(Sung in Swahili)

Je, umekumbuka kumuombea (Have you remembered to pray)
yule umpendaye? (for a loved one?)
Jamani twazingirwa na maovu mengi (We are surrounded by much evil)
Kwa hiyo inatupasa, kuombeana sana (So we need to pray for each other)

Mtoto wako, atoka asubuhi sana (Your child leaves early in the morning)
Kwenda shule, sokoni na kadhalika (To go to school, to the market and so on)
Apitapo kumejaa mabaya mengi sana (Wherever he passes lives much evil)
Mama, mwombee mtoto wako (Mother, pray for your child)

Refrain:Mwombee mtoto wako (Pray for your child)
Apitapo ajali ni mingi (Where he passes have been many accidents)
Mbwa wakali wamzingira (A lot of dangerous dogs surround him)
Siku hizi vibaka ni wengi (These days the rapists are many)
Oh, mwombee mtoto wako (Oh, pray for your child)

Ewe mama, watenganishwa (Mother you’ve been separated)
Na mume wako kaenda safari ya mbali kikakazi (Your husband has traveled for work)
Je, umemwombea Kule aliko mbali nawe? (Have you prayed for him wherever he is?)
We kumbuka amezingirwa na maovu mengi (Remember he is surrounded by much evil)

Refrain:Mwombee mume wako (Pray for your husband)
Kule nasikia kuna wachawi (I hear there are witchdoctors there)
Na wenzake kumwonea wivu (When others are jealous of him)
Keelewana na mabosi zake (For understanding with his bosses)
Afya njema asiugue (To enjoy a healthy life)

Ewe Baba watenganishwa (Father you have been separated)
Na mke wako kaenda safari ya mbali shuleni (Your wife has traveled for school)
Je, umemwombea kule aliko mbali nawe (Have you prayed for her wherever she is?)
We kumbuka amezingirwa na maovu mengi (Remember she is surrounded by much evil)

Refrain: Mwombee mke wako (Pray for your wife)
Kamwombee sana mke wako (Pray very much for your wife)
Aweze kufaulu shuleni (To be successful in school)
Majaribu mengi yampata (A lot of temptations follow her)
Uvumilivu kwa kila jambo (Perseverance in everything)

Oh, mwombee mtoto wako (Oh, pray for your child)
Oh, mwombee mume wako (Oh, pray for your husband)
Oh, mwombee mke wako (Oh, pray for your wife)

Advertisement