hard for you to solve?)
Chozi gani zito kwako usilolifuta?(What tear is too heavy for you to wipe?)
Ombi gani kubwa sana usilolijibu? (What prayer is too great for you to answer? )

(Chorus)

Advertisement