(Sung in Swahili)
Daudi kasema,nilikuwa kijana sasa ni mzee (x2) (David said I was young now I’m old)
Sijawahi kuona mwenye ameachwa mimi (I have never seen the righteous forsaken)
Wala watoto wake kuombaomba mikate barabarani (Or their children begging bread)
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake wanadamu (God is faithful in his promises to us)
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake si kama wanadamu (He is faithful, not like man)
Akiongea Yesu ameongea, (When He speaks, Jesus has spoken)
Akikuahidia kitu, Baba ameahidi na ujasiri (When He promises,  it is done)
Atatenda kwa wakati wake (He will do it in season )
Ninamwita Bwana wa amani (I call unto the Lord of peace)
Ninamwita mfalme wa amani (I call unto the King of peace)
Ndio maana mimi ninaimba kwa sababu ya amani yake (I sing of his peace)
Ni uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba (What power can oppose my Father’s?)
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani (What power?)

Refrain:
Mfalme wa amani, mfalme wa amani uinuliwe (Prince of peace, be lifted up)
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu (My Lord you are good) x3

(Refrain)

Usilie, usilie, usiliwe wewe (Do not cry)
Usilie Bwana anakujua ndugu yangu (Do not cry my brother, The Lord knows you)
Amesikia kilio chako wewe mama (He has litened to your cry mother)
Unalia nini kwa wanadamu, mama yangu (Why are you crying to the worldly mother?)
Wanadamu hawatakusaidia na kitu (The worldly will not help you)
Wanadamu hawatakuwezesha kwa kitu chochote (They will not enable you)
Tunaye mmoja anayepanguza machozi ya watu wake(We have one that wipes our tears)
Ni yule mfalme wa amani (He is the Prince of peace)
Ni yule aliyesema yote imekwisha (He is the one who said “It is Finished”)
Mama unayoyapitia ni yeye anayeyaona (He knows what you’re going through)
anajua shida yako mama yangu (He knows your troubles, mother)
Anajua magumu yako baba yangu (He knows your hardship, father)
Ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia (Troubled? don’t go to the witchdoctors)
Ukiwa na magumu usiende kwa wafumu wa dunia (Troubled? don’t look for worldly solutions)
Muite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi (x2) (Call the King of peace, He answers prayers)
Ni uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba (What power can oppose my Father’s?)
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani (What power?)

(Refrain)

Mfalme wa amani, uinuliwe Bwana wangu (Prince of peace, be lifted my Lord)
yale unayotenda inashangaza dunia nzima (You works astonish the whole world)
Wanaokosa amani ndani ya nyumba zao wape amani (Those who lack peace at home, grant them peace)
Wanaokosa amani ndani ya kazi zao wape amani (Those who lack peace at work, grant them peace)
Ni wewe Bwana wa amani ya kudumu (You are the Lord with everlasting peace)
Ni wewe Bwana wa amani ya Afrika (You are the Lord of Africa’s peace)
Amerika wanalia amani (American’s cry for peace as well)
Tunawe Bwana mfalme wa amani (We have you Lord, King of peace)(x2)
Hakuna kitu kile kinachokushinda Bwana (There is nothing too hard for you my Lord)
Yeye Mfalme wa Amani (He is the prince of peace)

(Refrain)

Advertisement