Furaha Tele (Great Joy) By Ambassadors of Christ Choir

2 Comments


(Sung in Swahili)

Kuna nchi pale ng’ambo ya ule mto (There is a land beyond the river)
Ni nchi nzuri na ya kupendeza (A beautiful land of bliss)
Ndio nyumbani kwetu (A land we call home)
Kuna nyimbo huko ni kuabudu daima (A land of continuous singing and praise)
Malaika wapiga tarumbeta (Where angels play harps)
Natamani ‘fika huko (I long to get there one day)

Refrain:
Furaha tele, Tukifika mbinguni (O what a joy, When we get to heaven)
Tutapita njia zilizopambwa nzuri za dhahabu (Treading beautiful streets of gold) Tutauimba, Wimbo mpya wa Musa (And sing a new song, A song of Moses)
Tukisema hozana hozana Yesu (Saying Hosanna Hosanna to Jesus)
Hallelujah abudiwa (Hallelujah be exalted) (Repeat)

Nikifika huko, nitapumzika kwa kweli (When I get there, I will finally rest)
Nitautua mzigo mzito (I will lay down my heavy burden)
Yesu anipokee (Jesus will receive me)
Nitaonana na, ndugu tul’opoteana (I will be reunited with departed brethren)
Sote tukusanyike mbele ya Yesu (And together we will be gathered before Jesus) Natuimbe nyimbo (Singing His praises)

(Refrain)

Tutatembea, shambani mwake Bwana (We will walk in the garden of the Lord)
Tuchune matunda tufurahie (With great joy we’ll gather fruits)
Tule mezani na Yesu (And dine with Jesus)
Atayapanguza, machozi tulolia (And He will wipe all of our tears)
Kifo kamwe hakitakuwepo tena (Death will be no more)
Tutakua washindi (For we will be victorious)

(Refrain)

Lyrics submitted by Caroline Jonathan

Parapanda ya Bwana (The Lord’s Trumpet) Lyrics by Ambassadors of Christ Choir

3 Comments


(Sung in Swahili)

Parapanda ya Bwana ii karibu (The Lord’s trumpet is near)
Parapanda karibu kusikika (The trumpet shall be heard soon)
Wazima wote watasikia (All who live shall hear it)
Na waliokufa wote wafufuke (Those who are dead shall rise)
Walomsubiri watavikwa taji zilizong’aa (Those who waited for Him will be crowned)
Bali waovu wataukimbia uso wake (But the evil shall flee His face)

Refrain:
Tutamwona mfalme wetu Yesu, akirudi (We shall see our kings’ return)
Tutafurahi, tupumzike, wote tuloshinda (We’ll rejoice and rest all who’ve conquered)
Nao malaika wote, wapige panda (The angels shall sound the trumpets)
Nyingi za ushindi (With resounding joy)
Na tutaruka mawinguni (And we shall rejoice in the clouds)
Tumlaki mfalme wetu (While meeting our King)

Watakaokuwa ni washindi,  Watafurahia ajabu (The winners shall rejoice)
Na majina yao yataitwa, Naye Yesu mwokozi wao (Their names called by Jesus their savior)
Wataruka kwa furaha angani (They shall jump for joy in the air)
Wakiongozwa naye Yesu (Led by Jesus)
Nyimbo tamu zitasikika angani (Sweet songs shall be heard)
Ndugu yangu usikose pale (My brother, do not miss it)

Utakuwa wapi siku hiyo ndugu? (Where will you be on that day?)
Utakuwa wapi siku hiyo? (Where will you be on that day?)
Mwokozi Yesu atakapoyaita (When our Savior Jesus shall call)
Majina yao aliowakomboa (The names of all He has saved)
Walio ya furaha mavazi katika damu ya Yesu (The ones who wear garments washed with His blood)
Wakavumilia hadi kufika mwisho (Those who persevered to the end)

(Refrain)

Ni Kwanini? (Why?) Lyrics by Ambassadors for Christ

11 Comments(Sung in Swahili)

Refrain:
Ni kwanini umeyaruhusu, (Why have you permitted)
Ee Mungu mwenyezi (Oh God Almighty)
Yatusononeshe moyoni (For our hearts to be troubled)
Kwanini unaruhusu (Why have you permitted it?)
Ona haya machozi; Tazama tunavyolia (Look at these tears; how we weep)
Twajiuliza sana Bwana (We ask ourselves Lord)
Ni kwanini uliyaruhusu (Why you permitted it)

Nikumbukapo usiku huo (When I remember that night)
Usiku wa huzuni nyingi (A night filled with sorrow)
Ulipokubali Bwana kwamba (When you permitted Lord)
Wenzetu wapumzike (That our friends should rest)
Najiuliza moyoni, (I ask in my heart)
Kwanini Bwana Mwenyezi (Why, Oh God almighty)
umeruhusu tusononeshwe kiasi (You’ve allowed us to suffer thus?)

(Refrain)

Mlipuko ni ghafla (An explosion is sudden)
Tulipovamiwa na mauti (When we were invaded by death)
Bwana ulimruhusu ndugu Gautane (Lord you allowed Gautane)
Aiage dunia (To leave the world)
Ndugu Amosi, Mansi kijana mnyenyekevu (Brother Amos, Mansi a humble brother)
Twawakumbuka wote – hatutawasahau (We remember them all – we shall not forget them)

(Refrain)

Twahuzunika Bwana, tena nawe wajua (We mourn Lord, you know this)
Lakini kwa hayo yote (But for all that)
Chukuliwa kwa matendo mema (Be lifted by your great works)
Uliyoyakubali wale watumishi wako (That you allowed your servants)
Wayatende katika siku hizo (To do in those days)
Chache za maisha (Those few days of their lives)

Twayakumbuka matendo yenu (We remember your works)
Mema yasiyoelezeka (The good works that cannot be counted)
Mliotena duniani (That you did while in the world)
Twawakumbuka tulivyoishi vizuri (We remember how we lived well)
Kwa muda mlikuwa nasi; hatutawasahau (In the time you were with us – we won’t forget)
(Repeat)

Tuombeane (Pray for Each Other) Lyrics by Ambassadors for Christ Choir

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Je, umekumbuka kumuombea (Have you remembered to pray)
yule umpendaye? (for a loved one?)
Jamani twazingirwa na maovu mengi (We are surrounded by much evil)
Kwa hiyo inatupasa, kuombeana sana (So we need to pray for each other)

Mtoto wako, atoka asubuhi sana (Your child leaves early in the morning)
Kwenda shule, sokoni na kadhalika (To go to school, to the market and so on)
Apitapo kumejaa mabaya mengi sana (Wherever he passes lives much evil)
Mama, mwombee mtoto wako (Mother, pray for your child)

Refrain:Mwombee mtoto wako (Pray for your child)
Apitapo ajali ni mingi (Where he passes have been many accidents)
Mbwa wakali wamzingira (A lot of dangerous dogs surround him)
Siku hizi vibaka ni wengi (These days the rapists are many)
Oh, mwombee mtoto wako (Oh, pray for your child)

Ewe mama, watenganishwa (Mother you’ve been separated)
Na mume wako kaenda safari ya mbali kikakazi (Your husband has traveled for work)
Je, umemwombea Kule aliko mbali nawe? (Have you prayed for him wherever he is?)
We kumbuka amezingirwa na maovu mengi (Remember he is surrounded by much evil)

Refrain:Mwombee mume wako (Pray for your husband)
Kule nasikia kuna wachawi (I hear there are witchdoctors there)
Na wenzake kumwonea wivu (When others are jealous of him)
Keelewana na mabosi zake (For understanding with his bosses)
Afya njema asiugue (To enjoy a healthy life)

Ewe Baba watenganishwa (Father you have been separated)
Na mke wako kaenda safari ya mbali shuleni (Your wife has traveled for school)
Je, umemwombea kule aliko mbali nawe (Have you prayed for her wherever she is?)
We kumbuka amezingirwa na maovu mengi (Remember she is surrounded by much evil)

Refrain: Mwombee mke wako (Pray for your wife)
Kamwombee sana mke wako (Pray very much for your wife)
Aweze kufaulu shuleni (To be successful in school)
Majaribu mengi yampata (A lot of temptations follow her)
Uvumilivu kwa kila jambo (Perseverance in everything)

Oh, mwombee mtoto wako (Oh, pray for your child)
Oh, mwombee mume wako (Oh, pray for your husband)
Oh, mwombee mke wako (Oh, pray for your wife)

%d bloggers like this: