(Sung in Swahili)

Refrain:
Ni kwanini umeyaruhusu, (Why have you permitted)
Ee Mungu mwenyezi (Oh God Almighty)
Yatusononeshe moyoni (For our hearts to be troubled)
Kwanini unaruhusu (Why have you permitted it?)
Ona haya machozi; Tazama tunavyolia (Look at these tears; how we weep)
Twajiuliza sana Bwana (We ask ourselves Lord)
Ni kwanini uliyaruhusu (Why you permitted it)

Nikumbukapo usiku huo (When I remember that night)
Usiku wa huzuni nyingi (A night filled with sorrow)
Ulipokubali Bwana kwamba (When you permitted Lord)
Wenzetu wapumzike (That our friends should rest)
Najiuliza moyoni, (I ask in my heart)
Kwanini Bwana Mwenyezi (Why, Oh God almighty)
umeruhusu tusononeshwe kiasi (You’ve allowed us to suffer thus?)

(Refrain)

Mlipuko ni ghafla (An explosion is sudden)
Tulipovamiwa na mauti (When we were invaded by death)
Bwana ulimruhusu ndugu Gautane (Lord you allowed Gautane)
Aiage dunia (To leave the world)
Ndugu Amosi, Mansi kijana mnyenyekevu (Brother Amos, Mansi a humble brother)
Twawakumbuka wote – hatutawasahau (We remember them all – we shall not forget them)

(Refrain)

Twahuzunika Bwana, tena nawe wajua (We mourn Lord, you know this)
Lakini kwa hayo yote (But for all that)
Chukuliwa kwa matendo mema (Be lifted by your great works)
Uliyoyakubali wale watumishi wako (That you allowed your servants)
Wayatende katika siku hizo (To do in those days)
Chache za maisha (Those few days of their lives)

Twayakumbuka matendo yenu (We remember your works)
Mema yasiyoelezeka (The good works that cannot be counted)
Mliotena duniani (That you did while in the world)
Twawakumbuka tulivyoishi vizuri (We remember how we lived well)
Kwa muda mlikuwa nasi; hatutawasahau (In the time you were with us – we won’t forget)
(Repeat)