(Sung in Swahili)

Hadithi, Hadithi Njoo… (Story, Story come)

Kuna bwana mmoja wa kichaa (There was once a madman)
Alipenda kuomba chakula (Who liked to beg for food)
Kwa mama fulani, mama fulani (From a certain mother, a certain mother)
Siku moja yule mama alipanga amtilie sumu (One day the mother planned to poison him)
Yule wazimu akila afe, aondoke kabisa (The mad man to die, and disappear for good)
Kule njiani alipatana na watoto wa yule mama (On his way, he met the mother’s children)
Akawagawanyia, kile chakula (He divided the food among them)

Watoto wake wakala wakafa (Those children ate and died)
Yule wazimu akabaki mzima (The mad man was left alive)
Ishara kwamba unayoyatenda (A sign that what you do)
Unajitendea mwenyewe (You do for yourself) (Repeat)

Refrain:
Ukitenda mema (When you do good)
Unajitendea mwenyewe (You do it for yourself)
Ukitenda maovu (When you do evil)
Unajitendea mwenyewe (You do it for yourself) (Repeat)

Salimia watu, pesa huisha, gari hupata puncture (Greet people, Money and cars are fleeting)
Hivi ni vitu vya dunia (This are things of the world)
Hichi kidole nacho wanyoshea watu (This finger that I point at people)
Vingine vinne ninajinyoshea mwenyewe (There are four that I point at myself)
Hichi kidole nacho wanyoshea watu (This finger that I point at people)
Vingine vinne ninajinyoshea mwenyewe (There are four that I point at myself)

Ninaozongumza nao, juu ya wenzangu (The ones talk about my fellow men)
Wanazungumza nao, juu yangu mimi (They talk to them about me) (Repeat)

Tenda mema – ondoka uende (Do good, and leave)
A’lo na chuki na wewe mpende (The one with hate, love them instead)
Kwa sababu unayoyatenda (Because what you do)
Unajitendea mwenye (You do it for yourself) (Repeat)

(Refrain)